Rais Karume akataa kukutana na Watanzania UK! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Karume akataa kukutana na Watanzania UK!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by alibaba, Apr 15, 2010.

 1. a

  alibaba Senior Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Juhudi za Tanzania Association UK (TA UK) na zile za Zanzibar Walfare Association (ZAWA) Za kujaribu kumpata Rais wa Zanzibar ambae pia ni makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ili aweze kukutana na watanzania waishio UK Ziliishia kupiga ukuta leo hii pale Ofisi ya Balozi wa Tanzania UK ilipovithibitishia Vyombo hivyo viwili kuwa Mheshimiwa huyo hataweza kuonana na Watanzania kutokana na Shughuli nyingi alizonazo.

  Pamoja na wingi na umuhimu wa shughuli zake ningedhani kuwaona Watanzania ingekuwa moja ya yale yaliyomuhimu katika ratiba yake.

  Binafsi nimefadhaishwa sana na Matokeo hayo na Rai yangu ni kuwataka viongozi wa TA UK na ZAWA kwa pamoja Kwenda Ubalozini na kujaribu kumshawishi Balozi aone umuhimu wa mkutano wa Mh. huyo na wananchi kwani sikumbuki tunapoendea miaka kumi ya uongozi wake kukutana na wananchi ajapo hapa Uingereza.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Safi sana Karume! Hao watanzania warudi bongo watamwona tu mh
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kwani Rais anajipangia ratiba yeye mwenyewe? Yeye anapangiwa na wasaidizi wake wakishirikiana na ubalozi; tena mambo hayo yanafanywa mapema sana hata kabla ziara haijafanyika. Sasa kama ubalozi ulizubaa au watz wenyewe waliokuwa na hamu na kuongea naye hawakuushtiua ubalozi mapema ili ratiba iwe na hicho kipengele unafirki Rais angefanyeje? Ni wazi si rahisi kupata muda wa ziada na kuongea nanyi.
   
 4. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Hata ingekuwa miaka 20, kukutana na kila kundi la raia inakuwa ngumu sana kama haiwezekani kabisa. Punguzeni kutafuta lawama.
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Labda hakuona umuhimu wa kukutana nao!
   
 6. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 765
  Likes Received: 550
  Trophy Points: 180
  Na mimi nimemkubali. Watanzania walioko Tanzania hawapati hivi vi fursa vya kukutana na Rais tena watu 30 kwenye chumba na kuuliza maswali na dukuduku zao.

  Watanzania 40 wa Uingereza wana tija gani na mda wa Rais zaidi ya kumuomba makaratasi ya Uraia? Makaratasi ya uhamiaji ya Watanzania 60 sio kipaumbele cha ratiba ya Rais.

  Na Karume sio mtu wa kukaa na kuchekacheka na vi halaiki vodogo vidogo vya wahamiaji wa London. Uwanja wa Taifa haji atakuja kuonana na Watanzania thelathini London?
   
 7. I

  Inkoskazi Member

  #7
  Apr 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tujaribu kupunguza siasa/lawama katika kila jambo. Hao ndugu zetu hapo UK wa muhimu kwao ni balozi wanayeishi nae hapo siku zote kuliko huyo Karume anejipitia na safari yake ya siku mbili iliyoratibiwa toka Zanzibar.  Moringe wote ni Wamasai lakini sio kila Mmasai ni Moringe
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Karume siyo Makamu wa Rais wa Muungano.... tuanzie hapo kwanza.. yupo Makamu mmoja tu.. naye ni Dr. Mohammed Shein.. Karume ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.. (sijui kama bado lipo)
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Msikurupuke Karume anajua fika kuwa akuna Nchi inaitwa Tanzania ila kwa tulivyozoea tunasema Tanzania ni nchi hewa kila mwenye uenyeji mpishe ,Maana kama Zanzibar si nchi sasa hiyo balozhi ya Tanzania alimpokea kama nani ?
   
 10. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Safari hii mtachekea bafuni! Mlidhani Karume ni JK anayeonana na wauza mandazi wa London? Yule Karume ni Presidential ati.
   
 11. Kiwalani

  Kiwalani Senior Member

  #11
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Itakuwa ratiba imekaa vibaya tu; mbona amekubali kwenda Minneapolis, MN mwanzoni mwa Julai kushiriki mkutano wa DICOTA www.dicotaus.org ?
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  He, Vereje...!!!???
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Apr 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ila sidhani kusema neno "kukataa" ni kumtendea haki..
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Naam, Bali ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri na pengine (ndivyo ilivyo) ni mkubwa kuliko Waziri Mkuu! Sasa fanya hesabu zako urudi kwenye hoja.
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280

  Kumbe huko ughaibuni WaTz wana vyama viwili tofauti kama nchi mbili tofauti? Kuhusu Karume, mnadhani huyu mmwinyi angewaambia nini la maana na kubadilisha nini katika hali hii ya Maisha magumu kwa kila MTz? labda aendelee na propaganda zake za kutetea Chama Cha Matumbo. Bora hata hakuja. Nawashauri wenzetu endeleeni kupambana na maisha kivyenu huko tena kihalali achanane na hawa jamaa wasokuwa na machungu na sisi.
   
 16. K

  KISUKALI Member

  #16
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 28, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji,
  Kwanza pokea Saluti toka kwangu,pamoja na kujiunga na jukwaa hili kipindi, leo nachukua fursa yangu ya kwanza kuchangia:
  Mtoa hoja kutumia neno "kukataa" nafikiri ni katika mila zetu za kujaribu kuwaheshimu viongozi wetu, japokuwa mara nyingi viongozi wenyewe wameonyesha udhaifu mkubwa kiasi kwamba si wakustahili hizo heshima tena. Maoni yangu ni kuwa Mh. huyo Ameogopa/Amekimbia kukutana na hao jamaa Zetu waioshio UK. Pamoja na kuitwa wauza Maandanzi au wangetokea Watu 30 au 40 Naamini wangekuwa na hoja za Nguvu mbele ya Karume Wangekuwa na Uhuru mpana wa kujimwaga mwaga kwa Maswali bila ya kuwa na Hofu au wasiwasi wa kugongewa Mlango kesho au kupoteza kazi yako ukiwa Mwandishi wa Habari Au kubambikiwa matatizo usiyokuwanayo.
  Kwa hali hiyo Karume ameamua na kukubali kumalizia miezi michache ya ngwe yake iliyobakia kwa kutulia tuli katika Tope alizokalia bila Kuzioga au kumpa Fursa mtu Amwogeshe nazo. Yawezekana ni uamuzi wa busara, nina hakika si Wakijasiri!
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Apr 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  "ni mkubwa" kuliko Waziri Mkuu? si kweli kwa sababu hawako katika uwanja mmoja.. ni tofauti na Waziri Mkuu ndiyo..
   
 18. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #18
  Apr 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kwani lazima kuonana nao?hee jamani mbona mnawatwishwa wenzenu mizigo mizito?kwani ni mara ngapi anaenda huko?
   
 19. a

  alibaba Senior Member

  #19
  Apr 17, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  X-P,
  Mbona unajitoa? Na wewe ndie uliealika Watu kusikiliza Ngurumo za Maalim Seif? Haingekuwa vizuri kwako na kwa wengine kusikia " Ngurumo" za upande wa pili?
   
 20. S

  Siao Member

  #20
  Apr 17, 2010
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana lolote hao.........................!!!??
   
Loading...