Rais kawapa kitendawili Morogoro wakitegue

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
RAIS KAWAPA KITENDAWILI MOROGORO WAKITEGUE.

Leo 00:58hrs 14/02/2021

Je, wakazi wa Morogoro ni wavivu kushindwa kuzika wapendwa wao hadi wapate msaada kwa Abood!?basi lenyewe analolitoa kwenda kuzika ni lile Leyland la 1980's namshauri atoe na zile yutong na Marco polo pia,Je watu walikuwa hawazikwi kabla ya hadithi za wanamorogoro kushindwa kuzika wapendwa wao wakisubiri msaada wa bus la Leyland!?

Kihistoria mambo ya kuzika alianza Mzee Hood,alitoa bus la kuzikia ila alipokatwa katika kura za maoni akaacha kutoa bus,Mbinu hiyo ikadakwa na Mpinzani wake Abood akaanza kutoa bus akaenda nao utaratibu ambao ukawa mazoea kwa watu wa Morogoro,mwanzo alikuwa na timu ya watu wanafatilia kujua taarifa za misiba na kuleta taarifa kisha anaratibu msaada wa usafiri.

Mambo yakabadilika baada ya wananchi kujengewa mazoea na kunogewa na kupenda dezo,sasa wao ndiyo wanapigana vikumbo kuomba kusaidiwa usafiri na hata gharama zingine kama chakula kwenye msiba,

-Mbinu za Medani:Ilikuwaje amsifie halafu kesho yake amseme hadharani.

Mimi Msemakweli Chakubanga niliyefuzu mbinu za medani nilichokiona ni kama kuna matumizi makubwa yaliyopitiliza ya nguvu za kupuliza (nguvu za giza) kutoka kwa Mbunge kwani utaweza shangaa mwenyewe na hata mimi nashindwa kunyoosha vizuri maelezo yangu,najua hata mtaani nitatafutwa na chawa wake waliojaa kila mtaa wa Morogoro ili wanipoteze,

Mwaka 2016 Rais aliingia ghafla kwa kushitukiza Mjini Morogoro maeneo ya Msamvu akitokea Dodoma, alimpiga sana Mbunge,alimpa makavu live huku akiangalia ofisi yake ya bus na ofisi yake pale chini kilipokuwa kiwanda cha Mafuta Moproco, na hoja ya Rais ilikuwa hiyo hiyo na safari nyingine alikuwa katika wilaya za mkoa huo alikuwa anampigia uko,kuna siku alikuwa na ziara mkoani hapo cha ajabu alimsifia sana,kwani walimpokea wakampa maji ya kunywa mbinu za medani za kichawi zikafanya kazi,

Juzi akiwa katika uzinduzi wa soko pia alimsifia sana tena sana na yale mapokezi yalijulikana kuwa ya siku moja tu na mbinu za medani za kichawi zikaelekezwa kwa siku moja tu, sasa Mzee akaongeza siku za kukaa pale akiwa jukwaani yaani alibadirisha gia angani akaomba radhi wasaidizi wake kwa kuongeza siku ya pili,sasa hapa sisi watu wa mbinu za medani za nuru ya rohoni na uchawi tunaelewa vizuri kuwa nini kilishindwa baada ya kuongezwa ziara ya siku ya pili kusikotegemewa,

Siku iliyoongezwa ndiyo iliyo muumiza mbunge kwani haikuwepo katika utaratibu wa kimwili bali wa kiroho,uzuri Mh Rais ni mtu wa kiroho sana na ukitaka kumpata uende kiroho sio kwa medani za kichawi,ndiyo maana kesho yake akawa kama si yeye na kumpiga mbunge kama hamjui na kumgalagaza kwa hasira kwani hata yeye mzee anafika wakati haelewi alimsifiaje vile jana yake kwa hiyo alishusha nyingi za uso mpaka shoo ya mbele uwezi kuitambua ha ha ha.

Wapendwa katika medani ya kiroho na imani ipo haja ya kuombea Mkoa wa Morogoro kwa ujumla hasa pale Morogoro mjini kwani wale watu wa pale hawafanani na watanzania wengine kwa imani kuwa maiti zao zitaozea ndani kama Mbunge hakuleta masaada wa magali yake kwenda kuzika na hii pale inachukuliwa kuwa ni fadhila kubwa kuzidi chochote kilichofanywa hata kabla ya uumbaji na kuwa Mungu ndiyo amemleta Mbunge kwa kazi hiyo ya kuwazika,Sasa angalia Rais jinsi alivyo piga anasema huyu jamaa ameuwa viwanda na wanamorogoro wamekosa kazi na pesa mwishowe wana kufa na yeye anawazika tu,tuiombee Morogoro.

Mkoa wa Morogoro kuna watu wameufanya shamba lao la bibi,wakati fulani Rais akiwa Kilosa pia alichukizwa kuhusu mashamba,Morogoro inahitajika uongozi imara kuliko mikoa mingine kuanzia Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa idara zote ndani ya Halmashauri,ukiwa legelege kuna watu wanakuweka mkononi wanafanya yao, Pia mkoa wa Morogoro unaonyesha hauna vipaumbele vya mkoa wako kama vipio ni nadharia tu. Morogoro kuna kila kitu ila wananchi wake ni maskini sababu hazijulikani.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Uandishi wako unasubiri rais aseme ili wakutafute wakupe kazi!

