Rais Hussein Mwinyi na CAG Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
665
430
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Viongozi na watendaji wa Wizara na Idara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutekeleza wajibu wao katika kusimamia mifumo ya ukusanyaji na matumizi ya fedha za Serikali, huku akibainisha kuwa Serikali haitegemei ripoti ijayo ya mwezi June, 2022 kusheheni lundo la dosari.

Dk. Mwinyi ametoa indhari hiyo Ikulu Jijini Zanzibar baada ya kupokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), hafla iliohudhuriwa na Makamo wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman, Makamo wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdulla, Mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema viongozi na watendaji hao wana wajibu wa kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kusimamia mifumo ya ukusanyaji na matumizi ya fedha, huku akionya endapo ripoti ijayo itafanana na ile iliowasilishwa kwake hii leo, itamaanisha bado Viongozi na Watendaji hao hawajachukua hatua zinazostahili.

Alisema suala la Bajeti ni muhimu katika kutekeleza mipango ya Serikali na kusisitiza kuwa hilo sio jukumu la CAG pekee bali ni la Viongozi na Watendaji wote.

Alisema kila mmoja ana wajibu wa kurekebisha hali hiyo na kusema malalamiko mengine yanayotolewa na watendaji hao hayazingatii wajibu walionao katika kusimamia makusanyo na matumizi ya fedha za umma.
 
Huwezi kuwa msafi katika sehemu iliyo oza juhudi za rais Mwinyi zinakwamishwa na Wana CCM
uko sahihi, huyo CAG ni kama chura tu katika mto hazuii ngombe kunywa maji.

Ripoti iliopita aliibua ufisadi wa kutisha, wawakilishi wa CCM wakasema yeye mwenyewe hana uhalali kwani hakuchaguliwa kisheria.LOL
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom