Rais Jakaya Kikwete aanikwa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Jakaya Kikwete aanikwa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 13, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Na Saed Kubenea - Imechapwa 07 September 2011


  [​IMG]


  MAISHA binafsi ya Rais Jakaya Kikwete, kabla na baada ya kuwa rais yameanza kuanikwa duniani kote kwa njia ya mtandao ambako anatuhumiwa hata "kupewa zawadi ya suti" na fedha taslimu.

  Kwa mujibu wa taarifa za sasa, uchokonozi wa maisha ya Rais Kikwete umeanzia mwaka 2005 katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.

  Imedaiwa Jakaya Kikwete, alipewa fedha taslimu dola za Marekani 1,000 za kugharamia ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Kilimanjari-Kempinski iliyoko jijini Dar es Salaam.

  Aidha, imedaiwa kuwa aligharimiwa nauli ya kwenda Uingereza na kurudi. Aliyegharimia safari hiyo ametajwa kuwa ni Ali Albwardy, raia wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE).

  Madai mengine ni kwamba mfanyabiashara Ali Albwardy, ambaye ndiye mmiliki wa Kilimanjaro-Kempinski, "alimwezesha" Kikwete kwa kiasi cha dola milioni moja za Kimarekani (sawa na Sh. 1.6 bilioni), kwa ajili ya shughuli za kutafuta urais mwaka huo.

  Mtandao wa WikiLeaks, mashuhuri duniani kwa uibuaji taarifa nyingi za kibalozi na watawala duniani hivi sasa, unamweka Kikwete kwenye orodha ya viongozi wa ndani na nje ya Afrika ambao matendo yao yaliyofanyika ufichoni, yameanza kuanikwa.

  Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu alikana Kikwete kupelekwa nje na mtu yeyote, kushonewa nguo na kupokea fedha zozote, akisema "hakuwa akikusanya fedha" za chama chake.

  Rweyemamu aliwaambia waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam, Jumatatu kuwa madai ya WikiLeaks ni "matusi na dharau kubwa" kwa rais, akiongeza kuwa kama ni hatua nyingine "itachukuliwa kitaasisi."

  Hii ni mara ya pili Kikwete kutajwa katika tuhuma za aina hiyo. Mwaka 2005 alidaiwa na gazeti la African Analysis la nchini Uingereza kuwa alipokea "mabilioni ya shilingi" kutoka Iran ili zimsaidie katika mbio za kugombea urais.

  Gazeti lilidai kuwa aliyepewa fedha hizo kumpelekea Kikwete alikuwa Rostam Aziz, mmoja wa maswahiba wake.

  Taarifa hizo zilipovuja na kusambaa, Kikwete aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa hiyo ilikuwa kashfa na kwamba alikuwa amefungua kesi dhidi ya gazeti na mwandishi.

  Lakini siku tatu baada ya kauli ya Kikwete, mwenye gazeti la African Analysis, Ahmed Rajab alisema "hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa" na kwamba alikuwa akiisubiri kwa hamu. Hadi leo hakuna kilichosikika kutoka kwa Kikwete.
  Taarifa za WikiLeaks zinasema fedha za mfanyabiashara zilikabidhiwa kwa Kikwete mwenyewe katika hafla maalum iliyofanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro-Kempinski.

  Katika taarifa yake ya 30 Agosti 2011, mtandao huo unasema pia kuwa Bw. Albwardy aligharamia ununuzi wa jozi tano za suti za "hadhi ya kimataifa" kwa Kikwete.
  Balozi Michael Retzer wa Marekani wakati huo, kwa mujibu wa mtandao huo, anamnukuu meneja wa hoteli ya Kempinski, Bi. Lisa Pile akisema Kikwete alipewa fedha hizo, ikiwa ni mchango wa mfanyabiashara huyo kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

  Mtandao haukueleza iwapo Kikwete aliwasilisha fedha hizo kwa uongozi wa CCM; jambo ambalo linaweza kuzaa mtafaruku kati ya Kikwete na chama chake – kama hakuwasilisha.

