Rais Kibaki amjibu Odinga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kibaki amjibu Odinga

Discussion in 'Kenyan News and Politics' started by Rutashubanyuma, Feb 1, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Rais Kibaki amjibu Odinga

  Monday, 31 January 2011 19:41 newsroom  NAIROBI, Kenya
  RAIS Mwai Kibaki amemjibu Waziri Mkuu Raila Odinga, kuhusiana na madai yake kuwa hakuhusishwa kwenye mchakato wa uteuzi wa nafasi nne za kikatiba. Odinga amemlalamikia Rais Kibaki kwamba hakumshirikisha katika uteuzi wa nafasi nne za Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Mkurugenzi wa Mashitaka na Mkurugenzi wa Bajeti.
  Rais Kibaki hivi karibuni alitangaza kuwateua Jaji Alnashir Visram kuwa Jaji Mkuu, Profesa Githu Muigai kuwa Mwanasheria Mkuu, Kioko Kilukumi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka na William Kirwa kuwa Mkurugenzi wa Bajeti. Hata hivyo akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Makongeni, Nairobi, Odinga alisema; “Mimi sitaki kupigana na Kibaki hadharani, nataka kusuluhisha haya maneno kiungwana."
  Mawaziri Profesa George Saitoti (Usalama wa Ndani) na Yusuf Haji (Ulinzi), walimjibu Odinga wakidai wamewasiliana na Rais Kibaki ambaye aliwathibitishia kuwa kulikuwa na mazungumzo ya kushauriana kabla ya majina hayo kutangazwa.
  Profesa Saitoti pia ni Mwenyekiti wa chama cha PNU ambacho Rais Kibaki ni mwanachama wake na Haji anatoka chama cha Kanu ambacho ni mshirika wa PNU.
  Katiba mpya inamtaka Rais kushauriana na Waziri Mkuu kabla ya kufanya uteuzi wa masuala yanayohusu katiba hiyo.
  Hata hivyo majina hayo yaliyotangazwa na Rais Kibaki yanatakiwa kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa.
  Uteuzi huo umeligawa bunge ambapo wabunge wa PNU na wale wa Kanu wameunga mkono uteuzi wa Rais Kibaki, wakisisitiza kuwa Odinga alishirikishwa, ambapo chama cha ODM kinachoongozwa na Odinga kimepinga uteuzi wa Kibaki.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Raila ni vyema akawa mkweli kuwa alishirikishwa ila hawakuafikiana juu ya matarajio ya pande mbili..............................Raila alitaka wajaluo wenzake wale na Kibaki hakutaka kwa kuhofia Rutto kulalamika ya kuwa hasimu wake amechagua Jaji Mkuu, Mwanasheria MKuu na DPP ambao watamsulubu yeye Rutto na kamwe haki anayostahili hawezi kupewa..............................
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii habari imekatika au! Maana sioni KIbaki akimjibu Raila
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mkuu pia hata akili zao ni kama zimekatika katika hivi, juzi ilikuwa KANU, mara Narc, mara PNU against ODM lakini tuunde serikali wote na sasa going to KKK - Kikuyu (Uhuru Kenyata) Kalenjin (Ruto) Kamba (musyoka) ghrrrrrrrrrr
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Umoja wa kitaifa!! This is an Imposible Thing Ever, Angalia kule kwa Mugabe na Tsvangirai, Huku Kibaki na Odinga. This is un workable!!
   
 6. n

  ntangeki Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kenya ni mfano halisi kuwa Katiba mpya bila Maadili haina maana yoyote.!!! Kenya imeshindwa kabisa kujivua gamba la ukabila...kila kitu kwao kinaanza na kabila na kinaisha na kabila....inasikitisha.
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  bongo tumechagua kuanza na udini na kumaliza na udini!
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Hii habari imekatika auMaana sioni KIbaki akimjibu Raila
  Amemjibu kupitia wasaidizi wake wa karibu........hahitaji yeye mwenyewe kumjibu moja kwa moja.........................
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Kenya ni mfano halisi kuwa Katiba mpya bila Maadili haina maana yoyote.!!! Kenya imeshindwa kabisa kujivua gamba la ukabila...kila kitu kwao kinaanza na kabila na kinaisha na kabila....inasikitisha.
  Tusibeze hatua muhimu ambayo wenzetu wamesogea........................tukumbuke hakuna Taifa kamilifu.............ila tusiache kujiboreshea maisha yetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo...............................
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Serikali ya Umoja wa kitaifa!! This is an Imposible Thing EverAngalia kule kwa Mugabe na TsvangiraiHuku Kibaki na OdingaThis is un workable!!
  This is true.........decision making process becomes tedious and cumbersome...........................from legalized consultations a weaker side in the coalition government hopes for elusive consensus...................

  matokeo yake ni ugomvi usio na mwisho.....................sielewi kwa nini waliamua kuingiza mambo ya muda mfupi ya GNU au serikali ya mpito katika katiba yao ambayo ni ya muda mrefu..........................
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Binafsi huwa simwamini Raila Odinga. Nakumbuka alipowafukuza kazi mawaziri kina Ruto namwenzake alisema ameshauriana mna Kibaki lakini ilikuja gundulika kuwa hakumshirikisha Kibaki na ndo maana Kibaki aliwarudisha ofisini. Hii ya kusema hakushauriana na Kibaki bado siiamini manake yamekuwapo mashauriano kati yake na Kibaki takgu mwaka jana!
   
Loading...