Rais Jakaya Kikwete Akutana na Wamachinga Mkoani Mwanza,Awapiga Tafu Shilingi Millioni Kumi

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
[h=1]Rais Jakaya Kikwete Akutana na Wamachinga Mkoani Mwanza,Awapiga Tafu Shilingi Millioni Kumi[/h]

ch1.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wawakilishi wa kundi moja la wachuuzi (machinga) wa jijini Mwanza ambao leo January 6, 2012 walikwenda Ikulundogo ya jiji hilo na kumweleza changamoto zinazowakabiri, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji pamoja na taaluma ya kufanyia biashara. Rais Kikwete ametoa milioni 10 kwa ajili yawamachinga hao kukopeshana mitaji.Picha na IKULU
 
Hata kama angewapatia mtaji wa milioni 100 bado ni fisadi tu!

Hizo ni kodi zetu!
 
Wamachinga gani hao, kama sio wanatumia mgongo wa machinga kupata hako kamkate kisha wagawane!
 
Si kazi rahisi kuwarubuni watu wa mwanza, jk anatwanga maji kwenye kinu tu. Mwanza ccm bye bye!
 
Pesa chukueni, kuleni ni haki ya jasho lenu na ushuru mnaolipa, lakini mambo yetu yale kama kawa, haongwi mtu hapo!
 
Ule mfano wa 'malofa' unawahusu hao vijana? Na ni lini atatoa hela kwa machina sehemu zingine? Hapo magogoni wanapita kila siku mbona hasalimiani nao au kuwapa mahela?
 
Huyu jamaa kweli ni sifuri inayoelea........a floating zero.

Yani baada ya kuongea na hao watu sijui saba ambao wapo chini ya ulinzi.........(angalia kuna polisi kila mahali),
akaona tatizo lao ni mtaji? au ni yale yale ya CCM..........kugawa ubwabwa na vipapatio na buku mbilimbili.....

Hiyo hela ndo itawapa sehemu ya kufanyia biashara?

huyu jamaa sijui kwa nini hajifunzi, aka akili ya aina gani huyu?
 
Back
Top Bottom