Rais Kabila Anusurika Kuuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kabila Anusurika Kuuliwa

Discussion in 'International Forum' started by kilimasera, Feb 28, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Watu tisa wamefariki dunia baada kundi la watu wenye silaha kuivamia ikulu ya jamhuri ya Kongo na kupambana na walinzi wa ikulu wakiwa na nia ya kumuua rais Joseph Kabila.
  Kundi la watu wenye silaha wakiwa na bunduki na mapanga waliyavamia makazi ya rais wa Jamhuri ya Kongo, Jospeh Kabila wakiwa na nia ya kumuua rais huyo na kuipindua serikali yake.

  Mapambano makali yaliyodumu takribani lisaa limoja yalizuka baina ya walinzi wa ikulu na kundi hilo ambapo watu saba toka kwenye kundi hilo waliuawa huku walinzi wawili wa ikulu nao wakipoteza maisha yao.

  Rais Kabila na mkewe hawakuwepo ndani ya makazi hayo wakati shambulio hilo lilipotokea.

  Waziri wa mawasiliano, Lambert Mende alijitokeza kwenye televisheni ya taifa na kusema kuwa hali sasa iko shwari.

  "Hawa watu walitaka kumdhuru rais Kabila", alisema waziri Mende na kuongeza kuwa baadi ya watu toka kwenye kundi lililofanya shambulizi hilo waliuliwa na wengine walikamatwa na kutiwa mbaroni.

  Rais Joseph Kabila alichaguliwa katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 2006 na ana mpango wa kugombea tena katika uchaguzi ujao mwezi novemba mwaka huu.

  Alirithi urais toka kwa baba yake, Laurent Kabila aliyeuliwa mwaka 2001.
   
 2. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Dah Inabidi kuongeza ulinzi sana kwake...Hawa Jamaa hawana mchezo.....Lakini habari zinasema bwana alikuwa kwenye makazi yake...
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mambo ya kiintelijensia hayo lazima yatachanganya tu sijui mie nimesoma magazeti mengi wanasema hakuwepo sasa sijui si unajua sababu za kiusalama na kutaka kuonyesha kwamba jeshi halina udhaifu yawezekana alikuwepo ama hakuwepo!ila nashangaa inakuwaje wavamizi wafike mpaka ikulu ina maana ulinzi hautoshii nina maana ana walinzi wachache??
   
 4. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hii mambo ya congo bana...inawezekana kabisa mpango mzima ulikuwa kwenye hao hao presindental guards kama kwa baba yake ilivyo kuwa...inaweza kuwa kuna mtu kachomekwa..ndani ya systeam...ila ali miss target wakati wa kuvamia...kwani walifika mpaka ikulu..kama 50m ndio wakazuiwa kwenye road block hapo ndio shughuli ikaanzia..

  Jamaa atagombea tena mwaka huu november na bado kuna upinzani upande wa mashariki mwaka DRC...ndio ambako hajakamanata sana..bado kuna internation peace keeper kwenye nchi..maneo ya Bunia,Goma Ben...haijatulia kabisa..I hope atajiongezea ulinzi..au apeleke wengine mafunzoni Ufaransa..
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kweli madaraka ni gharama sana mie nilidhani ataogopa kugombea hivi kwanini CONGO haitawaliki tatizo kubwa ni nini yaani naona watu wanashindwa kua pamoja kabisa!na hali hii sijui kama itakuja kutulia!
   
 6. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  I cant imagine eti watu watoke kwenda kuvamia ikulu....i cant think of it at this era.
   
 7. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anything is possible now.. Watu wamechoka maisha ya mulo mmjoa kwa siku. Na Congo with all its richness...utashanga saana cku utaenda Kinshasa..umaskini wakutisha, na hapo ni mji mkuu. Sasa fikiria miji mingine kama bukavu, goma n.k..??
   
 8. papason

  papason JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Tatizo la huyu jamaa (Comrade Kabila Jr.) hajui kusoma alama za nyakati au sijui ni ubishi wakee tuu, raia wameisha mchoka lakini yeye amebakia kuwa king'ang'anizi sita shangaa nikisikia kafanyiwa kitu mbaya kama babake!
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanangu sio tatizo lake tu kila kiongozi mwafrica akiishakaa hataki kutoka unakumbuka ya kibaki wa kenya!!mie sijawahi kusikia kama msumbiji kuna matatizo kama haya ya kung'ang'ania madaraka sijui kwanini hawa jamaa mie naona akiondoka vizuri itasaidia sana hata kujenga mshikamano kwa raia wake hata hapa kwetu tanzania CCM wasingekua wanatumia ubabe mie nadhani watu bado wengi tu wangekua wanakipenda chama ila kwa sasa wanakichukia sababu kimekua kinatumia ubabe mwingi kwenye maamuzi na kuwakandamiza watu wa hali ya chini ama kweli taabu tu
   
 10. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Basicaly Congo juu ya utajiri mkubwa wa Madini mbali,Misitu,Mito...pande za kusini(North Kivu) na mashariki tena ambako kuna copper na jicho la mmarekani liko uko..then kuna Uraniu, nchi una utajili mwingi wa asili sana...ambao bado haujaanza hata kutafitiwa..

  So yote haya kila mwanasiasa anatama awa ontop either kwa nguvu au democrasia...achilia mbali majeshi ya nchi zingine kuingia na kufanya vurugu..na kuchukua miti na hata dhahabu...kupita north ambako uganda,burundi na rwanda zinashabihiana.

  So west countries ambako lina watu wao wengi sana...wanafanya mambo mbali mbali kujua nini kinapatikana zinaweza zenyewe kwa zeneyewe kuwa na makundi..kama nchi zinazo msaport Jean Mbemba...na za Kabila...so zinakuwa zina mpa uwezo flan flan achukue mamlaka ili weweze kuingia kirahisi...etc...Ndio issue kuu...Uku.
   
 11. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi kwa hili nahisi ulinzi kwa huyu raisi si wa makini sana
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hata kwa baba yake haukua makini na ndio maana aliuawa
   
 13. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  CORRECTION:
  1. Tukianza na Headline:
  RAIS KABILA ANUSURIKA KUUWAWA SIO KUULIWA

  2. Katika kiswahili hakuna wingi wa saa, (yaani huwezi kusema masaa) ni SAA hata kama ni 1000

  3. Usiseme Mapambano makali yaliyodumu takribani lisaa limoja
  Sema Mapambano makali yaliyodumu takribani saa moja

  Tusaidiane kukuza kiswahili chetu kwa kukitumia kwa ufasaha: hapo kwenye masaaa wengi wanapata sana taabu hata waandishi na watangazji wa redio, mpaka kwenye matangazo ya kampuni za simu utasikia ONGEA KWA MASAA 24
  Asanteni kwa kunisikiliza.
   
 14. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaaaam haaya bwana malenga wetu
   
 15. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kudokeza kwenye thread yangu moja on Jukwaa la Siasa kuwa marais kama Mugabe, Kabila, Museveni, CCM wakae mkao wa kufuturu maana saa ya ukombozi yaja na wala si mbali mtasikia mambo yakiitikia. Kama kakoswakoswa basi ujue yuko njiani kwenda kuonana na baba yake soon.
   
 16. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe....its all bout western countries interests and this hurts......tunakufa sisi,wao wachukue madini wakaendeleza kwao sisi watuletee misaada......sasa yule Mbemba ile kesi iliisha? ataweza gombea tena kweli na ile kesi yake kama bado ipo? i also think Kabila is not strong enough!
   
 17. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  I hope you don't take it personal mkuu, tunawekana sawa tu kilimasera, au sio mtu wangu?
   
 18. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nimekuelewa mkuu c unajua kiwahili kigumu sana na lafudhi pia inasumbua
   
Loading...