gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 824
- 1,516
Ni baada ya kuangalia taarifa ya habari ya TBC iliyo muonyesha mlemavu huyo akitumia baiskeli ya kawaida na kuhatarisha maisha yake.
mheshimiwa raisi ameahidi kumsaidia mlemavu huyo bajaji ndani ya wiki moja kutoka katika msahara wake
======
Katika hali isiyokuwa ya kawaida THOMAS KONE mlemavu wa miguu amekuwa akitumia usafiri wa baiskeli ya matairi mawili katika shughuli zake za kujitafutia maisha.
Mwandishi wa TBC MBOZI KATALA amekutana na THOMAS KONE katika hekaheka zake za kutafuta maisha na kuwataka watu wenye ulemavu kufanya kazi zitakazo waingizia kipato badala ya kukaa mitaani na kusubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema.

Nikiwa sebuleni leo hii nikitizama taarifa ya habari TBC1 iliwekwa habari ya kijana Anthony ambaye ni mlemavu wa miguu lakini anafanya shughuli zake kama kawaida na kikubwa anatumia baiskeli ya matairi mawili. Yaweza kuwa kama ndoto lakini anafanya hvyo ili kujitafutia riziki kwani ana familia ya mke na watoto wawili.
Alipohojiwa alisema kwamba kwa miaka nane sasa amekuwa akijituma kutafuta riziki bila kuchoka wala kukatishwa tamaa kwa sababu ya ulemavu wake. Pia aliomba msaada wa kupata BAJAJ toka kwa Rais Magufuli kwani hachukulii ulemavu wake kama kikwazo bali fursa.
Baada ya muda kidogo ukasomwa ujumbe na mtangazaji Gabriel Zakaria na kusema kwamba Rais Magufuli ameridhia ombi hilo na ndani ya wiki moja atapatiwa BAJAJ hiyo na itatokana na mshahara wake.
Kwa maoni yangu, Tanzania tumepata RAIS ambaye anatambua shida za wananchi, anakuwa mstari wa mbele katika kusaidia wanyonge (alimsaidia pia kwa kutoa mil.5 binti kipepeo benedicta wa chuo kikuu mzumbe) lakini yote hii ni kupitia vyombo vya habari. Pongezi Mh. Rais kwa kuonesha kuwa ukarimu wako na roho yako nzuri ni kwa ajili ya kila mtanzania hasa asiyejiweza lakini anajituma katika kufanya kazi.
Rai yangu, vyombo vya habari vikitumika ipasavyo, vitaleta tija kwa taifa na kudumisha umoja wetu bila kutengeneza matabaka.
[emoji767]Soli ya Kiatu