Rais - Jifunze Kutokana na Makosa ya Wengine

Well done Mkinga, uchambuzi na mantiki ya mada yako vinajitosheleza.

Ushabiki, ujinga, umaskini na kibri ndio sumu kubwa katika mioyo inayoojidhirisha kila kukicha katika mijadala mitaani na kwenye mitandao. Lakini weledi, busara na utashi wa kukaa na kujifunza kutoka kwenye historia vimetupwa mbali kwa sasa.

Tuko pabaya kwa sasa. Maendeleo sifuri, umaskini unaongezeka kila uchao na wakati huo huo uhuru na haki vinaminywa.
 
Labda rais wa bao!
Huyu hataki kabisa kuskia la mtu!!...ni mikwara tu..!! Historia huhukumu ukiwa bado ungali hai...!
 
Demokrasia ni uhuru wa kuamua mambo yanayokuhuru. Kwa upana zaidi, demokrasia ni mchakato wa kufikia maridhiano ya kijamii. Bila demokrasia hakuna maendeleo endelevu.
 
Hekima yatuasa kuwa Historia ni Mwalimu maridadi. Ni mwalimu mzuri kwa sababu hutuonesha yaliyowahi kutokea na athari zilizosababishwa. Hutuonesha pia watu maarufu kama vile watawala mazuri na mabaya waliyoyafanya, na hatimaye kulitokea ni nini. Wenye hekima hujifunza kutokana na waliyoyafanya wengine. Huiga kutoka kwa waliofanikiwa. Lakini pia huepuka kufanya yale ambaye yalifanywa na waliotangulia halafu yakasababisha madhara au dhahama kwao wenyewe au watu wa jamii zao.

Hulka ya binadamu mara nyingi ni kutafuta kile ambacho anakikosa sasa na kuacha kuthamini kile alicho nacho lakini akipata alichokuwa akikosa halafu ukamnyang'anya alichokuwa nacho kabla ndiyo utajua ni kipi kati ya vile viwili ni cha thamani kubwa zaidi kwake.

Tanzania kwa muda mrefu, japo siyo kwa kiwango timilifu, imekuwa ni nchi iliyojengwa kwa misingi ya kulinda uhuru wa raia wake yaani uhuru wa kutoa mawazo na uhuru wa kuamua. Safari yetu ya kuelekea kwenye ukamilifu haikuwa imenyoka lakini kwa ujumla haikuwa mbaya. Siku za huko nyuma, japo Mwalimu Nyerere alifuta mfumo wa vyama vingi lakini alijitahidi sana kuimarisha uhuru wa kutoa mawazo na kuchagua viongozi ndani ya chama. Na alisistiza sana juu ya umuhimu wa kufanyika maamuzi kwenye vikao. Nia ilikuwa ni kuzuia uwezekano wa maamuzi ya mtu mmoja. Uhuru huo unaweza kuwa haukuwa wa 100% lakini lengo lilikuwepo, na ndani ya katiba ya TANU na CCM hayo yaliwekwa wazi.

Pamoja na uhuru huo, Tanzania ilikuwa ni nchi maskini na ni maskini mpaka leo. Jambo la kushangaza ni kwamba Tanzania iliyokuwa maskini iliendelea kuwa ya amani na utulivu licha ya umaskini wa kutupwa wa watu wengi. Tanzania maskini ilikuwa na amani lakini mataifa mengi ya Afrika yaliyokuwa tajiri na huduma bora zaidi kuliko Tanzania yalikuwa na vurugu. Wapo watu wanadhani Tanzania ilikuwa na amani kwa sababu ya werevu au uzuri wa CCM au kwa sababu Mwalimu alikuwa na nguvu sana. Naamini Mwalimu alikuwa na nguvu sana lakini siyo nguvu ya misuli bali nguvu za kichwani. Aliijua vema hulka ya mwanadamu, alijua ni nini humletea mwandamu utulivu kuliko kitu kingine chochote. Alijua kuwa hitaji la kwanza la binadamu ni uhuru.

Huko Libya Muamaar Gaddafi alishindwa kuielewa hulka ya binadamu alidhani kilicho muhimu kuliko vyote ni barabara nzuri, hospitali nzuri, mishahara mizuri, ajira, nyumba nzuri, posho za kila mwezi, kuwaletea wanamuziki wakubwa, shule nzuri, na kuwalipia mahari wanaotaka kuoa. Akaamini kwa kuwa ametenda hayo basi atapigiwa vigelegele kila atakapokwenda. Pamoja na kuwapa hivyo vitu vyote, aliwanyima raia wake uhuru, wengine wakazuiwa kufikiri, akataka afikiri yeye pekee yake kwa niaba yao, waliojaribu kuhoji walikiona cha mtemakuni, na wengine walipoteza maisha.Muammar Gaddafi hakuruhusu sauti ya kumhoji wala ya kumwambia kuwa amekosea.

