Rais Jakaya Kikwete njiani kuelekea Kenya kwenye mahadhimisho ya miaka 50 ya Nchi hiyo

Wajinga wenye husuda, chuki na choyo na gubu ya mioyo ndio mnaandika km ulivyoandika hapa. Kwa akili za maiti hivi lazima ufe maskini

we mbwa jibu hoja, kwanini mr jk anakimbilia kwenye sherehe za uhuru kenya wakati ya kwetu juzi alisusiwa na marais wote wa EAC? Usipende kutetea ujinga, tabia hii ya kujikombakomba inatuudhi watz
 
Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru leo.
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwaongoza Watanzania pamoja na wakuu, wawakilishi na mabalozi wa nchi zaidi ya 40 duniani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika leo.


Miongoni mwa wakuu na wawakilishi hao wanatoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).


Wengine ni wakuu na wawakilishi kutoka Benki ya Dunia (WB) na Umoja wa Afrika (AU).
Sherehe hizo zilizotanguliwa na mkesha wa Desemba 9 juzi, zitafanyika kitaifa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.


Mkesha huo ulifanyika katika viwanja vya Kawe, Mnazi Mmoja na Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam, ulipambwa na burudani mbalimbali, ikiwamo ufyatuaji wa fataki.


Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Saidiki, ambaye mkoa wake ni mwenyeji wa sherehe hizo, mbali na kuhudhuriwa na wakuu na wawakilishi hao, sherehe hizo zinatarajiwa pia kupambwa na burudani mbalimbali.
Burudani hizo ni pamoja na vikundi vya sanaa pamoja na vijana wa halaiki.


Pia zinatarajiwa kupambwa na gwaride maalum kutoka majeshi ya ulinzi na usalama, litakalokaguliwa na Rais Kikwete.
Desemba Mosi, mwaka huu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema wakuu wanane wa nchi, makamu watatu wa rais na mawaziri wakuu watatu kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADAC) walikuwa wamethibitisha kushiriki katika maadhimisho ya hayo.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha, Pinda, alisema kuwa kutokana na ugeni huo, serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama imeimarisha ulinzi kukabiliana na tishio lolote la ugaidi kutoka kundi la Al-Shaabab cha nchini Somalia.


“Ulinzi siku hiyo utaimarishwa vya kutosha kuhakikisha viongozi, wakuu wa nchi na wageni waalikwa,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Hata hivyo, Pinda hakuwa tayari kuwataja viongozi hao kwa majina na nchi zao, kwa maelezo kuwa ni mapema kutokana na sababu za kiusalama.


Pinda alisema kuwa sherehe hizo pia zitapambwa na gwaride maalumu kutoka vikosi vya ulinzi na usalama, maonyesho ya zana na vifaa vya kivita na halaiki na uhamasishaji itayohusisha vijana 6,550 kutoka shule za msingi na sekondari.


Waziri Mkuu alitaja makundi mengine maalum yatakayohudhuria kuwa ni wazee maarufu, viongozi wastaafu na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wakuu wa vyama vyote vya siasa nchini.

Mr BigMan nadhani una mwili mkubwa Kama unavyojiita bigMan,na kutokana na imani za Wajapani,watu wenye miili mikubwa wana akili ndogo,wanaamini kwamba oxygen inayoenda ubongoni kwa wenye maumbo makubwa ni ndogo hivyo hupelekea watu hawa kuwa na akili ndogo,nimesema hakuna hata Rais mmoja wa EAC aliyekuja,we unatuletea uozo huu,sehemu gani wametaja Rais wa EAC?,Bingu wa Muthatika(RIP) alikuwa wa EAC?
 
