Rais, Fukuza Washauri Wanaofanya Vetting

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,525
41,040
Urais ni taasisi kubwa sana, unaotegemea sana utendaji wa idara mbalimbali. Idara hizo zisispofanya kazi vizuri, lawama zote zinaenda kwa Rais na Serikali nzima.

Ukweli ni kwamba, hata kama tutakuwa na pesa nyingi kiasi gani, hata tukawa na vyanzo vya kuingiza pesa nyingi kiasi gani, bila ya kuwa na watu sahihi kila eneo, ni kupoteza muda, na nchi hii haitafika popote.

Fikria kuwa nchi hii mwaka 1961 wakati tunapata uhuru, tulikuwa sawa na nchi kama Malaysia, Thailand na Singapore. Lakini leo tumeachwa mbali kiasi cha UNDP kueleza kwamba sisi tukiendelea na mwendo ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu, Malaysia wakabakia palepale, sisi itatuchukua zaidi ya miaka 250 kuwafikia: Fikiria kwa taarifa za 2021

Tanzania GDP $67.8 billion
Malaysia GDP $373 billion
Thailand GDP $505.9 billion
Singapore GDP $397 billion

Ufahamu kuwa:

Malaysia ina watu milioni 33

Singapore ina watu milioni 5

Thailand ina watu milioni 71

Pekee tulichowazidi hawa ni uwezo wa kuzaliana, kwa sababu kuzaliana hakuhitaji akili wala maarifa. Wanyama wenye akili kidogo kama nyumbu ambao ni kitoweo cha simba wanazaliana kuliko simba. Nzi mdudu asiye na akili na anakufa baadabya siku chache, anatotoa maelfu ya watoto kwa siku chache za maisha yake. Kuzaliana sana kusiko na mpangilio siyo sifa, kama ni sifa, basi inaobesha uduni wa akili.

Ukijiuliza, kwa nini haya yote yanatokea? Jibu sahihi ni aina ya watu tulio nao. Ni aina ya viongozi tulio nao. Ni aina ya watendaji tulio nao.

Viongozi wanaoamini maisha ya watu wa nchi na maendeleo ya nchi yanaweza kupatikana kwa kuhamasisha kazi ya bodaboda, umachinga au umama nitilie, hata siku moja hawawezi kubadilisha ustawi wa Taifa hili.

Viongozi wanaoona unyonge na umaskini wa wananchi ni sifa badala ya kuuona ni laana, hawawezi kulibadilisha Taifa hili.

Tuna watu wasio na uwezo wa kujenga mifumo bora ya uzalishaji bali usiku na mchana wanapanga namna ya kuiba kidogo kinachopatikana.

Bila ya kuwa na mifumo ya kuwatambua na kuwatumia watu wenye maono, wanaochukizwa na umaskini, walio maadui wa rushwa lakini wanaojivunia uadilifu na mafanikio, watu waliosheheni ubunifu, kwenye maeneo ya maamuzi, usimamiaji na utekelezaji ndani ya Serikali na taasisi zake, sisi kuhusu maendeleo, tusahau, tusahau, tusahau kabisa.

Kwa sasa, ifahamike, kuna maafisa ambao wanafanya kazi ya kumsaidia Rais katika kuwatambua watu wanaostahili kupewa uteuzi. Kwenye hili anaweza kuomba kupewa majina ya watu safi, wenye maadili, uwezo kwa kutegemea sifa alizoziweka. Lakini pia anaweza kuja na jina, akawapa watu wake kutaka kupata ukweli wa sifa, uwezo na uadilifu wa mtu huyo.

Lakini kinachotokea kwa sasa, ni baadhi ya hawa wanaofanya vetting, kuitumia nafasi waliyopewa kujinufaisha wao wenyewe kwa kupewa fedha na wanaofanikiwa kupata nafasi za uteuzi. Kwa kuwa wanakuwa wamehongwa, sifa zinazohitajika kwa nafasi ya uteuzi zinawekwa pembeni, kwao kilicho muhimu ni pesa waliyohongwa. Hii inafanyika zaidi kwa wale ambao tayari ni wateuliwa, na wanataka au wabakie hapo hapo kwenye nafasi walizoteuliwa au wapande zaidi, hata kama wana madudu na uchafu mwingi.

