CAG aweka wazi mbinu chafu za kujipatia fedha isivyo kihalali ndani ya Shirika la Bima la Taifa

vtuko

Member
Jun 12, 2016
41
25
CAG AWEKA WAZI MBINU CHAFU ZA KUJIPATIA FEDHA ISIVYO HALALI NDANI YA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA

Katika ripoti ya CAG (2020/2021), miongoni mwa taasisi ambazo viongozi wanajipatia fedha za umma kwa njia za ujanja ujanja ni Shirika la Bima la Taifa (NIC).

CAG anaonyesha wazi kwamba, kiasi cha shilingi za kitanzania milioni sabini na mbili (Sh. 72,000,000.00) zililipwa kwa wafanyakazi wasiostahili malipo hayo kupitia vocha ya malipo namba PV/NMB/G/2010/9783 ya tarehe 12 Oktoba 2020.

Hii sio bahati mbaya kwani Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima, Dkt.Elirehema Doriye amekuwa na tabia hiyo ya kujipatia fedha kwa njia za ujanja ujanja. Katika malipo hayo yaliyofanyika kinyume na taratibu lazima gizani Mkurugenzi Mtendaji huyo ana chake kwani hiyo ni tabia yake.

Maoni aliyoyatoa CAG ni kwamba taasisi za umma zinazowanufaisha wachache kiujanja ujanja zinatakiwa zifuate sheria na miongozo ya matumizi ya fedha za Serikali. Kwa kuwa fedha ya Serikali ni ngumu na inahitajika kila sehemu kwa shughuli za maendeleo, inapotokea kiongozi mmoja anatumia cheo chake kujipatia fedha hisivyo halali anakuwa moja kwa moja anarudisha nyuma shughuli za maendeleo za nchi yetu.

Hivyo maoni hayo ya CAG pekee hayatoshi. Wale wote walionufaika na fedha hizo wanatakiwa wazirudishe ili kulinda uadilifu wao katika utumishi wa umma. Katika misingi ya Taifa letu tumefundishwa kuwa, cheo ni dhamana, hapaswi mmoja kati yetu kutumia cheo chake wala cheo cha mtu mwingine kwa faida yake (Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu), lakini Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa amekuwa akitumia cheo chake kujinufaisha yeye na genge lake.

Serikali imuagize Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa kuhakikisha fedha hizo zinarudishwa na CAG ahakiki kwamba fedha hizo kweli zimerudishwa na ikiwezekana kuwe na riba katika fedha hizo ambazo watu wamejipatia isivyo halali. Hii itasaidia kukomesha michezo michafu ambayo imekuwa ni mazoea kwa baadhi ya viongozi kama Dkt. Elirehema Doriye.
 
Back
Top Bottom