Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Tanzania ya mshikamano

Nicolas J Clinton Gabone

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
892
Reaction score
536
RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN NA TANZANIA YA MSHIKAMANO

Na, Nicolas Jovin Clinton Gabone.
Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Vijana wa Mageuzi (JUVIMA)-NCCR-Mageuzi
Dar Es Salaam
4 May 2025.

Rais Samia Suluhu Hassan ni moja ya wanawake wachache wenye uwezo na nguvu ambao wamefanikiwa kuongoza Mataifa yao hapa Afrika ikiwemo yeye ambaye amepata nafasi ya kuiongoza JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ambalo ni Taifa lenye ushawishi wake hapa Afrika na Duniani kote tangu kuasisiwa kwake, sifa ya TANZANIA sote tunaijua ulimwenguni kote ni sifa njema ambayo tunasema Karibu wote msiyokuwa na makwao

Tangu ameongoza Nchi hii alianza kama nyota njema inayoangaza matumaini mapya ya Watanzania (waliyowengi) kutoka kwa mtangulizi wake, mvuto na nyota yake vilianza kuchomoza kabla hata ya mtangulizi wake kufariki Dunia, wahanaharakati na wanasiasa ikiwemo na mimi tulimpigia chapuo kama kiongozi shupavu sana mwenye jicho la huruma, anayependa maendeleo lakini mama mwema sana na ni mama mwema sana lakini amebadilika sana tena sana!

Leo nijaribu na mimi angalau kuzungumza na wewe Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kuhusu Tanzania ya mshikamano wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 7 wa vyama vingi hapo mbele mwaka huu 2025.

Mheshimiwa Rais ni wazi kuwa kuna milio ya haki na amani kila kona ya Tanzania, kuna wanaoimba haki na wengine amani lakini kwa sauti zile zile, naamini unasikia sauti hizi za watoto wa Mama Tanzania ambao wewe ni muangalizi mkuu wa sauti hizo.

Mama Rais, Tanzania mpaka sasa imegawanyika vipande tayari tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu kibaya zaidi na masuala ya dini yameanza kujipenyeza, hili ni suala la Hatari sana kuna wanaotetea kwa kuzani wewe ni muumini mwenzao na wengine wakisema wanaambiwa kwa sababu wewe ni wa dini ile...!

Wewe kama muangalizi mkuu wa Mama Tanzania ni muhimu sana uwe na masikio milioni 70 kwa wanaokupenda na wasiyokupenda ndivyo ilivyo hata Yesu hakupendwa na wote ila yeye aliupenda Ulimwengu, naamini unaipenda Tanzania na wewe.

Maoni na Ushauri wangu kwako Mama Rais.

Unaombwa sana kuunganisha wadau wa kisiasa na kijamii kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025, unaombwa kuchukua hatua za kimkakati zinazolenga kukuza maridhiano, uwazi, na ushirikiano kwa sababu kama tutaenda kwenye uchaguzi mkuu tukiwa tumagawanyika kama Nchi . hali ya kisiasa Tanzania inaweza kuwa ya wasi wasi sana, ingawa umepiga hatua tangu uchukue madaraka kama Rais wetu lakini bado Tanzania inakabiliwa na changamoto za ukosefu wa imani kati ya vyama vya siasa, wadau wa haki za binadamu, Demokrasia na hitaji la muda mrefu la mifumo huru ya uchaguzi na Katiba inayosanifu mazingira ya demokrasia ya vyama vingi.

Wadau unaombwa kushirikiana nao kwa niaba ya Mama Tanzania ni pamoja na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Baraza la Wakristo Tanzania (CCT), Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), vyama vya siasa, Taasisi za Vijana, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na mashirika ya haki za binadamu, hawa ni wadau muhimu sana kuahakikisha Tanzania yenye mshikamano na utangamano tunapoelekea uchaguzi mkuu. Yawezekana serikali ina ushirika na wadau hawa lakini kipindi hiki Mama Rais iwe zaidi na kwa dhati kabisa kwa sababu migogoro mingi ya kisiasa ina hatua zake za kuanza na kuenea katika hatua hizo sisi tupo hatua ya TENSION wewe ni mwanadiplomasia namba moja unanielewa ninaposema TENSION katika hatua kama hii ya mtanziko lazima kiongozi Mkuu wa Nchi aombwe kuchukue hatua mapema.

