Ni wakati sasa wa kumuangukia Ridhiwan Kikwete na kumfikiria kwenye nafasi za juu hapo baadaye?

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
1,669
2,000
Ijumaa khareem,

Kwaunyenyekevu mkubwa naomba kuwarejesha awamu ya nne Pale tulipoambiwa kuwa Mtoto wa Rais wa Tanzania wakati huo Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, Ridhiwani Kikwete amekamatwa huko Hong Kong China akifanya biashara ya madawa ya kulevya,

Kwakuwa sheria za Nchini China ukiiondoa Beijing mtu yeyote akikamatwa na madawa ya kulevya hukumu yake ni kunyongwa mpaka kufa na kuna mamia ya Watanzania wamenyongwa nchini China sote ni mashahidi wa hili "Watanzania tukashangaa huyu mtoto wa Rais anakosa nini kwa baba yake mpaka abebe unga tena yeye mwenyewe mpaka China?!! "

Tukaambiwa baada ya Ridhiwani Kikwete Mtoto wa Rais wetu kukamatwa na kutakiwa kunyongwa mpaka kufa baba yake Mzee Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Rais wa awamu ya nne akafanya makubaliano na mamlaka za China zisimnyonge mwanae Ridhiwani Kikwete na badala yake atawapa gesi yote ya Mtwara inayofikia 57.7tct jambo ambalo walilidhia na ushahidi ni kwamba Ridhiwani yuko hai hata leo,

Awamu iliyopita tukaambiwa Mtwara gesi yote ilishauzwa kwa Mabeberu na mambo yaliyofanyika huko Si-yakizalendo kabisa hivyo tuwekeze nguvu kwenye JHNPP ilikujipatia Umeme wa uhakika nchini,Mimi akili yangu kwa haraka ika 'Click ' ni ule mchongo wa Mzee Jakaya kwa Ridhiwani na Wachina hakika moyo Wangu ukamchukia Mzee Jakaya na Mwanae Ridhiwani kwa kutaifisha gesi yetu Chaajabu baadae kidogo tukamsikia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akimtaja tena Ridhiwani Kikwete kwamba ni mwanamtandao wa wauza madawa ya kulevya ( Unga ) Tanzania naamini hili sakata sote tunalikumbuka binafsi nikazidi kuichukia familia ya Mzee Jakaya na Dk Jakaya mwenyewe kwa dhuluma kubwa waliolifanyia Taifa hili,Mungu nisamehe Mimi na Wale walioumizwa kama Mimi kwa uongo

Leo nikaribu mwongo mmoja umepita tunaambiwa mazungumzo baina ya Serikali ya Tanzania na Makampuni ya Shell ya Uingereza na Uholanzi, ExxonMobil ya Marekani,Ophir ya Uingereza, Pavilion ya Singapore,Medco Energi ya Indonesia; na StatOil ( Equinox ) ya Norway wanaendelea na Host govnment agreement ( HGA ) ili wawekeze $30bl karibu Shilingi 69.5trilioni ili kuwekeza kwenye gesi ileile ya 57.7tct aliyoitoa Mzee Jakaya Mrisho Kikwete ili kumnusuru mwanae mpendwa Ridhiwani Kikwete muuza madawa,hakika nchi ngumu sana hii,

Mimi na wenzangu tunajiuliza gesi yetu yote Tanzania ilianza kugunduliwa tangu miaka ya 1974,1982 na ilipofika miaka ya 2000's ndio tukajua ujazo halisi wa gesi yetu kuwa ni Jumla ya futi za ujazo trilioni 57.7ctc ambazo zilikuwapo awamu ya kwanza hadi hii ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan,

Najiuliza|Tunajiuliza,

1. Kama deposit ya gesi yetu yote imesalia kuwa ni 57.7tct tangu enzi za baba wa Taifa hadi leo zama za Mama Samia hiyo gesi aliyotoa Mzee Jakaya kumnusuru mwanae Ridhiwani asinyongwe hadi kufa ni ipi?

2. Kama nia ilikuwa kumchafua Mzee Jakaya wakati wa Utawala wake kwanini Ridhiwani aendelee kutajwa kwa ubaya hata awamu ambazo baba yake hakuwa madarakani?

JIBU NI MOJA TU :

Mhe Ridhiwani Kikwete ni kijana mnyenyekevu sana,Mchamungu,Mpole,Mtu wa bashasha wakati wote,Hana makundi,Mzalendo wa kweli,Asiyependa vyeo japo vyeo vinamtaka,na anayechukia rushwa kwa vitendo,Nimtu asiyependa mtu yeyote anyanyaswe akiwa ndani ya nchi yake,Nimtu anayefikiri juu ya Umoja wa Kitaifa ndio maana katika hotuba zake zote hakuwahi kusigana na Upinzani wala Wapinzani na nikijana aliyekulia na kulelewa na The core CCM yaani Ridhiwani ni CCM by blood,

Nimekumbuka usemi mmoja " mti wenye matunda ndio huchakazwa kwa mawe" ila muda ni mwalimu wa kweli leo Dunia imegundua Ukweli kuwa "Ridhiwani kinachomtesa nikile alichopewa na Mungu kwaajili ya kuwatumikia Watanzania hapo baadae" kwa dhati ya moyo wangu leo nimempenda na kumuheshimu sana Mzee Jakaya Kikwete pamoja na familia yake hii aliyeifunza Unyenyekevu na subra,Leo Mungu amewatetea pale mlipokaa kimya kwa kukosa mtetezi,

photo_2021-10-29_09-49-04.jpg
#HAKIKA TULIKUTENDA#TUSAMEHE SISI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom