Rais apingwa tena: Msajili wa HAZINA asema si kosa shirika kufungua fixed account

Kwani kuna mtu alisema ni kosa? Rais alisema zikae kule BOT ili mabenki waende wazikope kule kwa interest
 
hawa wataalam wanathibisha kwamba hawaombwi ushauri au hawasikilizwi?alianza benno ndulu
Hawaombwi mkuu. Huku Serikalini tunatoa ushauri kwa MADOKEZO ama kupitia MINUTES za vikao. Jamaa yako hana muda na madokezo
 
Kuna waziri alikurupuka na kusema wanamshauri mkulu na anaekeleza ushauri
 
sasa wataalam wa uchumi ndani kabisa ya serikali wameamua kuwapiga ngumi za chembe,vumilieni,alianza beno ndulu
Ukweli kuweka hela FD si kitu kibaya,kwani katika hali ya kawaida mwekaji anapata faida mara tatu,yaani hela zake kuwa salama,kuweza kuzitumia kama dhamana ya mkopo kwa kutumia FD yake,na pia kupanua wigo wa mapato yake.Tatizo ni hilo la utaratibu na uwajibikaji hasa kama fedha siyo yako.Wengi shauku yetu ni kujua kama riba iliyopatikana baada ya FD kuiva ilitolewa Taarifa katika hesabu za mwenye mali na kama ilitolewa basi kutakuwepo utaratibu wa jinsi ilivyotumika.Tatizo lingine ,ni pale ambapo hizo fedha zilitolewa kwa kazi maalum lakini hiyo kazi haikufanyika au imecheleweshwa kwa muda kadhaa ili fedha zizae(FD interest),hapa ndo mwenye fedha yake anapata ukakasi.na la mwisho ambalo sitaki kuliamini kwamba ,"aliyeongea na mtu wa masoko wa Benki husika aliahidiwa au alipewa chchochote" maana ili upate fedha lazima upoteze fedha".Tuamini kwamba fedha iliwekwa FD kwa nia nzuri mpaka hapo uchunguzi ukikamilika.Ukweli kwa watu wenye maamuzi na fedha yao hii moja ya njia nzuri ya kujiimarisha kiukwasi na pengine kujenga mahusiano mazuri na Benki yako.
 
Duh! Yaani mahojiano yoote yale umeamua kuyaripoti hivo, mbona jamaa ameelezea vzr sana kuhusu hiyo mada
 
Back
Top Bottom