kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Rais Magufuli ni mzalendo kwelikweli wa taifa hili anayeipenda nchi yake sawa na walivyo Baba wa Taifa Mwl Nyerere na Robert Mugabe.
Bahati yao mbaya ni kuwa wanazipenda sana nchi zao lakini hawana uwezo wala namna ya kuyatatua matatizo ya kiuchumi ya wananchi wao kwa kuorodhesha tu ubaya wa wakoloni mamboleo. Ukoloni ulikuwepo, upo, na utakuwepo. Mzee Nyerere, Gadafi, na Mzee Mugabe hawakufua dafu kiuchumi pamoja na kuthubutu kuuorodhesha ubaya wa wanyonyaji.
Wakoloni ndio wenye mitaji, teknolojia na masoko ya kuchimba na kununua madini yoooote duniani. Bahati mbaya viongozi wetu wanaoingia mikataba na wakoloni hawa hawana tofauti na akina Mangungo wa enzi zile. Maana bila kuyachimba na kuyauza madini hayatakuwa na maana yoyote kwetu na sisi uwezo wa kuyachimba wenyewe bado uko mbali sana. Tunachohitaji ni win-win kwenye kuchimba.
Taifa liketi chini bila kubaguana, tushirikishwe kujadili nini chakufanya juu ya maliasili zetu na taifa letu. Rais peke yake hana na hatakuwa na majibu ya tatizo hili la kimfumo na kihitoria. Sanasana bila kujali dini wala vyama atuunganishe kupata katiba na Sheria safi zitakazoweza kulinda rasilimali zetu kikamilifu, hata ikibidi kutoa adhabu za vifo kwa walafi.