Rais Dkt. Mwinyi ashiriki Doha Forum 2023

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameshiriki ufunguzi wa Jukwaa la 21 la Doha (Doha Forum) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Hoteli ya Sheraton Doha, Qatar tarehe: 10 Desemba, 2023.

Baada ya ufunguzi wa Jukwaa hilo iliwasilishwa mada ya kikao cha kwanza isemayo ikimaanisha nini kifanyike kutanzua Mzozo wa Mashariki ya Kati baina ya Israel na Palestina iliyowashirikisha wasemaji akiwemo Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Mhe. Sheikh Mohammed Bin Abdulrahman Bin Jassim Al Thani, Rais wa Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis, Waziri Mkuu wa Palestina Mhe. Mohammad Shtayyeh pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mhe. Jordan Ayman Al Safadi.

Pia Viongozi mbalimbali na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wamehudhuria Jukwaa hilo kama wasemaji na washiriki akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres.

IMG-20231210-WA0035.jpg
IMG-20231210-WA0033.jpg
IMG-20231210-WA0040.jpg
IMG-20231210-WA0038.jpg
IMG-20231210-WA0034.jpg
IMG-20231210-WA0037.jpg
IMG-20231210-WA0036.jpg
 

Attachments

  • IMG-20231210-WA0038.jpg
    IMG-20231210-WA0038.jpg
    30.2 KB · Views: 3

Similar Discussions

Back
Top Bottom