Rais anapodanganya Umma na kulialia eti Umasikini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais anapodanganya Umma na kulialia eti Umasikini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Jan 29, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Rais Kikwete akiwa safarini kwenda Davos, alisimama LIbya na kukutana na Ghaddafi na kumpa shukrani kwa msaada uliotolewa na Libya kujenga nyumba kwa familia zilizoathirika kwa mafuriko.

  Katika hotuba yake, Rais Kikwete alisema yafuatayo ambayo nayanukuu na kuyajengea hoja ya yeye kuudanganya umma!

  Nanukuu gazeti

  Rais anadai Taifa letu ni masikini sana na dola milioni 15 ni nyingi sana!

  Kweli dola Milioni 15 ni nyingi hasa zikitumika kwa matumizi yasiyo ya msingi au kipaumbele mbayo ni jambo la kawaida sana kwa Serikali ya Tanzania kutumia fedha kwa mambo yasiyo ya msingi au kipaumbele kwa Taifa zima.

  Hata kama fedha hizi zingekuwa ni za mtu, shirika au Taasisi binafsi, inapofikia kuwa fedha zinatumika kwa minajili ya kuwa zipo zitumike, swali linakuja, iweje kama Taifa tuendelee kudai sisi ni masikini?

  Kwa nini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaendeleza ulaghai, udanganyifu na kutukuza umasikini na unyonge kwa kudai eti nchi ni masikini hatuwezi kuwa na Dola milioni 15 na kuzitumia kwa vitu vya muhimu?

  Labda nitumie Jedwali hili kuonyesha ni vipi kauli ya Rais ni ya kizandiki na kinafiki!

  1. Benki Kuu imejenga na kukarabati nyumba nne kwa ajili ya Gavana na manaibu wake. Jumla ya gharama zote ni karibu Shilingi Billioni 6 ambazo ni sawa na Dola Millioni 5 ambayo ni asilimia 30 ya Dola Milioni 15.

  2. Nyumba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, shirika la umma linalokabiliwa na matatizo ya kifedha kuipatia Tanzania umeme wa kutosha, imegharimu si chini ya Shilingi Bilioni 1.5 ambazo ni sawa na Dola Milioni 1 na ni asilimia 7 ya Dola Milioni 15 zinazohitajika kujenga hii barabara iliyoharibiwa na mafuriko.

  3. Chama Cha Mapinduzi, kimetumia takribani kati ya Shilingi Billioni 9 na Bilioni 14 kununua magari 200 kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Taifa wa mwaka huu 2010. Magari haya kutoka Japani ambayo nayapa makadirio kutokana na bei za International Motor Mart au Toyota Motors of Tanzania ambazo kwa magari ya Toyota kati ya Rav4 na Land Cruiser VX yana bei ya chini bila kodi na ushuru kati ya Dola 35000 na Dola 55000. Hivyo iwe kwa kadirio la chini la Shilingi Bilioni 9 ambayo ni sawa na Dola Milioni 7 ambayo ni asilimia 47 ya dola milioni 15.

  Kwa mifano hiyo mitatu ya matumizi ya Taasisi na Mashirika yanayohusiana na Serikali ya Tanzania, ni dhati kuwa Tanzania ina uwezo wa kujitegemea na hizo dola milioni 15 si nyingi sana kiasi cha kutangazia umma na dunia kuwa eti sisi ni masikini! Ukichukua matumizo yote ya hizi taasisi tatu tuu, unakuta kuwa tayari Tanzania dola Milioni 13 ambazo ni asilimia 86 ya dola Milioni 15 zinazohitajika kujenga upya barabara na reli huko Morogoro!

  Jana katika hotuba yake kwa Bunge la Marekani, Rais Barack Obama aligusia suala la matumizi ya lazima na umuhimu wa Serikali ya Marekani kufunga mkanda na kuachana matumizi yasiyo ya busara na ya holela.

  Je Rais Kikwete baada ya miaka yako minne ya kuwa madarakani:

  a. umefanya nini kupunguza deni la Taifa?
  b. umeanya nini kupunguza matumizi ya Serikali?
  c. umefanya nini kuondokana na umasikini?

  Nasubiri majibu kutoka kwa Rais mwenyewe au Wapambe wake!
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  You nailed it mkuu, inatia hasira mpaka basi. Suppose we put an educated guess on how much is spent for him and his delegates to do this globe troting............... Unaweza kukuta hiyo $15mn is just for 3 trips!!!!!!
   
 3. Z

  ZuberiKing New Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu,rent ya nyumba ya gavana ili USD7800 kwa mwezi,ambayo kwa mwaka ni USD93,600.Sijui kama huyu Rahisi wetu anajua kuwa hata nchi Tajiri haziwezi kufanya upuuzi kama huu.
   
 4. A

  AmaniKatoshi Senior Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Rev Kishoka , na wachangiaji wengine wenye mapenzi mema kwa nchi uyetu ya Tanzania. Ninakupongezeni san kwa brief analysis inayoonyesha jisni Raisi wetu anadanganya na haoni aibu kulia lila......kwa mifano michache tuu uliyoorodhesha, mtu mwenye akili ataelewa huo UMASKINI ambao Raisi Kkwete anupigia filimbi ni upi? Ningemuelewa kama angesema, UMASKINI TANZANIA UNATOKANA NA CHAMA TAWALA KUWA NA UONGOZI ulioigawa nchi sio katika misingi ya ukabiola tena kama ilivyodhaniwa, bali MASKINI na MATAJIRI mostly MAFISADI. Na hawa MATAJIRI wanatumia kodi ya mwalimu kwa mfano KUJINENEPESHA na sio kwa lengo la kuwakamua wananchi kutoka katika umaskini. Mimi ninasema hata MKUKUTA ni propaganda! JK anapowaambia wananchi kuwa kukarabato sehesmu zilizo za maafa ni hela nyingo, lakini yeye anakuwa na convoy kuzunguka dunia...how much they spend each day on his trips? Ni wakina mama wangapi wanakufa Mawezi hospital kila siku just kwa kukosa vitu vidogho na vya garama ndogo sana ambayo serekali ingeweza walao kuhakikisha vipo? Morogoro hospital ni mfano, mama mjamzito anatakiwa kwenda kujifungua atakuwa anabeba ndoo (kwa ajili ya kujisaidia) nguo nyembe etc, hadi lini, wakati huo huo mkubwa anaetakiwa kushughulikia tatizo hilo anapimwa afya Marekani, france Uswis etc? Hizi dola za safari hizo kwa mwaka ni about 200% ya dola 15 million kwa ajili ya kukabiliana na maafa.

  Lingine ni kuwa, watanzania tataendelea kudanganywa hadi lini? Serekali badala ya kuangalia matatizo ya wananchi, inaweka nguvu kuhakikisha inashinda uchaguzi unaofuata ata kama ni 5 years later.....maendeleo yatatoka wapi?

  Ndugu zangu tuamke. Mwaka 2005 marafiki zangu walipokuwa wanamsherekea JK kupitishwa kugombea uraisi,,,,,nilipatwa na homa ya gafla kwa sasabu za kuhofia kuwa "hawakuwa maejua nini kiko mbele yao" ie UMASKINI" . Leo hii nikiwauliza what they were selebrating, hakuna hata mmoja anadiriki kuniangalia usoni........ tunakokwenda ni wapi?

  UMASKINI TANNZANIA ni wa kujitakia, haswa kwa kiwango kikubwa ikiwa ni sera isiyoonkekana ya serekali. Watu wakiendelea kuwa maskini, ukiwapa kanga during election basi watakuchagua maana watona wewe ni mfalme. Burundi, Rwanda na QAngola ambazo zimekuwa na vita siku nyingi..leo ziko wapi .....tanzania is far behind.

  Asante sana Rev Kishoka!
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wanafikiri sisi sote ni wajinga....!
   
 6. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mchungaji,

  sijawahi kuona Mkuu wa nchi kama rais wetu;huwa najisikia vibaya sana nikimsikiliza akionglea mambo muhimu ya taifa letu.utakumbuka wakati wa mktikisiko wa uchumi wa dunia aliwahi kusema maneno haya baada ya kuulizwa nchii itaathirika vp na janga hili; "hili haliwezi kutukumbuka sisi,ni kwa ajili ya mataifa makubwa na mabenki yao,sisi tuna benki ndogo ndogo hivyo hilo si letu".

  Nilishangaa sana na kauli hiyo,yaani yeye alijua kuwa tatizo na Economic recesion ni kwa ajili ya mabenki tu?sasa sijui tatizo ni uwelewa wake mdogo au wa wasaidizi wake?

  Mie mpaka sasa sijaelewa ila kwa kuwa alisema huwa hawasikilizi wasaidizi wake nina wasiwasi sana na uwezo wake wa kung'amua mambo.Haiwezekani kuongea bilion 15 ni nyingi kwsa nchi kama hii ambayo ina motorcade za BMW na posho nyingi..pesa zipo na azitumie vizuri,zilitoka wapi za RDC?huku ni kututia aibu tu
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Gembe.. siku chache zilizopita alipokuwa akizungumza na mabalozi kwenye sherry party alizungumzia gharama ya ujenzi wa hiyo miundo mbinu... alisema ni bilioni 10! juzi Engineer Chambo akasema sijui bilioni 13.. leo wamefikia bilioni 17, by the end of next week itakuwa bilioni 20.

  I got a pendekezo.. why not go to bilioni 50 yaishe. It looks we have a thing for 50!!
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Na ya Speaker Sitta kule Dodoma ni dola elfu nane kwa mwezi. Tunahitaji jasiri mmoja wa kufanya mabadiliko ya uongozi wa Nchi yetu kwa amani.
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu wetu wa nchi, anasikitisha sana. Kwa kweli nakumbuka jinsi alivjojibu kuhusu economic recession, ni aibu tupu!!

  Mi nahisi inawezekana ni mbishi, hawasikilizi washauri wake au washauri hawamuandai vizuri. Kuna tatizo sehemu!!
   
 10. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ina maana hata wataalamu wa kujumlisha hasara iliyotokea katika hiyoo miundombinu bado ni TATIZOOO??

  Hakuna cordination mpaka kwenye assesment inavyoonekana wizara wana yao na IKULU wana yao.!!! capacity limitation in thinking!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Tatizo la Muungwana hajui nini kinaendelea;tabia yake ya kupenda sifa ndiyo tatizo na najua mwanzoni inawezekana alimpigia chambo coz ni swahiba wake na kumuuliza "hivi ni shilingi ngapi itatosha kurekebisha barabara zilizoharibu?",chambo akamwambi kama bilioni 10 hivi.Navyomfahamu jamaa lazima akaidandia hiyo bilioni kumi na kuwaambia wafadhili.

  Baadaye TANROADS walipohakiki na kufana tathmini ikafikia bilion 13 na hii ni wiki iliyopita kwenye cabinet sasa leo huko Libra anasema bilion 15;hivi kweli tuna shida ya pesa ndogo ndogo kama hizi?na bado mkulu na Shein wanasafiri safiri kwenda nje?inaingia akilini?

  Kila siku anang'ang'amia kukutana na Marais wa marekani Je anajifunza nini kutoka kwao?au ndiyo kupiga picha tu na kusema kuwa mie ni rais wa kwanza kuonana na Obama?inaongeza nini kwa wananchi?Obama majuzi alisema kuna haja ya viongozi kuwatumikia wananchi zaidi ya kujihudumia nafsi zao.

  Miaka minne amenekana ameshindwa ila anatakiwa ajipange na kuangalia njia ya nzuri za kubadilisha uchumi wa nchi hii;Rejea mwelekeo wa sera ya chama cha mapinduzi kwa miaka kumi ambao lengo lilikuwa ni kujenga taifa leny uchumi unajitegemea ;kuondoa utegemezi wa wafadhili katika shughuli za kimaendeleo ,mkapa aliweza kuanzisha mfumo huu kwa kujenga mfumo mzuri wa ukusanyaji mapato.

  kuanzia mwaka 2005 kumekuwa na kusuasua kwa mafanikio wa kiuchumi na kushuka kwa hazina ya pesa za kigeni na hili linachangiwa na wizara ya fedha na uchumi kuongozwa na mawaziri wasio na uwezo;mawaziri wanaopenda safari za nje kila siku bila kufanya kazi za kujenga na kusimamia uchumi(October -Dec TRA hawakufkia lengo laukusanyaji mapato)

  Kama unakuwa na kiongozi mkuu(Muungwana) ambaye anaenda nje kuombamsaada wa kifedha;kuna haja gani ya kila waziri naye kusafiri kwenda nje?kufanya nini?kwanini serikali isiwe inapelekea wataalamu vijana(watendaji) nje ili wakajifunze na kuja kufanya kazi kwa ufanisi?ila kila siku utasikia mawaziri wako canada..wtf?Hata Memeb hana haja ya kusafiri coz kuna mabalozi kule.nchi haina maendeleo yoyote kwanini tunakuwa na gharama kubwa za kupeleka mawaziri safari za nje?ulimbukeni?

  Taifa lilipo hivi sasa,mpaka tunaanza kulilia bilioni 15 ni wakati sasa ambapo linahitaji kiongozi ambaye atakuwa anajua taifa linaendaje?priority zetu ni zipi?tunakiwa tufanye jambo gani ili kufanikisha mipango yetu?pesa zitatoka wapi?usimamizi ukoje?.

  Kimsingi tunahitaji kubadilika sana;tena sana!Mzee mwanakijiji naomba umtumie Muungwana hotuba ya state of union ya juzi ili asome na aone jinsi wengine wanavyojua kueleza mambo .

  Na kwa kuwa atakaye mpinga Jk atakufa basi ajifunze na tunahitaji mabadiliko na haya ni mawazo yangu kwake na wapambe wake.

  Gembe
   
 12. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Tena kumbuka mheshimiwa ni mchumi!
   