Mwacheni aende kuna siku atakuta ikulu imetekwa na wengine, mnayakumbuka ya Uganda yule raisi alikuja Tz kwa Nyerere halafu ikulu yake likaingua li mtu marehemu Idd Amini
 
Wakenya na wana EAC wengine wakiwa wanatudharau waTZ tusichukie coz hizi ndio sababu zenyewe,tulipokuwa tunasherehekea miaka 50 ya uhuru wetu ni Rais gani wa EAC alikuja?,na juzi ni nani alikuja?,kwa nini hatuna priorities Nchi hii?,sasa Urais wa Tz unadhalilishwa sana na huyu Mh.,eeeh mwenyezi Mungu kwa nini umetunyima akili waTZ za kujenga Nchi yetu na kutupa ujinga wa kujijengea heshima nje ya Nchi wakati Nchi yetu masikini,wajinga na mafisadi ya kupindukia?,iko wapi akili uliyowapa wengine ukatunyima sisi?inauma kwa kweli.

Jamaa yangu wewe umesema yote. na nimeyasema hivi hivi kwenye uzi mmoja uliopita hivi majuzi, kuwa majirani hata viji nchi vidogo vilivyotuzunguka vinatuona Wa Tanzania wote hatuna maana na kuwa ni watu wa hovyo na tuliokosa vipaumbele (priorities) kama jinsi viongozi wetu walivyo wa hovyo.

Kwa ujumla majirani hawa kipimo cha tabia ya Tanzania kuwa ni watu wa hovyo ni viongozi wetu wenyewe. Na ni kweli kuwa taasisi ya Urais imekuwa ya kienyeji mno. Wanadai Rais wa Tanzania anaweza akatokea hata kwenye msiba wa kaka wa Rais wa nchi jirani bila ya mwaliko.

Utakumbuka Rais wetu ndiye aiyekua kidedea wa kuwangia kifua na kufanya 'shuttle diplomacy' kwenye majukwaa ya kimataifa dhidi ya mkono wa sheria wa ICC kwa ajili ya akina UhuRuto. Na wakati huo huo hao akina UhuRuto wenyewe changanya na maswaiba wao akina M7 na PK waki mtenga.

Halafu muda si muda anakuja kulia faulu bungeni kuwa majamaa wanam 'sideline'. Sasa unajiuliza kuwa kiongozi huyu mbona amekosa 'pride' kwa taasisi ya Urasi anayoingoza na WaTanzania kwa ujumla.
 
Lala salama hiyo mheshimiwa kula vyako bana, acha wenye wivu wa kike...
 
Aende2 tena aweke bili kabisa kwenye ndege,ila ninachouliza,Huwa hachoki kukaa kwenye pipa??
 
Jamani huo ni mwaliko wa "Happy besdeim Kenya 50 years"
Mwacheni akasafishe meno bhana. Jirani akikukaribisha kwa shughuli Yake lazima uje.
 
Mods huu uzi umewekwe kinafiq sana. Safari zote ni muhimu kw taifa letu. Asingeweza kukosa maziko za mandela na pia hawezi kukosa miaka 50 ya uhuru wa majiran zetu. Haitaleta picha nzuri ukizingatia mahusiano tuliyonayo

Kweli nimekubali, ukiwa CCM lazima unakuwa na akili ya maiti.
 
Sipingi safari ila duh kusema ukweli zimezidi, yani kila kitu Rais anafanya mwenyewe, hadi hollywood kuitaftia nchi njia kwenye movie industry akaenda yeye, representatives wote wamekaa wanafanya nini? hizo kazi zina watu wake au kibongobongo anawajibika sana since anakula mshahara zaidi ya 90% ya marais Afrika..
Cha ajabu wao hawaji, wanaleta vibaraka huku...
 
Kwa mara nyingine tena Rais Jakaya Kikwete amepiga safari ya juu kwa juu toka South Afrika to Kenya kwenye mahadhimisho ya Miaka 50 ya nchi hiyo iliyopata uhuru mwaka 1963.

Hii safari yake nje ya nchi inamfanya rais wetu kuwa nje ya nchi kwa takribani miaka 3 toka aingie madarakni na miezi kadhaa.

Traveller tena, na bado mbona.
 
Safari nje ya nchi zaendelea kutafuna fedha.

