Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
VIONGOZI wa chama cha National League for Democracy (NLD) Zanzibar, wamependekeza utawala wa Rais Amani Abeid Karume uendelee kwa miaka miwili zaidi, ili kutoa nafasi ya kumaliza matatizo yaliyojitokeza katika uandikishaji wapiga kura.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika Idara ya Habari (Maelezo) Zanzibar, Naibu katibu Mkuu wa NLD, Rashid Ahmed Rashid na Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa Chama hicho, Nassor Khamis, walisema mazingira ya sasa hayatoi nafasi kwa uchaguzi mkuu uliokuwa huru na wa haki.
Walisema hoja zao za kutaka uchaguzi mkuu wa 2010 ucheleweshwe hadi mwaka 2013, zinatokana na kuwa watu wengi bado hawana vitambulisho vya ukazi au vyeti vya kuzaliwa, ili kuwawezesha kupata vitambulisho hivyo.
Walisema wananchi hawapaswi kulaumiwa moja kwa moja kwa kukosa vitambulisho, lawama ni kwa ofisi ya vitambulisho, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na Chama cha Wananchi (CUF).
Tulikuwa Pemba hivi karibuni na utafiti mdogo tulioufanya unaonesha kuwa watu wengi watakosa kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kwa sababu ya kutokuwa na vitambulisho. Mfano katika baadhi ya shehia zaidi ya watu 300 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 70 wamekosa kujiandikisha kwa sababu ya kutokuwa na vitambulisho au vyeti vya kuzaliwa.
"Tunataka serikali isaidie kuhakikisha kwamba kila Mzanzibari anatendewa haki kwa kupata fursa ya kuchagua rais. Bora tuchelewe ili haki itendeke, Rashid alisema. Alielekeza lawama dhidi ya ofisi ya Msajili wa Mzanzibari na kutoa vitambulisho na kusema watendaji hawakujiandaa na wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwa Rais Karume.
Alisema hakuna taarifa iliyotolewa mapema na serikali, ZEC wala ofisi ya vitambulisho, kuwa vingetumika katika uandikishaji Zanzibar katika uchaguzi wa mwakani.
ZEC na ofisi ya vitambulisho wangekataa suala la vitambulisho kuwa lazima katika uchaguzi wa mwakani kwa sababu wananchi hawakuandaliwa na taarifa haikutolewa. Kwa hivi sasa haiwezekani kuwatenga watu wote kwa sababu ya uzembe, ni lazima watu wapewe fursa, alisema Rashid.
Pia alitoa lawama kwa ofisi ya vitambulisho kuwa, imekuwa ikitoa vitambulisho kwa watu wasio Wazanzibari. Wazungu na watu kutoka Tanzania tayari wana vitambulisho hivi, kwa hiyo Rais wa Zanzibar atachaguliwa na wageni. Khamis aliungana na Rashid katika kulalamikia utendaji wa ofisi ya vitambulisho na ZEC na kusema CUF imekuwa inasababisha vurugu.
Tayari tumemwandikia barua Rais Karume barua na nakala tumempelekea Rais Jakaya Kikwete kuhusu kasoro zote katika demokrasia nchini ikiwamo udhaifu wa ofisi ya vitambulisho, Uhamiaji na Idara ya Mambo ya Nje kwa kuwapa wageni vitambulisho na haki za kuishi nchini bila ridhaa ya wananchi, Khamis alisema.
Katika mkutano huo, pia wanasiasa hao walikanusha taarifa zilizotolewa na ubalozi wa Marekani kuhusu tahadhari ya usafiri wa kuja Zanzibar na kusema Zanzibar na hasa Pemba ambako mvutano wa uandikishaji ulianzia, hali ni shwari.
Taarifa ya Marekani kuwataka raia wake kuchukua tahadhari wanapokuja Zanzibar, imetolewa bila utafiti wa kina. Pemba ni shwari. "Marekani wamezoea kuingilia mambo ya ndani ya Zanzibar na kwa taarifa yao, uchumi wa Zanzibar unaweza kuathirika, walisema na kuongeza kuwa wamewaandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kulalamikia hatua hiyo ya Marekani.
SOURCE: HABARI LEO.