Uchambuzi wa Ripoti ya CAG (2020/2021): Shirika la Bima la Taifa

vtuko

Member
Jun 12, 2016
41
25
Katika ripoti ya CAG (2020/2021), miongoni mwa taasisi zenye madeni makubwa kabisa ni Shirika la Bima la Taifa (NIC). Shirika la Bima lina deni la shilingi bilioni 275.

Miongoni mwa mapendekezo aliyoyatoa CAG ni kwamba, taasisi zenye madeni makubwa kama NIC zipewe fedha kutoka Serikalini ili kuweza kuziondolea mzigo huo wa madeni.

Cha ajabu ni kwamba, jana kwenye mitandao ya kijamii imeonekana Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (Dkt. Elirehema Doriye) akitoa gawio la shilingi bilioni 1.5 kwa Serikali.

Kwa namna ya bima inavyofanya kazi, inamaanisha wengi wa wanaoidai NIC ni wabima, tena hasa wale wa bima za maisha.

Hivyo, kuna wanyonge wanateseka kwa Shirika kushindwa/kuzembea kuwalipa mafao yao huku Shirika likijipendekeza kwa Serikali kwamba linatoa gawio.

Hapa kuna mkanganyiko, yule anayehitaji kusaidiwa, ndiye anatoa mabilioni kwenda kwa yule anayetakiwa kumsaidia na wakati huohuo wanyonge wanaoidai NIC wanaendelea kuteseka na kuiwekea Serikali kinyongo kwamba haiwajali wanyonge waliochangia bima kwa kipindi cha muda mrefu, bima zao zimeiva, lakini NIC inashindwa/inazembea kulipa mafao yao kama mikataba yao ya bima inavyotaka.

Nitoeni tongotongo nami niyajue mambo haya…
 
Back
Top Bottom