  Balozi Retzer ananukuliwa akisema Kikwete alikubali kupokea fedha za mmiliki wa Kempinski pamoja na kuandaliwa safari ya matembezi nchini Uingereza.
  Katika majibu yake juzi, Rweyemamu alikana madai kuwa Kikwete alisaidia "Mwarabu" kupata hoteli ya Kilimanjaro na ujenzi wa hoteli katika mbuga za wanyama za Serengeti na Ngorongoro.

  Lisa Pile anayetajwa kuthibitisha Kikwete kupewa fedha anaelezwa na mtandao huo kuwa ni raia wa Australia. Ameishi nchini tangu mwaka 2004 akifanya kazi katika hoteli ya Kempinski.

  Kwa sasa, Pile ameajiriwa katika hoteli ya Sukhothai, iliyopo mjini Bangkok, nchini Thailand ambako ni meneja mtendaji msaidizi wa masoko katika hoteli hiyo tangu Oktoba 2008.

  Kabla ya kuja nchini, Lisa Pile alifanya kazi kama hiyo nchini China katika misururu ya hoteli za Kempinski.

  Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja katika kipindi ambacho Kikwete na chama chake wameshindwa kujitetea dhidi ya tuhuma za ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT) kabla ya uchaguzi mkuu wa 2005.

  Miezi mitatu iliyopita, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (PCCB), Edward Hoseah alinukuliwa na mtandao huo akisema, "Vita vya kupambana na ufisadi nchini vimekuwa vigumu kutokana na Kikwete kukingia kifua baadhi ya watuhumiwa wakubwa."

  WikiLeaks linamnukuu Balozi Retzer akisema, "katika tukio la 18 Oktoba 2005, mtu ambaye inasemekana ana uraia wa India au Asia ya Kusini na ambaye anahusika katika masuala ya biashara na Ali Albwardy, ghafla aliita Pile na kuanza mazungumzo katika lugha ya Kiswahili."

  Anasema, "Sina uhakika na walichokisema. Lakini jina la Jakaya Kikwete lilitajwa mara nyingi sana na baadaye alimkabidhi bahasha ambayo ilikuwa na dola za Marekani 1,000 ambazo zingetumika kulipia ukumbi wa mkutano ambao Kikwete aliufanya katika hoteli hiyo."

  Pamoja na kwamba Kikwete amekuwa mteja wa kila mara katika hoteli hii, lakini Balozi Ratzer anasema, "Hakuna mahali popote ambapo jina lake linaonekana katika vitabu vya kumbukumbu" vya hoteli hiyo.

  Katika hali ambayo mtandao unasema ilimwacha mdomo wazi, Balozi Ratzer anajihoji: "Haya yote yana maana gani?…nahisi kwamba Ali Albwardy ana mkono katika fedha za mafuta nje ya Falme za Kiarabu. Nahisi kutoa nguo za bure na mchango katika shughuli za uchaguzi, kunalenga ufanikishaji wa biashara hizo."

  Balozi Ratzer anamtaja Anthony Diallo ambaye alikuwa waziri wa kwanza wa maliasili na utalii kwenye serikali ya Kikwete, kuwa amepanga kuongeza mchango wa utalii nchini ili usaidie kukuza uchumi.

  Kutajwa kwa Diallo kunatokana na hoja kuu moja. Ali Albwardy aliahidiwa na serikali kupatiwa haki ya kujenga hoteli mbili kubwa nchini – moja ikitarajiwa kujengwa katika eneo la Ngorongoro na nyingine katika mbuga ya wanyama huko Serengeti, mkoani Mara.

  Mtandao unasema Lisa Pile alikuwa anafahamu hata siri za Baraza la Mawaziri. Kwa mfano, raia huyo wa kigeni, anaeleza Balozi Retzer, alikuwa akijua kuwa "Serikali ina mpango wa kupeleka bungeni mswada utakaoruhusu ujenzi wa hoteli mpya ya kitalii kwenye maeneo ya hifadhi." Alisema mswaada husika ulikuwa uko katika ngazi ya baraza la mawaziri.

  Hata hivyo, ujenzi wa hoteli hizo tayari umesitishwa baada ya serikali kupingiwa kelele na wanaharakati wa mazingira na mashirika ya kutetea haki za wanyama duniani.

  Kwa mujibu wa sheria za hifadhi, hakuna ruhusa inayotolewa kwa ajili ya ujenzi wa kudumu wa aina yoyote katika hifadhi za kitaifa.

