Rais Karume akataa kukutana na Watanzania UK!

Mimi naona Karume amewakosea Watz na anatakiwa awaombe radhi kwa kuwakwepa kama kweli alikataa kuonana nao! Unless kama kulikuwa na sababu ya msingi ya kutoonana nao, kwa hili simwelewi!
 
Juhudi za Tanzania Association UK (TA UK) na zile za Zanzibar Walfare Association (ZAWA) Za kujaribu kumpata Rais wa Zanzibar ambae pia ni makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ili aweze kukutana na watanzania waishio UK Ziliishia kupiga ukuta leo hii pale Ofisi ya Balozi wa Tanzania UK ilipovithibitishia Vyombo hivyo viwili kuwa Mheshimiwa huyo hataweza kuonana na Watanzania kutokana na Shughuli nyingi alizonazo.

Pamoja na wingi na umuhimu wa shughuli zake ningedhani kuwaona Watanzania ingekuwa moja ya yale yaliyomuhimu katika ratiba yake.

Binafsi nimefadhaishwa sana na Matokeo hayo na Rai yangu ni kuwataka viongozi wa TA UK na ZAWA kwa pamoja Kwenda Ubalozini na kujaribu kumshawishi Balozi aone umuhimu wa mkutano wa Mh. huyo na wananchi kwani sikumbuki tunapoendea miaka kumi ya uongozi wake kukutana na wananchi ajapo hapa Uingereza.
Alibaba,
Tangu lini Karume wa sasa amekuwa makamu wa raisi wa muungano?
 
Mkuu,kama sijakosea Rais Karume wa Zanzibar SI Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.Nafasi hiyo anayo Mhe.Mohammed Shein
Nafikiri Mzee Karume amekwepa tu kujibu maswali magumu ambayo angeulizwa na waTanzania hasa muda huu wa kukaribia uchaguzi Mkuu mnamo Oktoba
 
Back
Top Bottom