Mazungumzo
Rais Samia, nakuomba kufanya mazungumzo tena usichoke kufanya hivyo maana wewe ndiye unaye beba taswira ya Tanzania muda huu mazungumzo haya yahusishe wadau wote waliyotajwa
Kwa mfano, Tusogeze mbele uchaguzi mkuu kwa kipindi cha miaka miwili au vinginevyo ili tukubaliane kufanya Mageuzi ya dhati ya kikatiba na kisheria, Bunge la Jamhuri ya Muungano lirefushe madaraka yako na Bunge lenyewe ili kupisha Mageuzi hayo kwa sababu kisingizio cha serikali yako ni kwamba muda hautoshi, muda unatosha na kama hautoshi basi tusogeze mbele uchaguzi mkuu kwa namna bora ili Mama Tanzania abaki salama.

Wadau kama TEC, CCT, BAKWATA, TLS, Shura ya Maimamu na wengine wapewe jukumu la kusimamia na kuratibu baadhi ya vipindi vya mazungumzo ili kuhakikisha upande wowote hautawaliwi na siasa za chama ili kuilinda Tanzania kisiasa na kiuchumi.
Mama Rais, unajua kabisa mgogoro wa kisiasa utasababisha mdororo wa kiuchumi, hii itasaidia kujenga imani kwa Taasisi hizi za dini zinazochukuliwa kuwa na upande ili kuhakikisha maoni ya pande zote yanazingatiwa ikiwa na Taasisi za Vijana na vyama vya siasa.

Taasisi za vijana ziwe na nafasi kubwa katika majadiliano kwani Vijana wengi wanakabiliwa na changamoto lukuki za kiuchumi, kijamii na ajira ambazo zinaweza kuathiri uchaguzi mkuu au kwa namna nyingine kwenye madaraka yako, najua unataka kuendelea kuwa Rais wetu.

Taasisi za dini zina nafasi kubwa katika jamii ya Tanzania kwa sababu zinawakilisha idadi kubwa ya watu na zinathaminiwa kwa maadili yao, Mama Rais utoe wito kwa TEC, CCT, BAKWATA, TLS, vyama vya siasa na wadau wa maendeleo kuandaa mikutano ya pamoja ya amani na umoja kabla ya uchaguzi mkuu ikilenga kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa uchaguzi wa amani, haki na wazi
BAKWATA, CCT, TLS na Shura ya Maimamu washiriki kwenye uhamasishaji wa uchaguzi wa amani huku haki ikionekana imetendeka ili kukuza imani na ushiriki wa wote kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Vyama vya siasa hasa vya upinzani kama CHADEMA, ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi, CUF na vingine vimeonesha wasi wasi kuhusu mifumo ya uchaguzi na haki za kisiasa. Ili kuleta mshikamano wa Kitaifa, Rais Samia, unaombwa kuimarisha juhudi za maridhiano, ili twende sote kama Taifa

MAMA, endelea na mikutano ya viongozi wa vyama vya siasa kama ule wa Januari 2023 na uwe na ajenda za wazi kama Mageuzi ya dhati ya sheria za uchaguzi na uhuru wa Tume ya uchaguzi, kumbuka nimeomba kusogezwa mbele kwa uchaguzi hivyo mambo haya yanaweza kufanyika kwa utulivu, maarifa na upendo wa dhati kwa Mama Tanzania bila papara ili Taifa libakie salama na tufanye maendeleo na hasa Mapinduzi ya haraka ya kiuchumi.

