matumbo
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 7,224
- 3,960
Juzi juzi tu hapa nilikuwa napitia tovuti moja ya radio.. nikasoma kwamba mheshimiwa raisi ameahidi atawaleta usher Raymond na Terrence Jay. Wasanii hao kutoka marekani watakuja kuendesha semina kwa wasanii wa bongo kuhusu sanaa ya Muziki, Filamu na mengineyo. Wasanii, mashabiki na wadau kadhaa wa muziki wameibuka na kutoa maoni yao juu ya ujio huo wengine wakipinga na wengine wakiunga mkono.
Nimekuwa nikijiuliza tu je! Haya maamuzi anayoyafanya mheshimiwa raisi huwa anapata wapi ushauri au huwa anaamua kwa mtazamo gani..? Nimekuja kugundua kwamba wasanii na wadau walioko karibu na mheshimiwa raisi ndiyo wanaochangia kwa kiasi kikubwa kutoa vipaumbele wanavyovitaka wao bila kujali mamia ya wasanii wanataka nini.. kwa mfano.. kulikuwa hakuna msanii ambaye alikuwa anataka studio ya mastering kwanza… wasanii wote wa aina zote za sanaa walikuwa wanataka HAKI MILIKI KWANZA kwa kazi wazifanyazo.
Ukiyaona ya Usher Raymond na Terrence J kuletwa bongo na mshua ni makubwa sana.. ngoja nikupe ya steve Nyerere ndipo utagundua ile kauli ya Luchi (2014) kwamba "Ni kitu gani ambacho wasanii tumefanya kwa elimu tuliyoipata mara kwa mara kutoka BASATA na COSOTA, kuna msemo Yule mwenye kuaminika kwa kidogo hudhaminiwa kwa kikubwa'.. je, Mheshimiwa Jakaya kikwete tumekuwa waaminifu kwa kidogo.".
Tunaweza kuona Luchi anatoa duku duku lake kubwa lakini mwanzoni alianza kwa kupongeza kwa juhudi ambazo Mheshimiwa amezifanya… anakuwa anaturudisha kulekule kwa wabunge ambao huwa wanaanza kwa kuunga mkono hoja alafu katika kuchangia akatoa changamoto kibao… sasa unaungaje mkono kitu chenye mapungufu… haiwezekani hiyo… tuache nidhamu za woga… kama wazo ni bovu sema bovu kama zuri sema zuri… enewei tuyaache hayo.
Leo Nilikuwa natazama You Tube marudio ya kipindi cha Mkasi cha Salama Jabir kilichoruka hewani 23/1/2012 ndipo nilipojionea maajabu ya Steve Nyerere. Niiweke vizuri hii Steve Nyerere ni raisi wa Bongo Muvi… anawakilisha wasanii wa filamu .. steve alianza kwa kusema kwamba "..tuna bahati sana sisi wasanii… tumepata… raisi anapenda sanaa.
Hakuna raisi tutakuja kumjutia akiondoka madarakani kama huyu kwa sisi wasanii, jamaa anaipenda anaifeel sanaa.." Kwa kauli hii nimetamani ndugu wa marehemu Kanumba, Mangwea, Langa, mzee small, Adam kuambiana, Muhidin Gurumo na wasanii wote waliokufa kipindi cha Mheshimiwa wajibu swali hili wanafaidika vipi na kazi za wapendwa wao baada ya kufariki… then steve Nyerere anawaambia watajuta siku raisi akiondoka madarakani… khe!! Sasa watajuta mara ngapi… hapo penyewe wanajuta wanaona bora wapendwa wao wangekuwa wanafanya kazi sehemu zingine sasa hivi wangekuwa wanashuhurikia kupata mafao kwenye mashirika ya Hifadhi za Jamii (PPF,LAPF n.k)
Katika mahojiano hayo Salama alimuuliza Steve kwamba ni faida gani ambayo ameipata, na vile vitu alivyokuwa anawapromise je wamevipata pia…? Katika swali hili steve alijibu majibu mawili.. Alijibu kama ifuatavyo.
KWANZA…."unajua raisi ni kitu kingine mungu wa pili huyo, mtu yeyote anapokuwa raisi ni mungu wa pili huyo, faida niliyoipata tu kukaa nae kula naye tu Yule bwana ni faida, yaani tukae tu tumeongea na raisi mimi kwangu ni faida hiyo, ni sifa ndani ya maisha yangu.
PILI…"lakini pia vilevile faida niliyoipata kwa Yule bwana anapokuwa anaelewa kwamba kuna mtu anaitwa steve Nyerere ndani ya nchi hii…"
TATU.. "sapoti ya familia yake… (wananiuliza) kwamba steve unataka kufanya nini.. tukupe mzigo…. Wanakwambia kabisa kweli utafanya.. tukupe mzigo.. bei gani.. unawaambia "nina shida na milioni mbili" anakwambia shika hii hapa kafanye mdogo wetu… ile ni moja ya sapoti… unajua ukipewa na mtoto ni sawa kama umepewa na baba"
Kwa staili hii kama Tanzania bado tuna wasanii wanaona fahari kula dinner na raisi kuliko kutafuta maslahi ya wasanii wote, unashangaakumsi kia Ommy Dimpoz kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya muungano juzi juzi tu (26/4/2014) wakati steve nyerere alishasema hivyo tangu mwaka 2012. Naanza kusadiki kwamba wasanii huwa wanakutana na mheshimiwa lakini hawamuelezi matatizo ya msingi matokeo yake wanaishia kupata shoo za kampeni tu na kupiga picha na mheshimiwa.
Katika miaka 50 ya muungano, katika miaka 53 ya uhuru wa Tanganyika na katika miaka 50 ya mapinduzi ya zanzibar lakini bado msanii wa Tanzania hayuko huru na ni mtumwa wa umaarufu wao wanaona raisi akishawafahamu ndio wamemaliza maisha ndio maana wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini ya muungano aliwatambua kama mnagombania umaarufu na sio wafanyakazi kama wafanyakazi wengine.
Kwa hali hii unaanzaje kulalamika juu ya ujio wa Usher Raymond na Terrence Jay kwa kutumia Kodi za umma ili wasanii wa bongo wapate nafasi ya kupata Breakfast, Lunch, Dinner na mtu mzima Usher Raymond.. wakati ndio vipaumbele vya wasanii wanaomzunguka raisi….
Kinyoooooonge…… basi mimi naona raisi yuko sawa tu awalete mwanawani wapige nao picha… itatusaidia kimataifa…. Mheshimiwa hajakosea kabisa... ikiwa raisi wa wasanii wa muvi anafikiria hivi.. hao waigizaji wanafikiria nini.. enewei CHENCHI IMEBAKI.
Imeandikwa na Malle Marxist