USHAURI KWA RAIS

Kama Rais amemteua au kumbakiza Waziri fulani wakati wa mabadiliko kwa kuegemea taarifa za wanaofanya vetting, halafu huyo waliyempa sifa nyingi za uwongo ama akaonekana kuwa mwizi, mbadhirifu au uwezo duni, anapoondolewa huyo mteuliwa, fukuza na wale wote waliofanya vetting iliyosaidia mtu huyo kuipata nafasi aliyopewa.

Mawaziri, wakurugenzi, makatibu wakuu, wanahangaika wakati wote kuwatambua watu walio karibu sana na Rais, kwa lengo moja tu, kuwahonga ili taarifa zao zimfikie Rais zikiwa na sifa nyingi za uwongo.

Rais, awe na watu wanaofuatilia kwenye taasisi binafsi na makampuni binafsi, waliopo ndani na nje ya nchi, kuwatambua watanzania wenye fikra chanya na wenye uwezo na uadilifu wa hali ya juu, ili watu hao waweze kupewa nafasi muhimu katika kulibadilisha Taifa hili lililozama kwenye tope la uduni, siyo kwa sababu ya kukosa rasilimali asilia bali kukosa rasilimali watu sahihi kwenye maeneo mengi mbalimbali.

Vigezo vya sifa za mtu kupata nafasi katika ofisi za umma, zitazamwe upya, maana kuna watu wengi kwenye ofisi za umma zaidi ya kuwa na uadilifu duni, hata maarifa na uwezo wao wa kufanya kazi ni duni sana, ndiyo maana mashirika yote ya kibiashara na huduma yaliyo chini ya Serikali, hakuna linalofanikiwa.
 
Anafukuza kisha analeta wapya wazee wale wale wenye ideology sawa na waliotoka.
Sasa ndugu yangu, unategemea tija kweli, kwa mfano yule Mzee wetu kutoka sijui Bunda, yeye tangu enzi za Mwalimu Nyerere tayari ni kiongozi, na hadi Leo bado anateuliwa na ndio ' think tank' wa kusaidia kuleta mabadiliko chanya??? Yaani tutakuja fika, tumechooka kwelikweli.....
 
Sasa ndugu yangu, unategemea tija kweli,kwa mfano yule Mzee wetu kutoka sijui Bunda, yeye tangu enzi za Mwalimu Nyerere tayari ni kiongozi, na hadi Leo bado anateuliwa na ndio ' think tank' wa kusaidia kuleta mabadiliko chanya??? Yaani tutakuja fika, tumechooka kwelikweli.....

Ni kweli ulichosema mkuu
Ila ukikaa ukafikiria tena viongozi vijana walioteuliwa wakina Nick, Babu Tale, wakina Msukuma ambao wanavikwa PhD feki ndio unazidi kuchoka kuhusu hii nchi. Sijui tunakwenda wapi. Ifike mahala CCM waachie hii nchi
 
Na kweli, vijana nao tuliowajaribu nao ni majanga.....kazi kwelikweli......
Ni kweli ulichosema mkuu
Ila ukikaa ukafikiria tena viongozi vijana walioteuliwa wakina Nick, Babu Tale, wakina Msukuma ambao wanavikwa PhD feki ndio unazidi kuchoka kuhusu hii nchi. Sijui tunakwenda wapi. Ifike mahala CCM waachie hii nchi
 
Ili upate watu wenye uwezo ni lazima ukubaliane na mfumo wa uwazi na uwajibikaji. Nafasi nyingi za 'teuzi' zilipaswa kufanyiwa usaili wa wazi.

Pili tumezidisha kuwa na SIRI, kila kitu nchi hii ni siri, manunuzi, mikataba n.k, kwenye giza ndiko uovu unashamiri. Mambo yasiyohitaji kiwa siri yawekwe wazi ili watu wawajibike.

Ni lazima na yeye SSH abebe sehemu ya lawama, serikali yake, wateule wake.
 
Urais ni taasisi kubwa sana, unaotegemea sana utendaji wa idara mbalimbali. Idara hizo zisispofanya kazi vizuri, lawama zote zinaenda kwa Rais na Serikali nzima.

Ukweli ni kwamba, hata kama tutakuwa na pesa nyingi kiasi gani, hata tukawa na vyanzo vya kuingiza pesa nyingi kiasi gani, bila ya kuwa na watu sahihi kila eneo, ni kupoteza muda, na nchi hii haitafika popote.