Mama Rais, ondoa mashtaka ya kisiasa dhidi ya wanasiasa wa upinzani ambayo hayana msingi wa kisheria kama tunavyoona kwa Tundu Lissu ili kujenga imani ya umma na matendo ya kuteka watu, kutesa na kuua yakome kwa sababu yanapanda mbegu ya visasi, damu yoyote inanena kwa ubaya au uzuri epusha utawala wako na mateso ya watoto wa Tanzania na damu zao kumwagika juu ya Ardhi ya Tanzania, kemea vitendo hivi wazi wazi Mama Rais, kama siyo wazi wazi basi waonye kimya kimya kwa sababu siyo kwamba hawajulikani wanajulikana na mara nyingine wanafanya mambo ili kukufurahisha wewe binafsi lakini wanalitia Taifa kwenye taswira mbaya ambayo wewe binafsi unachafuka sana kwenye uso wa Watanzania wenzako na Dunia, waonye waache kabisa.
Jeshi la polisi ni kama chombo cha kuumiza na kutesa watoto wa Mama Tanzania, linaonekana Jeshi katili kwa sababu ya matendo yao ya kupiga watu hovyo hovyo na kunyanyasa watu hii ni mbaya sana Mheshimiwa Rais, kama uliweza kuondoa marufuku ya mikutano ya kisiasa siyo jambo la kusifiwa ila ni haki ya kikatiba, mengine yanawezekana pia, akikisha vyama vya upinzani vina nafasi sawa ya kufanya siasa na mikutano ya hadhara bila vizuizi kama ulivyofanya kwa kuondoa marufuku ya mikutano hiyo mwaka 2023.

Mfano: Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba na Joseph Butiku, walikushauri kuwaita CCM na CHADEMA na ukafanya hivyo kuwa msingi wa kujadili tofauti za kisiasa, Mheshimiwa Rais, hatuwezi kuendelea kujadili siasa kila siku wakati tuna uchumi unaokua kwa style ya utapiamlo kwa pamoja lazima kuna muda tuondoke kwenye siasa na uchaguzi ili kujadili masuala mtambuka ya kiuchumi, Nchi yetu bado maskini sana Mheshimiwa Rais tunaitaji kujikomboa kiuchumi.

Vijana ni nguvu kubwa na injini ya Mapinduzi ya kiuchumi na siasa za Tanzania lakini wengi wao wanakosa ajira na fursa za kiuchumi jambo linaloweza kuathiri maamuzi yao katika masuala ya kisiasa na kiuchumi ni muhimu vijana kuwa sehemu ya mazungumzo ili agenda zetu zipewe kipaumbele cha dhati na kujadili changamoto zetu na kuziweka katika ajenda ya uchaguzi wa amani, haki na wazi.

Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS na mashirika ya haki za binadamu Nchini wana jukumu la kuhakikisha uchaguzi unafuata viwango vya haki, huru na uwazi, Rais Samia unaombwa kushirikiana na TLS kuunda timu ya wataalamu wa kisheria itakayofuatilia mchakato wa uchaguzi, ikiwa na wawakilishi kutoka mashirika ya haki za binadamu ili kuhakikisha sheria zinazingatiwa, ondoa vizuizi vya kisheria dhidi ya wanaharakati na waandishi wa habari kama ilivyoripotiwa na Human Rights Watch, ili kuimarisha uhuru wa kujieleza na kuripoti uchaguzi bila upendeleo wa vyama, kuna tafiti kedekede zimeonesha namna vyombo vya Habari vinavyo pendelea kipindi cha uchaguzi kwa sababu ya kibano cha serikali.
Unda mfumo wa kuripoti ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi unaosimamiwa na TLS na mashirika ya haki za binadamu ili kuwapa wananchi imani ya mfumo wa uchaguzi huru na haki.

Mfano: Ripoti ya Jaji Mohamed Chande Othman ya mwaka 2023 kuhusu haki za jinai inaweza kutumika kama msingi wa marekebisho ya sheria za uchaguzi

Kuimarisha Tume huru ya Uchaguzi, Wadau wengi ikiwa ni pamoja na CHADEMA, ACT-Wazalendo, TEC, Shura ya Maimamu, mashirika ya haki za binadamu, wanaharakati na viongozi wastaafu wameelezea wasi wasi kuhusu uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mheshimiwa Rais, teua wajumbe wa Tume wanaokubalika na wadau wote, wakiwa na sifa za maadili na weledi kama ilivyopendekezwa na Tike Mwambipile wa TAWLA na wadau wengine wa uchaguzi na demokrasia hakikisha Tume ina bajeti ya kutosha na uhuru wa kiutendaji kama ilivyoelezwa na wasomi Nic Cheeseman na Jorgen Elklit, unda chombo cha usimamizi cha uchaguzi kinachohusisha TLS, mashirika ya haki za binadamu na taasisi za dini ili kufuatilia maandalizi ya uchaguzi.

