Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Rais Jakaya Kikwete, keshokutwa Jumamosi, atarejea nchini Afrika Kusini kumzika Madiba!.
Kurejea huku kumetangazwa bungeni asubuhi hii na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,kufuatia swali la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zito Zuberi Kabwe aliuliza kwanini rais JK alihudhuria msiba wa Madiba bila kuandamana na ujumbe mzito wakiwemo Watanzania wawili pekee waliomtembelea Mandela tangu akiwa gerezani kwenye kisiwa cha Roben akiwemo JS Malecela?.
Naibu Waziri akajibu rais JK atarejea Bondeni kuhudhuria mazishi, this time atakwenda na ujumbe mzito ukijumuisha Makamo wa pili wa rais wa Zanzibar, Katibu Mkuu wa CCM na ujumbe mzito wa watu ambao rais ataona wanafaa kuwemo kwenye msafara huo.
Kuhudhuria huku ni muhimu na kunapelekea Madiba kupata heshima stahiki kutoka Tanzania.
Kwenye hili nawaomba sana tuungane kumpongeza JK kujitoa vilivyo kwenye misiba.
Kwa kumbukumbu zangu, huu utakuwa ni msiba wa pili kwa JK kuhudhuria msiba kisha kushiriki mazishi. Msiba wa kwanza ni ule wa Regia Mtema, JK alihudhuria Tabata kisha kuhudhuria mazishi Kilombero!.
Angalizo: Hili la misiba ni kwa mujibu wa kumbukumbu zangu tuu, inawezekana kuna misiba mingi JK alihudhuria mara mbili ila haiko kwenye kumbukumbu zangu!.
Rip Madiba!.
Pasco