Kwa mujubu wa taarifa ya Kamati ya Bunge la Bajeti iliyowasilishwa na mwenyekiti wake, Andrew Chenge, fedha zote zilizopitishwa na Bunge katika bajeti ya mwaka huu 2013/14 kwa safari za viongozi nje ya nchi zilimalizika ndani ya miezi miwili.
Hivi sasa serikali inatumia fungu la dharura.

Source: Gazeti la Mwananci la leo
 
Mr BigMan nadhani una mwili mkubwa Kama unavyojiita bigMan,na kutokana na imani za Wajapani,watu wenye miili mikubwa wana akili ndogo,wanaamini kwamba oxygen inayoenda ubongoni kwa wenye maumbo makubwa ni ndogo hivyo hupelekea watu hawa kuwa na akili ndogo,nimesema hakuna hata Rais mmoja wa EAC aliyekuja,we unatuletea uozo huu,sehemu gani wametaja Rais wa EAC?,Bingu wa Muthatika(RIP) alikuwa wa EAC?

Nakubaliana na wewe wenye mwili mdogo una akili sana,pamoja na akili zako nyingi nimeshindwa kuelewa kama umesoma vizuri mpaka comment za Pinda,lakini haijarishi kitu hoja je Rais kuna umuhimu wa kwenda ? Je kuna haja yoyote ya jirani akifanya hivyo nawe ufanye hivyo hivyo ? Je mazingira ya miaka mitatu iliyopita na sasa inafanana ? Nini nafasi ya Kenya baada ya kupata safu mpya ya uongozi ? Pamoja na akili zangu ndogo basi labda naweza kuelimika kupitia kwako mkuu
 
Nadhani tunahitaji kubadilisha foreign policy yetu kuwa ya kimanufaa zaidi ya kiuchumi kuliko kushikiria uhusiano tu na heshima,dunia imebadilika hata Africa ya sasa sio ile ya kipindi kile cha kupigania uhuru,Tanzania tunachekwa na kudharauliwa sana na majirani na bado tunapoteza resources nyingi kujitafutia sifa,tutapata sifa zaidi pale ambapo uchumi wa Nchi utakuwa juu na kujenga Taifa la watu welevu wapenda maendeleo na wanaotafuta Elimu zaidi na sio Imani za kishirikina kwa kila jambo,tunahitaji ukomavu wa kisiasa,tunahitaji visionary leaders,anayejua dunia ilipotoka,ilipo na inapokwenda.
 
Nakubaliana na wewe wenye mwili mdogo una akili sana,pamoja na akili zako nyingi nimeshindwa kuelewa kama umesoma vizuri mpaka comment za Pinda,lakini haijarishi kitu hoja je Rais kuna umuhimu wa kwenda ? Je kuna haja yoyote ya jirani akifanya hivyo nawe ufanye hivyo hivyo ? Je mazingira ya miaka mitatu iliyopita na sasa inafanana ? Nini nafasi ya Kenya baada ya kupata safu mpya ya uongozi ? Pamoja na akili zangu ndogo basi labda naweza kuelimika kupitia kwako mkuu

Mr BigMan sio lazima jirani akifanya kitu na wewe ufanye,ila lazima Nchi iwe na priorities,sio lazima kusafiri na kuhudhuria kila kitu,wakenya wa Jana,wakenya wa Enzi za jomo Kenyatta na wakenya wa Leo na kesho ni walewale,kwani ni uongozi gani uliotu sideline?mimi naishi na Wakenya nawaelewa vizuri sana,ni watu wa interest sio uhusiano na kujenga sifa Nje ya Nchi.
 
Jamani aende tu mana tumechoka,hapitwi?.Amenikumbusha jamaa mmoja kwetu akisikia kuna ki event sehemu au siku ya Idd anatafuta ndizi na kijiko anaweka kwenye mfuko wa kanzu lake anaenda huko.Pilau ikiwa tayari anatoa ndizi mbivu mfukoni
 
Yes , watanzania tuna matatizo ya akili, hata uwe tajiri kiasi kama huna akili ni bure, na tunaongozwa na "accidental leader" ambao hata wao wanajiuliza hivi hawa tunaowatala wana akili kweli?
 
Back
Top Bottom