Viongozi wanaoona unyonge na umaskini wa wananchi ni sifa badala ya kuuona ni laana, hawawezi kulibadilisha Taifa hili.

Tuna watu wasio na uwezo wa kujenga mifumo bora ya uzalishaji bali usiku na mchana wanapanga namna ya kuiba kidogo kinachopatikana.

Bila ya kuwa na mifumo ya kuwatambua na kuwatumia watu wenye maono, wanaochukizwa na umaskini, walio maadui wa rushwa lakini wanaojivunia uadilifu na mafanikio, watu waliosheheni ubunifu, kwenye maeneo ya maamuzi, usimamiaji na utekelezaji ndani ya Serikali na taasisi zake, sisi kuhusu maendeleo, tusahau, tusahau, tusahau kabisa.

USHAURI KWA RAIS
Rais, awe na watu wanaofuatilia kwenye taasisi binafsi na makampuni binafsi, waliopo ndani na nje ya nchi, kuwatambua watanzania wenye fikra chanya na wenye uwezo na uadilifu wa hali ya juu, ili watu hao waweze kupewa nafasi muhimu katika kulibadilisha Taifa hili lililozama kwenye tope la uduni, siyo kwa sababu ya kukosa rasilimali asilia bali kukosa rasilimali watu sahihi kwenye maeneo mengi mbalimbali.

Vigezo vya sifa za mtu kupata nafasi katika ofisi za umma, zitazamwe upya, maana kuna watu wengi kwenye ofisi za umma zaidi ya kuwa na uadilifu duni, hata maarifa na uwezo wao wa kufanya kazi ni duni sana, ndiyo maana mashirika yote ya kibiashara na huduma yaliyo chini ya Serikali, hakuna linalofanikiwa.
Naunga mkono hoja, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

P
 
Ni kweli ulichosema mkuu
Ila ukikaa ukafikiria tena viongozi vijana walioteuliwa wakina Nick, Babu Tale, wakina Msukuma ambao wanavikwa PhD feki ndio unazidi kuchoka kuhusu hii nchi. Sijui tunakwenda wapi. Ifike mahala CCM waachie hii nchi
Huwa nakupendaga sana, ila naona umeanza kurukwa na akili umekua mjinga
 
Ili upate watu wenye uwezo ni lazima ukubaliane na mfumo wa uwazi na uwajibikaji. Nafasi nyingi za 'teuzi' zilipaswa kufanyiwa usaili wa wazi.

Pili tumezidisha kuwa na SIRI, kila kitu nchi hii ni siri, manunuzi, mikataba n.k, kwenye giza ndiko uovu unashamiri. Mambo yasiyohitaji kiwa siri yawekwe wazi ili watu wawajibike.

Ni lazima na yeye SSH abebe sehemu ya lawama, serikali yake, wateule wake.

Umenena ukweli kwenye suala la uwazi. Usiri huashiria giza, na giza ni alama ya uovu. Mambo mengi maovu hufanywa kwa siri, hufanywa gizani.

Wakati wa awamu ya 5 tukajitoa kwenye uendeshaji wa Serikali kwa uwazi. Sijui tulikuwa tunakimbia nini kwenye uwazi!! Turudi kwenye uwazi ili uovu uweze kuwa dhahiri wakati wote. Kujitoa kwenye uwazi, bila shaka kulilenga kuyafanya maovu yasifahamike ili tujisifu kuwa kwa sasa hakuna uovu.

Uwazi hautafuta uovu ila uovu utaweza kufahamika na kushughulikiwa mapema kabla ya madhara makubwa.

Viongozi ambao wameshindwa kusimamia idara zao, na wizi ukatokea, majina yao yatangazwe wazi, yawekwe kwenye vyombo vyya habari, na wasishike nafasi zozote za umma kwa kipindi kisichopungua miaka 5.

Watuhumiwa wa wizi, watangazwe wazi, na wakipatikana na hatia waadhibiwe kwa mujibu wa sheria, na baadhi ya adhabu wasiruhusiwe kushika nafasi yoyote ya umma maisha yao yote.
 
Inapofika wakati wa kuteua watendaji wa serikali, rais anaangalia uccm wao, wakiharibu mambo asishangae
 
Back
Top Bottom