Rais JK Kumzika Mandela na Ujumbe Mzito Kutoka Tanzania!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Wanabodi,
Rais Jakaya Kikwete, keshokutwa Jumamosi, atarejea nchini Afrika Kusini kumzika Madiba!.

Kurejea huku kumetangazwa bungeni asubuhi hii na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,kufuatia swali la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zito Zuberi Kabwe aliuliza kwanini rais JK alihudhuria msiba wa Madiba bila kuandamana na ujumbe mzito wakiwemo Watanzania wawili pekee waliomtembelea Mandela tangu akiwa gerezani kwenye kisiwa cha Roben akiwemo JS Malecela?.

Naibu Waziri akajibu rais JK atarejea Bondeni kuhudhuria mazishi, this time atakwenda na ujumbe mzito ukijumuisha Makamo wa pili wa rais wa Zanzibar, Katibu Mkuu wa CCM na ujumbe mzito wa watu ambao rais ataona wanafaa kuwemo kwenye msafara huo.

Kuhudhuria huku ni muhimu na kunapelekea Madiba kupata heshima stahiki kutoka Tanzania.

Kwenye hili nawaomba sana tuungane kumpongeza JK kujitoa vilivyo kwenye misiba.

Kwa kumbukumbu zangu, huu utakuwa ni msiba wa pili kwa JK kuhudhuria msiba kisha kushiriki mazishi. Msiba wa kwanza ni ule wa Regia Mtema, JK alihudhuria Tabata kisha kuhudhuria mazishi Kilombero!.
Angalizo: Hili la misiba ni kwa mujibu wa kumbukumbu zangu tuu, inawezekana kuna misiba mingi JK alihudhuria mara mbili ila haiko kwenye kumbukumbu zangu!.
Rip Madiba!.
Pasco
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,217
2,000
Hivi hana wasaidizi?!

Leo yuko Kenya baada ya kutoka South Africa na bado anapanga tena kurudi South Africa!

This is too much!

Watumishi wa umma hawalipwi malimbikizo yao wanaambiwa serikali haina hela lakini Raisi kiguu na njia!
Jk sasa inabidi aitwe 'Msafiri', msafiri itakua jina muafaka kwake. Hakika rais wetu anasafiri sana!
 

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,065
2,000
...Kwenye hili nawaomba sana tuungane kumpongeza JK kujitoa vilivyo kwenye misiba....
Kama mtu anajaribu kutizama priorities za nchi kwa kufuatilia kazi za rais, basi kwa nchi yetu bila ya shaka kipaumbele cha kwanza ni misiba! Hivi anapata muda kweli wa kushughulika na vipaumbele halisi vya nchi hii?
 

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728
2,000
Zurura yote hii ni kuua soo la kutakiwa kumuwajibisha PINDA na Hawa Ghasia kwani matarajio yake akirudi UPEPO utakuwa umepita na maisha yataendelea.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,979
2,000
Pasco unatamani sana Rais aseme atakwenda na wanahabari ili nawe ujipenyeze penyeze.......... na hivi umeshaanza kugusa gidamu cha kiatu chake dah!
Pasco Lowassa leo ni Pasco Kikwete
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,329
2,000
Hivi hana wasaidizi?!

Leo yuko Kenya baada ya kutoka South Africa na bado anapanga tena kurudi South Africa!

This is too much!

Watumishi wa umma hawalipwi malimbikizo yao wanaambiwa serikali haina hela lakini Raisi kiguu na njia!
Nadhani huyu jamaa, angestahili kupata aka ya Yohama mtembezi, au Vasco da gama, kwa namna anavyopenda kuzunguka sehemu mbalimbali duniani!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom