Rais Dkt. Magufuli, ingilia kati suala la ving'amuzi kwani Wananchi wako tunateseka huku TCRA na Wizara wanafurahia tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,550
108,882
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzia na Usalama nchini Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo nakuletea Kilio changu Kikubwa Kwako na ambacho naamini pia ni cha Watanzania wengi ambacho TCRA ndiyo wanatusababishia haya maumivu bila kuchukua hatua zozote stahiki.

Mheshimiwa Rais mwaka jana kulitokea matangazo mara mbili kwamba Ving'amuzi vyote vinatakiwa kutowalipisha Watanzania zile Local Channels ambazo ni ITV, Channel Ten, Clouds tv, East Africa tv na Star tv bila kuisahau na TBC1 lakini Mheshimiwa Rais Sisi Wananchi wako tunasikitika sana kwamba hadi hivi Mimi GENTAMYCINE naandika huu uzi bado Sisi Wananchi wako tunaendelea Kulipishwa kila mwezi Shilingi Elfu Sita ( 6,000/= ) kama Tozo ya mwezi ili tuweze kuona hizo local channels tajwa hapo juu.

Mheshimiwa Rais ni mwezi uliopita tu December 2017 kuna Tangazo la TCRA lilikuwa likizunguka mitandaoni na nadhani hata wafuatiliaji wengi wa haya masuala ya Mitandao waliliona ambapo TCRA ilikuwa ikiwataka Wamiliki wote wa Makampuni ya Ving'amuzi nchini Tanzania kuanzia tarehe 1 January mwaka huu wa 2018 waache kuwatoza Wananchi Pesa ili waweze kuona hizo Local Channels tajwa hapo juu ila kwa masikitiko makubwa Mheshimiwa Rais hadi hivi leo hali ni ile ile na hakuna lolote lililotendeka na bado Sisi Wananchi wako tunaendelea tu Kunyanyaswa na TCRA kwa haki yetu tunayoistahili.

Mheshimiwa Rais haiingii akilini leo hii Sisi Wananchi wako unaotutetea kila uchao tunalazimishwa na hayo Makampuni ya Ving'amuzi kulipia hata Channel ambayo bado ipo katika majaribio ya TVE na nyinginezo ambazo hazina umuhimu wowote Kwetu. Na kinachotuuma zaidi Mheshimiwa Rais ni kwamba hata Waziri husika pamoja na Naibu wake wamenyamaza tu hali ambayo inazidi kutuumiza Sisi Wananchi wako wa hali ya chini.

Na hapa nisifiche wala kuzunguka Mheshimiwa Rais Kampuni ninayoiongelea na kuipigia makelele kwa huu Uonevu kama siyo Unyanyasaji ni hii ya StarTimes japo najua yawezekana kuna Watu wengine labda na Wao wana lawama zao kwa Ving'amuzi wanavyovitumia ila tunaomba sana msaada wako Mheshimiwa Rais katika hili na ikiwezekana utoe rasmi AMRI yako ya Kiutalawa kama siyo Kiuongozi ili hizo Local Channels zote Tano tuwe tunaziangalia bure kama ambavyo ilikubaliwa awali lakini pia uwawajibishe vilivyo Viongozi wa TCRA na wale wa Wizarani kwani wametusababishia mno usumbufu na mateso Sisi wapiga Kura wako.

Naomba kwa yoyote yule ambaye ana mawasiliano ya karibu na Msemaji wa Ikulu Gerson Msigwa anisaidie Kumfowadia haraka huu uzi wangu ili na Yeye asubuhi hii hii amfikishie Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kusudi ajue TCRA na Wizara husika wanavyotutesa kutokana na hili suala zima la Local Channels kuonyeshwa bure pasipo malipo. Inauma mno na inakera sana na mpaka unaona GENTAMYCINE nimeandika hivi jua nimechoka na nimekereka Kunakotukuka.

Nawasilisha.
 
kuna taasisi kazi zake ni kutoa matamko kisha kushindwa kuyatekeleza.
Kama hiyo sheria ya channel tano za bure mmeshindwa kuisimamia ni bora mkawaambia hao watanzania mnaowaita wanyonge kuwa hakuna channel za bure......
 
GENTAMYCINE CCM ni ileile, ila mkulu namkubali kwa kukurupuka na ulivyomsifia kesho utasikia akiongea kama alivyoongea kuhusu michango mashuleni lakini wapi wananchi wanakamuliwa vyakutosha
 
Ni zaidi ya mwezi sasa tangu TCRA wate tamko kuwa vingamuzi vyote lazma vionyeshe local TV zote free, lakini hakuna kinachofanyika na wenye vingamuzi wamegoma kutekeleza agizo hilo, je ndo tuseme uongozi wa TCRA umeshindwa kusimamia hili?

Ni TV moja tu local inayoonyenshwa free nayo ni TBC maanake nini, au kwa kuwa ya CCM?

Magufuli wamulike TCRA
 
haya malalamiko uliyotoa hapa umeshtaki TCRA lakini? maana wao wanajua everything is OK hawapati hayo malalamiko unayoyasema. Nina uhakika 100% endapo watanzania tukiacha kulalamika kwa customer care wa ving'amuzi then tukapeleka malalamiko yetu kwa wahusika (TCRA)/ watoa leseni Face to Face watafanyia kazi kwa haraka sana.
 
Samahani, hivi gharama za kupiga simu zimeshuka kama tulivyojulishwa? Maana miye nimezoea "kudip" na kutuma tafadhali nipigie tu. Mara ya mwisho nilikopa Tsh. 450, tar 10/11/2017.
 
Nchi hii ina mazingaombwe kibao, suala hili kila uchao tunalipigia kelele cha ajabu serikali na hawa TCRA wote wameziba macho na masikio! Eti ni serikali inayojali wanyonge!
 
Nchi hii ina mazingaombwe kibao, suala hili kila uchao tunalipigia kelele cha ajabu serikali na hawa TCRA wote wameziba macho na masikio! Eti ni serikali inayojali wanyonge!
Hawa TCRA watakuwa wanavuta mpunga huko kwa vingamuzi, haiwezekani wanatoa maagizo hawayafuatilii
 
Back
Top Bottom