Rais Hussein Mwinyi awataka Vijana kuacha tabia ya kuchagua kazi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,669
2,000
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema serikali inatambua ukubwa wa tatizo la ajira linalowakabili vijana na tayari imeanza kuchukua hatua kutekeleza ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana.

Dk Mwinyi aliyasema hayo katika kilele cha matembezi ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwenye Uwanja wa Mao Zedong, Zanzibar jana.

Aliwataka vijana kujituma kufanya kazi na waache tabia ya kuchagua kazi.

Alisema wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu CCM iliahidi kukabili tatizo la ajira na ahadi hiyo imeanza kutekelezwa kupitia wawekezaji walioanza kwenda Zanzibar kwa nia ya kuwekeza katika miradi mbalimbali.

Dk Mwinyi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alisema Serikali inakusudia kuendelea kuwajengea uwezo vijana kupitia mfuko wa uwezeshaji kiuchumi na kuimarisha shughuli za ujasiriamali ili kuwawezesha wananchi wajitegemee.

Alisema jamii ya Wazanzibari inakabiliwa na matatizo likiwemo la kutowajibikaji kwa watendaji wa serikali, hivyo akawataka vijana kujitambua na kuisaidia Serikali katika mapambano hayo.

Kuhusu kaulimbiu ya matembezi hayo isemayo ‘Uzalendo na Uwajibikaji ni Msingi wa Maendeleo ya Zanzibar kufikia Uchumi wa Bluu’, Dk Mwinyi alisema amevutiwa na ujumbe huo kwani unakwenda sambamba na malengo ya Serikali ya Awamu ya Nane kuhakikisha inapata maendeleo ya haraka ya kuchumi kupitia uchumi huo.

Alisema matembezi hayo ni kielelezo kuwa vijana wa CCM wanathamini Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964, ikiwa mwanzo wa safari ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanzania.

Alisema vijana ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa kuwa wao ni msingi muhimu wa uzalishaji.

Alisema mapinduzi ya 1964 yalifungua milango ya kujitawala na kuleta uhuru, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kufanya kazi.

Alisema mshikamano ndio utakaofanikisha amani na utulivu nchini na kufanikisha ndoto ya maendeleo, hivyo akatoa rai kwa wananchi kudumisha amani.

Dk Mwinyi aliupongeza uongozi wa UVCCM kwa kuandaa matembezi hayo kila mwaka katika kipindi cha shamra shamra za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.

Aliwahakikisha vijana kuwa Serikali itafanya jitihada kuweka mazingira bora ya Chuo cha Vijana kilichopo Tunguu ili kiendelee kuzalisha vijana wengi zaidi wazalendo.

Alisema Serikali imejipanga kuzipitia upya sheria zote zenye utata ama kukinzana, huku akiahidi kuendelea kuwapa fursa za uteuzi vijana katika ngazi mbalimbali.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James alisema jumuiya hiyo inatambua dhima iliyonayo katika mapambano dhidi ya vitendo vinavyorudisha nyuma maendeleo ya nchi, hivyo akabainisha kuwa inaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Nane.

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Mussa Haji Musa alisema matembezi hayo yalihusisha vijana 750 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar na kuzinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdallah Januari 5, mwaka huu katika kijiji cha Pwani Mchangani.

Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, akiwemo Makamu, Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, mawaziri, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Abdallah Juma Sadalla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Ahmed Said
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,021
2,000
Mwinyi ananena maneno ya mwenye shibe. Tuliyategemea maneno haya ya kejeli kwa vijana.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
56,161
2,000
Yaani huko Zanzibar kazi ni nyingi kiasi kwamba vijana wanabagua kazi? Kuna dogo ana Masters ameomba leo kazi ya u mortuary attendant kwenye hospital ya Kimataifa ya Chato
 

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,337
2,000
Ni kweli kabisa kuchagua kazi sio jambo jema lakini Serikali nayo inapaswa kuwatengenezea vijana mazingira mazuri ya kujiajiri na pia kuzipa ahueni investment za wazawa ili kuongeza ajira kwa vijana.
 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,840
2,000
Zile ajira alizoahidi zishaanza kuota mbawa.
Lazima aje na kauli mbadala.

'Vijana msichague kazi"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom