Rais Kabila azindua jengo refu zaidi Afrika Mashariki na Kati

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397

Rais Kabila amewasili katika uwekaji na uzinduzi wa jengo refu kuliko yote nchini la Mamlaka ya Bandari nchini -TPA

Serikali inamiliki kwa 100% jengo jipya ambalo ni refu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati la TPA linalozinduliwa leo

Mkurugenzi Mkuu wa TPA akitoa maelezo ya awali kwa wageni waalikwa

Mkurugenzi: Baada ya kuwekwa jiwe la msingi na kuzinduliwa leo, jengo litaanza kutumika mwezi January 2017.

Mkurugenzi: TPA imeshapokea maombi 32 ya wateja wanaotaka kupangisha katika jengo jipya.

Mkurugenzi: Meli, mizigo ipo; wanayosema kwa kubeza katika vyombo vya habari sisi hatuna muda nao tunachapa kazi

===========

Waziri Prof. Mbawala: Zaidi ya miradi 7 ya ujenzi wa miundo mbinu ya TPA itatekelezwa kwa wakati na ufanisi mkubwa.

Waziri Prof. Mbawala: Serikali ya Tanzania itaanzisha safari za ndege moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda DRC.

==============
Rais Magufuli: Tumshangilie mzee huyu..Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanya maamuzi ya ujenzi huu. - Rais Magufuli akihutubia.

Rais Magufuli: Wenzetu DRC kwa upande wa ziwa Tanganyika wanamafuta sasa itakuwa rahisi kuunganisha na lile la kutoka Uganda kuelekea.

Rais Magufuli: Tumeimarisha namna ya kusafirisha mizigo kwenda DRC, maeneo ya kupima tumeyapunguza sasa ni matatu tu.

Rais Magufuli: Wenzetu DRC kwa upande wa ziwa Tanganyika wanamafuta sasa itakuwa rahisi kuunganisha na lile la kutoka Uganda kuelekea Tanga.

Rais Magufuli: Nimemshukuru sana Rais wa Congo, Joseph Kabila kwa jeshi lake kuokoa watanzania madereva waliokuwa wametekwa kule.

Rais Magufuli:
Zaidi ya makontena 15,927 ya DCR yalipita katika bandari ya Dar es Salaam kwa mwaka jana pekee.

Rais Magufuli: Kulikuwa na watu ambao walifikiri bandari ni mali ya kwao, na kusahau ni mali ya serikali.

Rais Magufuli: Palikuwa na watu ambao kwao rushwa ilikuwa ni breakfast ya kila siku.

Rais Magufuli: Tumefacilitate mikwamo iliyokuwa ikitokea barabarani, tunataka mizigo isiwe inamaliza zaidi ya siku 3.

Rais Magufuli: Wakandarasi wameshatembelea maeneo ya kujenga reli, kama wajerumani walijenga sasa kwa nini tusijenge.

Rais Magufuli: Tunataka uchumi wetu ukue kwa asilimia 7. 2.

Rais Magufuli: Palikuwa na matatizo madogo madogo yaliojitokeza kwa siku za nyuma ,lakini nakuthibitishia Mh.Rais yote.

Rais Magufuli: Rais Magufuli: Sambamba na hilo tulianzisha ICD ( dry port) lengo la dry port lilitumika vibaya.

Rais Magufuli: Sambamba na hilo tulianzisha ICD ( dry port) lengo la dry port lilitumika vibaya.

Rais Magufuli: Vituo vitavyokuwa na mizani ya kupima mizigo barabarani inayokwenda DRC ni 1. Vigwaza 2. Manyoni na 3. Nyakahoro.

Rais Magufuli: Tukawaambia wafanya biashara wa malori, kama mizigo haipatikani wakaibebee huko huko inakopatikana.

Rais Magufuli: Walikuwapo watu ambao walifikiri bandari ni mali ya kwao, wakasahau kwamba hii ni mali ya serikali

Rais Magufuli: Bandari hii ya DSM tuna rekodi kuwa zilishawahi kupotea meli 60 na zina mizigo lakini sasa hata kontena halitapotea.