Kuzuia uhuru wa wananchi wa kulijenga chuki kubwa miongoni mwa wananchi wa Libya. Ilipopatikana nafasi ya kumwondoa Gaddafi, maelfu ya wananchi wake waliokuwa wakimshangilia siku zote, waliotakiwa kumlinda na kumpigania waligeuka kuwa maadui zake. Gadaffi aliyekuwa akiona ni jambo dogo kuwaua raia waliokuwa kinyume chake alipoona kifo kikimsogelea alikimbilia mtaroni kwa nia ya kukikimbia kifo. Kabla ya kifo chake alimwomba muuaji wake ambaye ndugu zake walikwishapotezwa na Gaddafi kumsamehe lakini haikusaidia. Muuaji wake ambaye aliagizwa kumkamata Gaddafi akiwa hai ili ashitakiwe hakuweza kuishinda hasira yake iliyotokana na kupoteza jamaa zake wakiwa chini ya utawala ya vyombo vya dola vya Gadaffi.

Leo wananchi wa Libya wapo katika maisha ya mashaka makubwa. Aliyeyasababisha hayo yote ni Gaddafi maana alikosa maono ya hitaji muhimu kuliko yote la binadamu. Yeye ndiye aliyejenga mazingira ya kuchukiwa. Laiti angewapa uhuru angeweza pia kujua wananchi wake wana fikra gani juu ya utawala wake.

Hitaji la kwanza la binadamu ni uhuru (siyo madaraka). Mwanadamu kwa asili anataka uhuru. Hii ndiyo sababu hata leo hii wapo vijana wanaotoka kwenye familia tajiri maeneo ya Masaki, Mbezi Beach, Mikocheni, familia zenye idadi kadhaa ya nyumba kwenye compound zao lakini wakifikia muda wa kujitegemea, walio wengi wanaoondoka hata kama wazazi wao wapo tayari kuwapa nyumba ndani ya compound wanazomiliki. Wapo tayari kuacha nyumba zenye viyoyozi na kuhamia kwenye nyumba zenye madirisha yaliwekwa tu nyavu za mbu huko Sinza au Mwenge, nyumba zisizo na AC wala vioo. Kwao viyoyozi na Masaki si kitu bali UHURU ndiyo hitaji lao la kwanza.

Upatikanaji wa mahitaji mengine huwa ni kwaajili ya kuimirisha na kuulinda uhuru. Watu wanataka ajira ili wawe na mapato yao, kisha wayatumie mapato hayo kuimarisha uhuru wao. Watataka wawe na nyumba zao, watataka wawe na familia zao, watataka wafanye maamuzi yao kwa sababu wana uwezo wa kuyagharamia maamuzi yao. Watu wanataka barabara nzuri na za kutosheleza ili wawe na uhuru wa kuamua watumie njia gani kwaajili ya kwenda wapi, na kwa muda wanaoutaka. Watu wanataka kuwepo na shule nzuri za aina tofauti tofauti, wanataka hospitali, n.k, hivyo vyote wanataka viwaongezee uhuru. Ukiwaondolea uhuru, hata kama utawapa hayo mahitaji yote, watakushangilia kwa muda tu kwa sababu ya hulka ile ya binadamu ya mara nyingi kufikiria kile asichokuwa nacho ni bora kuliko alicho nacho.

Nimeyasema haya kwa sababu siku hizi kuna fikra zimeanza kujengeka miongoni mwa watanzania kuamini kuwa uhuru siyo muhimu, demokrasia siyo muhimu, kilicho muhimu ni kuhakikisha watoto wanasoma bure, watoto wana madawati, barabara zetu na viwanja vya ndege vinakuwa vizuri, zahanati zinakuwa na madawa, n.k. Hivi vitu ni muhimu, tena ni muhimu sana lakini siyo muhimu kushinda UHURU WA RAIA. Ni rahisi sana kumfanya maskini aliye huru kuwa mtulivu kuliko tajiri aliyenyimwa uhuru.

Rais JPM afanye kazi kwa nguvu zote kwa kushirikiana na wananchi kwaajili ya kuupunguza au kuuondosha umaskini lakini kwa lengo la kuimarisha uhuru maana uhuru wa binadamu unakuwa mashakani pale nchi au mtu anapokuwa maskini wa kupindukia. Huduma nzuri za kijamii zilenge kuimarisha uhuru. Tusiue uhuru na demokrasia tukadhani kwamba huduma za kijamii ni mbadala wa uhuru na demokrasia. Huduma za jami ni polish ya uhuru na demokrasia.

Naona waliowengi tumeanza kubadilika kutoka kumtusi mh Rais nasasa tunaanza kutoa ushauri wa kiutu uzima.Hii ni safi sana.Wote tukifanya hivi naamin mh rais akili itatulia na kweli atatutendea haki
 
Well said, ila sijui kama ushauri utafika mahala pake.
 
Well spoken, good food for thought, masikitiko yangu ni ule msemo wa "Sikio la kufa huwa halisikii dawa"!!
 
Libya twajifunza athari za autocracy ! Mwandishi ameeleza kila kitu kwa weledi wa hali ya juu.badala ya kumshambulia tujikite kuangalia maoni haya yatatusaidiaje watanzania kujenga umoja,amani na ustawi wa taifa letu bila kuingiza mihemko na ushabiki wa kisiasa(kivyama).
Hebu rudia na kuisoma aya ya kwanza kwa umakini neno kwa neno,mstari baada ya mstari.

Hawa akina wakudadavua usiwajibu nadhani ni akina Juliana na yule wa mtoto wa kigogo wa ccm
 
great wisdom tangu nimejiunga Jamiiforums

mleta mada ahsante
 
Hii maada ni chakula kizuri cha ubongo...kwakweli sina la kuongezea..shukran sana mtoa mada.
 
Back
Top Bottom