Tenderness
Member
- Nov 28, 2015
- 29
- 18
Hiki ni kichaka kingine cha wezi wa pesa za Umma! Yaani mtu unazungushwa kama unafuatilia mali ya urithi vile, vocha nimesainishwa ila hundi hawatoi na wakati pesa ilishaletwa siku nyingi.. Toka mwezi wa saba mpaka leo tunaelekea mwezi december naishiwa kuambiwa sijui nenda TIRA mara sijui kwa msuluhishi wa migogoro ya bima.
Nataka nikwambie mh rais ni kwamba binafsi niliamua kukatia bima gari langu NIC kwa sababu ya uzalendo wangu tu kwa taifa langu, ila bahati mbaya matatizo ndo yakanikuta. Kilichotokea ni kama vile huyu meneja ametumia hiyo hela kufanya mambo yake hivyo ananizungusha ili yeye aendeleee kunufaika na pesa yake! Nimepoteza mpaka ajira yangu kwaajili ya kutumia muda mwingi kufuatilia madai yangu!
Naomba umulike shirika hilo kwani limekua kama kichaka cha kujipatia pesa wakati watanzania wa hali ya chini tunateseka,sio kama hatuoni kampuni binafsi, ni vile tu sisi wengine tunaipenda sana hii nchi kwahiyo hata tunafikiria kufanya lolote tunawaza kwanza nchi yangu inanufaikaje!
Mwisho kabisa nakutakia kila lililo jema katika safari yako ndefu ya kukamua majipu, ni kazi ngumu na yenye gharama kubwa lakini nataka nikukikishie kwamba MUNGU ANAEISHI yuko mbele yako atakushika mkono na kukupigania, na zaidi Watanzania wote tunasali sana kwaajili yako!
Ni mimi mzalendo, sijafunguka sana kwa sababu za kiusalama!