Rais Hollande aulizwa Ukapera Ikulu hadi lini?

Rais Hollande aulizwa Ukapera Ikulu hadi lini?

Nicolas J Clinton Gabone

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
897
Reaction score
559
Rais wa sasa wa Ufaransa, Francois Hollande, ameendelea kuisha Ikulu ya nchi hiyo bila mke huku akikataa kusema chochote kuhusu taarifa zilizozagaa kwamba anaweza kumuoa kipenzi wake asiye rasmi, mwigizaji Julie Gayat. Hollande aliachana na mzazi mwenzake mwanamama Valerie Trierweiler, January mwaka huu baada ya kiongozi huyo kubainika kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji huyo. Hollande alizaliwa Agost 12 Mwaka 1954 ni mwanasiasa alipata fursa ya kushika madaraka mbalimbali nchini humo, ikiwa ni pamoja na wadhifa wa katibu mkuu wa chama cha kisoshalisti cha Ufaransa kati ya mwaka 1997 na 2008. Alichaguliwa kuwa Rais wa Ufaransa Mei 6 mwaka 2012 akamshinda Rais aliye kuwa madarakani wakati wa kinyang'anyiro cha uchaguzi huo Nicolas Sarkozy na aliapishwa kuingia Ikulu Mei 15, mwaka huo. Kumbe na Dr Slaa anaweza sasa huku Prof Peter Mutharika wa Malawi akiwa ameoa baada ya kuwa Rais wa nchi hiyo. Hapa wanaotoaga matusi kwa Dr Slaa hamna hoja kabisa.
 
Uzuri wa Ufaransa hata rais akienda big brother hawana shida
 
Back
Top Bottom