Mfano: Mazungumzo ya wadau kuhusu sheria za uchaguzi za 2024 yanaweza kuimarishwa ili kushughulikia masuala ya Tume huru.

Kukuza umoja wa kitaifa kupitia ujumbe wa pamoja
Mama Rais, umekuwa ukisisitiza umuhimu wa umoja na maridhiano katika hotuba zako Ili kufanikisha hili unaombwa kuimarisha ujumbe huu kwa vitendo, unaombwa kutoa ujumbe wa wazi kwa Watanzania ukielezea maono yako ya uchaguzi wa amani, haki na wazi na jinsi wadau wote watakavyoshirikishwa katika mchakato wa uchaguzi huru na haki, weka wazi hatua za serikali yako za kushughulikia changamoto za kiuchumi kama gharama za maisha ambazo zinaweza kuathiri umoja wa kitaifa kama alivyopendekeza Dk. Richard Mbunda.

Mfano: Hotuba yako ya Aprili 2025 ilisisitiza umoja na demokrasia inavyoweza kuimarishwa na vitendo vya wazi vya kushirikisha wadau

Kushughulikia wasi wasi wa kisiasa ndani ya CCM, ndani ya CCM kuna wasi wasi kuhusu mabadiliko hasa mikutano ya hadhara na uhuru wa siasa, unaweza kuona makada wa CCM wako macho sana mara baada ya mikutano hiyo kuruhusiwa, hii inaletwa na hofu ya kuanguka kwa chama hicho lakini ukiangalia kwa utamaduni wetu kisiasa na kiuchumi jambo hili ni la hofu tu
Mama Rais, fanya mikutano ya ndani na viongozi wa CCM ili kuelezea faida za demokrasia ya ushindani na jinsi inavyoimarisha chama chenu na uchaguzi wetu, kwa sababu upinzani dhaifu ni njia ya CCM zaifu mara dufu, weka wazi kuwa hatua zako za maridhiano haziathiri nafasi ya CCM katika uchaguzi bali zinalenga kuimarisha demokrasia ya vyama vingi.

Mwisho kwa sasa
Kumbuka nimetangulia kusema tusogeze mbele uchaguzi mkuu ili kufanyika kwa haya yote kwa utulivu ili tushinde wote kama Taifa, tusikubali kugawanyika kabisa tujiepushe na hili kwa nguvu zote.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, una fursa ya kuimarisha umoja wa kitaifa kabla ya uchaguzi wa 2025 kwa kushirikisha wadau mbalimbali kama TEC, CCT, BAKWATA, Shura ya Maimamu, vyama vya siasa, taasisi za vijana, TLS, na mashirika ya haki za binadamu kuhakikisha Tume huru ya uchaguzi, kuondoa vizuizi vya kisiasa, na kukuza tafakuri ya pamoja.

Na, Nicolas Jovin Clinton Gabone.
Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Vijana wa Mageuzi (JUVIMA)- NCCR-Mageuzi
Dar Es Salaam
4 May 2025
 
Too late!
 
Unampigia Mbuzi gitaa, mtu anajiita chura kiziwi akifikiria kutosikikiza wananchi ndiyo inamfanya kuwa kuongozi bora.
Kwa akili ya kawaida, hivi unadhani wanaoteka watu na kuwaumiza hawafahamiki na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama?

Yaani gari ilifanya blockage ya basi mchana na kumteka Mzee Ally Kibao then anasema drama..
Mengine ni kichefuchefu kuyazungumza kama vile hatuna kiongozi wa nchi.
 
Samia ameshindwa kuongoza Taifa letu na aondoke haraka madarakani yeye na chama chake.
 
Back
Top Bottom