  Bi. Lisa ananukuliwa na mtandao akisema hadi kufikia Desemba 2005, mmiliki wa hoteli ya Kempinski atakuwa amefungua hoteli kama hiyo visiwani Zanzibar.

  Balozi Retzer anasema, "Utabiri wa mama huyo ulikuwa sahihi. Tayari Ali Albwardy amefungua hoteli yake ya Kempinski katika eneo la Pwani ya Mashariki mwa Zanzibar toka 5 Januari 2006."

  Balozi Retzer ananukuliwa akisema Albwardy alipata eneo la kujenga hoteli Zanzibar chini ya saa 12 tangu atoe maombi yake kwa rais hadharani.


   
 2. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa mazingira yetu ya kitanzania (2005) nadhani mpaka sasa hili si suala la kumlaumu sana JK, kwani watanzania wengi wanautamaduni wa kupokea vi zawadi, kwa hiyo hili suala mpaka kuja kufikia ukomo ni mpaka kizazi labda kijacho. Mfano ulaya mtu ukimpa zawadi anakuuliza maswali mengi na hata viongozi wa serikali akipewa zawadi anatakiwa aiweke wazi na pengine asiichukue kuogopa kuharibu sifa yake. Kwa hiyo kwa hili nchi kama Tanzania na watu wake tunahitaji kujifunza na kuelewa kuwa zawadi siyo nzuri na hili limekithiri sana kwenye serikali yetu (Mfano halisi nilishuhudia na kila siku inaendelea kutokea=Board of directors wa asasi mbalimbali za serikali hupokea either laptop mpya, au pesa eti kama zawadi).
   
 3. m

  makaptula Senior Member

  #3
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hii inanifanya niamini kwamba mchakato wote wa kubomoa mahakama na kufanya paking ya magari kwa ajili ya wageni wa kilimanjaro kempiski kuwa
  ni mchezo mchafu wa Raisi wetu
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Wamekosa ya kuandika. Vijiba vya roho vimewakaa. Mtamuona hivi hivi handsome man, hata akivaa gunia anapendeza. Wambili havai moja, wastara haumbuki.
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Hehe handsome boy kumbe pamba za kununuliwa!! Always tulijua wananunulika viongozi wetu lakini sikujua kwamba wako cheap kiasi hiki!
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Lahaula la kuwata..........
   
 7. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,378
  Trophy Points: 280
  Yaani JK ni wa ajaaabu sijapata kuona. Thanx to wikileaks. Dunia imeshamjua.
   
 8. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Wa Tanzania tunaendekeza njaa sana ndo tatizo letu
   
 9. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br /> Handsome mwizi?
   
 10. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hii habari meshaexpire siku nyingi na ikulu tayari imeshalitolea hili swala ufafanuzi. Waandishi siku hiz naona wamekosa cha kuandika
   
 11. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ukweli unauma eh kumbe nguo zote anazovaa ni za kuhongwa? ni aibu kweli mwanaume kuhongwa kama mwanamke
   
 12. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Wape basi wewe chakuandika kama unaona wamekosa cha kuandika msiwe wanafiki kwa kutetea wakati wewe mwenyewe umekalia msumari wa moto
   
 13. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Urais sio mchezo bhana Nyerere alisema hilo sasa mnaona? waswahili kuwapa nchi kuongoza tabu kweli
   
 14. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Safi sana wikileaks, lakini kama haya yalikuwepo kwa nini mnatuletea katika kipindi hiki, jamaa anapeta, bado miaka 4 amalizie ngwe yake.
  Tunawaomba kiongozi mtarajiwa yeyote wa nchi hii, mtuanikie matendo yake mapema.
   
 15. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Mkubwa! Naunga mkono hoja!
   
 16. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wewe na handsome wako wote Masaburi
   
 17. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tuendelee kujenga nchi yetu kwa aman na upendo. ila Haki siku zote...
   
 18. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  waendelee kumdharilisha maana yeye ameshadharilisha taifa huwezi kuhongwa suti kama rais ni aibu ya mwaka
   
 19. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2011
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  mmh,utumbo wa kuku.
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Naipenda sana misemo yako................
   
Loading...