Rais JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MkamaP, Jun 13, 2009.

 1. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Ushauri wangu kwa Rais wangu ni kuwa. Maendeleo ya nchi hayaletwi na kelele bali matendo.

  Utakubukwa kuwa Rais Bora kama utasimimamia KIDETE priorities hizi-
  1.Kutandaza Fibre Optics
  2.Mapinduzi ktk kilimo cha kisasa kwa large scale.

  Hakika ukishinda hayo hasa la kwanza utakuwa umetukombowa kutoka ktk umasikini.
   
  Last edited: Jun 13, 2009
 2. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sawa Mr. M
  Jaribu tena
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  R U in IT?
  Unaweza kunielimisha ni kwa vipi akitekeleza la kwanza atakua ametukomboa?
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Jamani msimfundishe kazi mzee wa Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya!! Subirini performance baada ya miaka mitano ambayo haijaisha.
   
 5. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hii la kwanza ni mhimu sana ktk utekelezaji na mwenendo wa uchumi ktk nchi yoyote.

  Kwanza Fibre optics zikitandanzwa bei ya mawasiliano inakuwa chini sana ,hivyo basi watu wanaweza fanya biashara yenye tija kwa wao na kwa Taifa kwa ujumla.

  Mfano unaweza kuwa na duka lako kwa njia ya mtandao bidhaa unanunua ukiwa nyumbani na kukufikia ukiwa nyumbani,watu hawatahitaji sana tena physical shop na vitu vyanamna hiyo,Hutahitaji sana kutafuta bangaloo pale kariakoo ili uanzishe biashara yani faida nyingi sana .
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu hatumfundishi ila tunatoa mawazo yetu ambayo tunaona yanafaa ktk mchakato wa ukuuaji wa uchumi wetu.Na nina kaasilimia kadhaa kuwa Rais hana utalaamu wa mawasiliano bali anaupata kutokana na washauri wake na maoni ya wananchi yani sisi.

  Nafikiri utakuwa ujuha kumwachia Rais afanye kazi ili sisi tuje tumfanyie tathimini ni kama dizaini ya kumukomoa ama mchezo ule wa kitoto ya kwamba "mwacheni si alijidai tuone atafika wapi" ,tukifikiri atayeumia ni yeye ama kuumbuka, kumbe wanaoumia na kuumbuka ni sisi wenyewe.

  Hivyo basi Wito wangu na miono yangu kwa Rais ni kwamba mwenendo aliouchukuwa japo bado si kwa vitendo yani ya kufanya mapinduzi ktk kilimo na utandazaji wa Fibre optics Ni njia CHANYA yenye mihili thabiti na iliyo na mwelekeo makini ktk ukuuji wa uchumi .

  Ambacho ningependa kukisema na ni imani yangu kuwa anakifahamu lakini nitakirudia tena na tena ni kuwa Kazi ya kutandaza hiyo backbone ama TRANSPORTING NETWORK si rahisi wenda kama anavyofikiria inahitaji commitment ya hali ya juu ,uangalizi makini na hali ya kufanya hivyo ndivyo vivyo kwa Kilimo.
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kuna paper nyingi sana zilizoandikwa zinazokataa kuwa uwepo wa IT unasaidia kuinua maisha ya wananchi wa kawaida. ( japo kuwa zipo nyingi zinazokubali pia)

  kwa vile faida ya unachokitaka hakiko dhahiri ( kitaaluma), nafikiri ungependekeza kufanywe mengine ya msingi zaidi kama kuhakikisha upatikanaji wa elimu kwa wote
   
 8. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Heshima mkuu.

  Mkuu mimi nakupinga kwa nguvu za hoja kwamba uwepo wa IT hakusaidii ukuwaji wa uchumi.

  Sitaki kuingia mbali sana kuelezea IT lakini itajitahidi kadri niwezavyo kuiweka role yake na umuhimu wake pia na faida ya moja kwa moja tofauti na unavyofikiri.

  Kwanza: Elimu: ukiwa na miundo mbinu makini ya mawasiliano upatikanaje wa ELIMU utakuwa wa kasi kwa bei rahisi tofauti na njia yoyote ile.Mfano
  upatikanaji wa mtandao wenye uhakika na affordable kwa kila mwananchi kutapunguza kabisa utegemezi mkubwa wa elimu wa kumtaka mwanafunzi kwenda ktk majengo ya shule ama chuo husika ili kujifunza.Kivipi? kutapunguza utegemezi huu?

  Ni kwa vile kutarahisishwa kwa kutengeneza system ambayo prof anakuwa UDSM pale dar wanafunzi wanajiunga na kumsikiliza ,kuona kuuliza maswali kwa kutumia ule mtindo wa CONFERENCE kokote ulipo eiza kutoka nyumbani ama maofini,yani kipindiki kikifika unachukuwa koputa unajiunga na lecuture inaendelea.
  Kwa kufanya hivyo kwanza kutapunguza bajeti ya kujenga majengo ,msongamano usikuwa na tija na ku enrole wanafunzi wengi kama sio wote wanaofaa kujiunga na na masomo husika.

  Kutampunguzia mwanafunzi mda na fedha za kutoka meru kuja kuishi Dar ili ahudhulie lecture pale udsm ,kutapunguza gharama za serikali kwa kutoa fedha za kujikimu kwa mwanafunzi na throughput ya wahitimu itaongezeka,yani faida nyingi na lukuki hata nashindwa kuzielezea.
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  1.Elimu bora
  2.Mfumo bora wa afya
  3.Utawala wa sheria
  4.ujasiriamali
  5.Mfumo bora wa kiuchumi

  Ina sikitisha kuwa wakati huu ambapo wenzetu wanaondokana na uchumi tegemezi wa kilimo sisi ndiyo kwanza tuna tafuta kuuboresha.