Rais Magufuli: Nakuomba Balozi wa DRC, ikitokea mfanyabiashara analalamika sababu ya rushwa, njoo kwangu tumtafute huyo anayetukwamisha.

Rais Magufuli: Nitafurahi sana kwenda kufungua kiwanda kilichojengwa na mtu kutoka Lubumbashi, meneo mengine hapa Tanzania.

Rais Magufuli: Baada ya kusema haya niwashukuru wafanyakazi wa TPA, sitawaangusha, nikushukuru waziri na watendaji.

===========

Rais Kabila: Ahsante sana kwa heshima ambayo unaipatia nchi yetu DRC ili tuweze kuja hapa leo na mimi nikiwakilisha.

Rais Kabila: Tangia miaka ya 60 wakati tulikuwa na Mwl. JK Nyerere hapa, tunaendelea kuimarisha uhusiano.

Rais Kabila: Kuna kipindi ambacho miaka minne mitano iliyopita biashara ilikuwa imeshuka na kuna sababu, ambazo ulitoa.

Rais Kabila: Bandari hii ipo DSM Tanzania lakini ni bandari yetu, 50% ya biashara tunayoifanya DRC inapitia bandari hii.

Rais Kabila: Ukweli bandari ya DSM ni bandari yetu kwa sababu upande wa Mashariki mwa kongo tuna mpaka na nchi nne.

Rais Kabila: Ningependa uhusiano uendelee na nitahimiza wenzetu waliopo Kongo waendelee na huo uhusiano.

Rais Kabila: Uzalishaji wa madini ya shaba umefikia zaidi ya tani 1,000,000 zitakuwa zinapita hapa TPA.
27378706522_3636dfe782_b.jpg

Jengo jipya la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) lina ghorofa 35, lina ofisi mbalimbali na Ukumbi utakaoweza kuchukua watu 1,200 kwa wakati mmoja.
 
Rais Kabila amewasili katika uwekaji na uzinduzi wa jengo refu kuliko yote nchini la Mamlaka ya Bandari nchini -TPA

Serikali inamiliki kwa 100% jengo jipya ambalo ni refu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati la TPA linalozinduliwa leo

Mkurugenzi Mkuu wa TPA akitoa maelezo ya awali kwa wageni waalikwa

Mkurugenzi: Baada ya kuwekwa jiwe la msingi na kuzinduliwa leo, jengo litaanza kutumika mwezi January 2017.

Mkurugenzi: TPA imeshapokea maombi 32 ya wateja wanaotaka kupangisha katika jengo jipya.

Mkurugenzi: Meli, mizigo ipo; wanayosema kwa kubeza katika vyombo vya habari sisi hatuna muda nao tunachapa kazi

Waziri Prof. Mbawala: Zaidi ya miradi 7 ya ujenzi wa miundo mbinu ya TPA itatekelezwa kwa wakati na ufanisi mkubwa.

Waziri Prof. Mbawala: Serikali ya Tanzania itaanzisha safari za ndege moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda DRC.

Waziri Prof. Mbawala:

Hivi ni lini tutaweza kubaki kwenye mstari wa kufanya jambo husika mahala pake bila vijembe?
 
Hivi ni lini tutaweza kubaki kwenye mstari wa kufanya jambo husika mahala pake bila vijembe?

Mpaka pale mtakapo acha kupiga vijembe bila ya mnaowasema kuwepo ili wawajibu hapo hapo kama midahalo ya USA. Infact wanajibu hoja zenu za kushutumu kila kukicha.

Siunaona ujinga wa CUF hautajwi sababu wanapopoana wenyewe kwa wenyewe. Ukilitupa kwa Jirani tu itakapopatikana fursa unajibiwa kwa vitendo kuweka record sawa.
 
Back
Top Bottom