Kama unavyojitanabaisha kwa hizo diploma zako as umesoma, kwa nini usingefanya research mapema kabla ya kauli ya rais alafu uje na article kama hiyo?

😷 Utasubiri mtu atumbuliwe ndipo ule uteuzi!
 
Kwa kutumia mbinu za kimedan kama ulivyotanabaisha unaweza ukaelezea ni kwa nn Rais akukata jina la Mbunge kama baadhi ya watu walivyotegemea kutokana na vile alivyo kua akimnanga awali?
 
Msomi fake anaye ngojea Mh. Rais aongee ndio aonganishe dots atunge story, so weak mentally, haya mambo ya kuongea au kuandika baada ya kujua matokeo ya jambo fulani yamepitwa na wakati, kwanini hujaandika haya kabla Mh. Rais hajasema? Umeandika tu baada ya Mh. Rais kusema.

It means ww ni mfuata upepo, huna firm base ya understanding of issues kabisa, ww you are firm on tissues, i.e petty issues, usomi wako wa vyeti tu, no competency, msomi hawi na tabia za hovyo hivyo.

In general Morogoro imebakia nyuma sbb ya culture ya wana morogoro, wavivu sana, ni kweli Abood kafanya kosa kubwa kuua viwanda na kuua ajira na katumia advantage ya uvivu wenu kuwa tawala kwa kuwapa vizawadi vya bus kwenda kuzika. So Abood ni kweli hafai kabisa, hana maendeleo kwa Morogoo mjini bali maendeleo yake tu, so ww ungetakiwa uandike haya kabla Mh. Rais hajasema kitu ili tujue mambo haya mapema. Kazi yako ni fuata upepo.

It means next month Mh. Rais akija akimsifia tena Abood utaandika kumsifia, wakati wote tunajua Abood hafai kabisa kuwa Mbunge wa Morogoro mjini, haleti maendeleo kabisa kwa watu.
 
Tangu wanaccm wakuchinjie baharini unahangaika utadhani kuku aliyekatwa kichwa ! Hiyo namba ya simu ndio kutafuta ukatibu kata ?
Mleta mada atasubiria sana, Morogoro na waarabu damu damu.

Akitoka Aboud anaingia Sallam. Radio za propaganda na network wanazo.

Mleta mada yeye yuko bize JF.
 
Hivi kijana sijui mzee husikii aibu kuandika mameseji kama haya? Shida ni nini, ni kuwa lazima uandike kitu au ni lazima uoneshe kumsifu mkuu?

We kubali tu kuwa mkuu hatabiriki that is all. Ishia hapo hapo na anawapa tabu sana mnaotembelea biti zake, maana leo anamsifu tu mnajaa wote mnamsifu na kesho anageuka maili mia anamponda yule yule aliyemsifu na kama kawaida yenu mnajaa tena. Sasa kiubinadamu mnajisikia mapimbi sana matokeo yake ndio haya sasa unajikuta inatakiwa utoe sababu ya kusifu pande zote.

Mkuu mbona kuna kazi nyingi za kufanya tu?
 
Jimbo la Morogoro mjini akiliachia Abood, atalichukua Rostam Aziz, akilikataa Al-Saedy alishajaribu kuweka nia.

Mleta mada utakuwa mbunge wa jimbo Morogoro mjini kupitia JF!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Leislie Mloka, nimekusoma muda mrefu ila nikawa nakuvutia pumzi tu. Hili bandiko lako lina conflict of interest kwa kuwa na wewe uligombea na Abood jimbo moja.

Kwa tunaokujua ulivyokuwa na uwezo mdogo darasani, sijui hata hayo madigrii uliyapataje. Kwa kupitia wewe naamini kuwa miujiza kwenye elimu bado ipo!

Baba ako aliupata ubunge wa Morogoro kibahati, kwanza kwa kuwa ni Mluguru, pili kwa kuwa alikuwa manispaa na tatu kwa kuwa hakukuwa na mtu wa maana wa kugombea ndipo wakamuokoteza mzee wako aje kugombea.

Baba ako mwenyewe kwa kipindi kimoja alichokaa madarakani, hakuna cha maana alichokifanya Morogoro zaidi ya kujinunulia Landcruiser na kulifunga kitela cha kubebea mizigo.. Bora hata Abood anatoa bus linabeba wananchi. Baba ako hakumjua mtu, hata watu bara barani alikuwa anawapita bila kuwapa lift. Angekuwa muungwana, angewapakia hata kwenye kile kitela enzi hizo ambazo dala dala ilikuwa ni Msamiati.

Sasa basi, kama bahati aliipata mshua wako, sio lazima na wewe uipate.. Usitumie nguvu nyingi sana kujipromo ili upate teuzi.. Hivi vyeo huwa vinakuja tu, ukivilazimisha sana huwa havidumu na mwishowe huweza kukuumiza.

Kwa umri wako, bado unayo nafasi ya kujaribu tena 2025. Kwa sasa tafuta tu kazi ingine ya kufanya.
 
Back
Top Bottom