  Hiyo ya IT ina faida gani kama watu hawata kuwa na uwezo wa kutosha wa kutake advantage of the technology? Kama tuna zungumzia on the basis ya wachache sawa ila kama una suggest vitu vitakavyo nufaisha taifa zima kwa sasa hili siyo moja wapo.
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu MwanaFilosofia1, nakubaliana na yale uliyoyasema kuanzia moja mpaka tano,Hata hivyo sikubaliani nawe kabisa juu ya kuondokana na suala la kilimo.Mtu yeyote katika madaraka iwe ulaya ,Urusi au Marekani atatambua kuwa hilo ndilo suala la msingi kabisa katika uhai wa Taifa lolote.
  Ondoa chakula mezani mwa wananchi .hasa wa mijini, kwa muda wa wiki moja tu na huna nchi.
  Wafalme wa Ufaransa walipata joto kali na hatimaye kupinduliwa kutokana na njaa miaka ya 1700's.
  Kilimo ndo muajiri mkuu wa wananchi
  Kilimo ndio msingi wa viwanda karibu vyote
  Kilimo ndio changamoto ya mitandao yote ya mawasiliano ,ikiwemo barabara

  Kati ya wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula duniani ni hayo hayo mataifa makubwa -hence Kilimo.
  Kilimo kilisahauliwa kidogo katika miaka ya hivi karibuni.Hivyo basi kuzinduka huku kwa serikali na kukumbushia "KILIMO KWANZA" ambayo ni reflection ya Mwalimu ya "SIASA NI KILIMO" it is a welcome back to reality.
  Tusijejidanganya , hakuna mbadala kwa Kilimo
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Thanks mkuu kwa maelezo yako.
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mimi bado siamini unachokisema wezetu wanaondokana na kilimo,Hawa jamaa wanalima kwelikweli tena kwa ma large scale kweli kweli tena kwa kilimo cha mimashine mikubwamikubwa.

  Kukidharau kilimo ni kujaribu kuidanganya akili na hata hivyo bado nafikiri ni miujiza kwa nchi kuendelea kama chakula chote ni Tegemezi.Hawa watu hawategemei uchumi wao sana ktk kilimo ni kwasababu hali ya hewa yao iko LIMITED,na hata hivyo mda mchache takribani miezi mitano inayowaruhusu kufanya kilimo wanaitumia vilivyo na hata baadae Kutupatia MSAADA tunapokumbwa na njaa.Na kusema hawa jamaa hawalimi mie nafikiri ni PROPAGANDA zisizo na Tija .

  Pia naamini HAKUNA Elimu bora,Utawala wa sheria,mfumo bora wa afya,mfumo bora wa kiuchumi n.k sehemu palipo na NJAA.Kwa kufupisha ni kwamba hakuna binadamu mstaraabu aliye na njaa.

  Bado naamini ni swala ambalo limekaa ki intuitive zaidi ya kwamba binadamu hawezi kuwa na mipango na mikakati kabla hujashiba ,hivyo nafikiri kujikombowa kwetu kutakuja baada ya nchi yetu kutofikiri tena kesho tutakula nini.

  Pili maendeleo hayategemei yule kaacha lile ama hili ama kaendelea kwa lile ama lile bali yanakuja kwa kuitumia fursa iliyopo kwa ufasaha zaidi ,Fursa ya kilimo ni moja ya fursa malidadi ambayo inaweza kutukwamuwa kwani tukiweza zalisha chakula kingi nchi zinazotuzunguka zinahitaji zaidi chakula hicho wenda zaidi ya dhahabu ama tanzanite inavyohitajika ulaya.
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe mkuu. Ila nilicho kuwa nasema ni kwamba kwa wenzetu kilimo siyo the main employer na uchumi wao hau tegemea kilimo as heavily as ours. Asante kwa maoni yako mkuu.
   
 14. Marlenevdc

  Marlenevdc Member

  #14
  Jun 14, 2009
  Joined: Oct 1, 2008
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well said...
   
 15. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,865
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hakuna kitu mbaya kama njaa!!
   
 16. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu
  Njaa ndiyo chazo cha matatizo yote na cha mhimu zaidi ni kuidhibiti hii njaa na baada ya hapo ndipo mipango bora itakapofanyika na hatimaye maisha bora.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Jun 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwanfalsafa1,
  Mkuu ukitazama nchi hizo unazosema hazitegemei kilimo.. utagundua kwamba pato lake la kilimo pekee ni sawa na pato ya mataifa mengi kama sii yote ya Africa kwa ujumla wa vitu vyote....Kila mtu hujipima suti kwa umbo lake mkuu wangu huwezi kuiga kila kitu. Marekani asilimia 10 ndio wakulima lakini wanazalisha mara 2 ya pato zima la nchi zetu maskini, lakini ukichukua jumla ya pato la kilimo ukalinganisha na maswala mengine ndipo unaposema Kilimo hakitegemewi..

  Haya tazama basi pato kubwa la Tanzania linatokana na madini lakini ni asilimia chini ya 2 ya pato hilo linachangia mfuko wa serikali kwa sababu sisi bado ni taifa tegemezi tofauti na Marekani au nchi tajiri wanaochimba wenyewe na pato libakia ndani!..
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nimekuelewa sasa mkuu. Kwenye hilo la kilimo sina ubishi tena.
   
 19. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Kwangu nafikiri siasa za majukwaani tuzipe nguvu kidogo na nguvu nyingi tuelekeze ktk ile misingi ya kujenga uchumi.Na nafikiri uchumi ukishatengemaa siasa safi zitakuja zenyewe kwa njia yake yenyewe.
   
Loading...