 13. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu Bullet ;

  Ndiyo kasomea uchumi ila siyo mtaalam wa mambo ya uchumi!
   
 14. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Tatizo la viongozi wa nchi yetu ni kukosa priorities, ni mara nyingi sana tumeshuhudia mambo yasiyo na tija kwa taifa hili ndiyo yanayotiliwa mkazo sana na serikali yetu na ndiyo hayo yanayotugharimu mabilioni ya pesa, ni ulimbukeni, roho za ulafi na ubinafsi wa viongozi wetu unaowafanya wasahau kabisa dhamana tuliyowapa ya kutusaidia kuongoza taifa hili.

  Nakumbuka kipindi fulani rais alisema eti "anasikitishwa sana na umaskini wa watanzania", kwangu nie kauli hii niliiona kuwa ni ya kizandiki isiyo na ukweli hata kidogo zaidi ya kujikomba kwa wananchi, kama kweli umaskini wa watanzania unamnyima usingizi mbona hatuoni lolote la maana analofanya kuwakwamua watanzania na umaskini huo, kazi imekuwa kupiga misele tu huko ughaibuni kuomba misaada, kweli Tanzania tumeshindwa kumanage resources tulizonazo hadi leo hii tumekuwa ombaomba..,ni aibu sana kwa kweli.

  Marehemu Baba wa Taifa [RIP] aliwahi kusema kuwa nchi hii haiwezi kuendelea kwa misaada, kwani ni uongo.., si haya tunayaona sasa, kama misaada tunayopewa ingeweza kutuendeleza sasa hivi tusingekuwa na unyonge huu tulionao, tungekuwa moja kati ya African Superpowers lakini misaada yote ya wazungu inaishia mifukoni mwa viongozi wetu kwa matumizi yasiyo na msingi hata kidogo..,inauma sana eti leo hii miaka 49 baada ya Uhuru Tanzania bado ina maeneo yasiyofikika kwa barabara, hayana umeme wala huduma za afya na maji safi na kila siku tunasikia misaada ya kuendeleza miundiombinu ya nini sijui.,mbona hawa wenzetu hawafaidiki nayo.,yote inaishia mikoa fulani fulani ambayo baadhi ya viongozi wanatoka na mikoa mingine inaendelea kukandamizwa.

  Ni aibu kubwa sana kwa Rais mzima kwenda huko ughibuni na kulia eti Tanzania haina dola nilioni 15, huu ni uongo wa hali ya juu, kama angejali kweli si serikali yake ingepunguza matumizi ya kipumbavu, hiyo bilioni 15 si ingepatikana fasta tu, ni picha gani ambay hawa viongozi wetu wanatujengea huko nje?, kwa mtaji huu tutaachaje kudharaulika huko duniani?.,wanapambana na ombaomba njiani wakati bwana mkubwa mwenyewe ndiyo ombaomba namba 1.,viongozi wetu lazima wabadilike kwa kweli, wamejisahau sana inawezekana ni kutokana na huu ukondoo tuliojivika sie wananchi..,lazima tupaze sauti zetu kukemea ujinga huu.,watatusikia tu kwani sisi si ndio waajiri wao jamani......?

  Naomba kuwasilisha.
   
 15. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  La hasha.

  Wanajua sio wote ni wajinga. Ila wanajua wengi kupindukia ni wajinga hivyo wanatumia hiyo fursa kujinufaisha.

  Wanajua werevu wachache hawawezi kuwawajibisha. Sio sasa wala hivi karibuni.
   
 16. K

  Kalimwage Member

  #16
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani Mkuu alienda bila kujitayarisha au wsaidizi wake walimwandalia hotuba kyk ndege na kuprint walipotua Airport Libya

  Inashangaza sana serikali ilishindwa kufanya tathmini ya hasara, any way amwombe Gadhafi

  vipi ha kwenda na mama salma, [/FONT]
   
 17. M

  Mndamba Member

  #17
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 22, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hapana; Wanajua sana. Ila sema tu kwamba huu ni utaratibu wetu wa kawaida hapa Tz kubadirisha badilisha makadilio ya ghalama za ujenzi ili mwishoni mwa siku kile cha juu kiweze kutunufaisha wachache. Kazi na dawa - Ufisadi kwa kenda mbele. (Yale ma-Twin Towers ya BOT) Watanzania tuna kazi ya ziada katika kuidhiti / kukomesha tabia hii miongoni mwa watendaji wetu.
   
 18. R

  Renegade JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  Maisha Bora kwa Mtanzania yanawezekana kweli?
  Matumizi ya serikali yako juu, kila siku wakuu ni ngonjera tu za kupunguza matumizi, Pinda alisema uongo kuwa serikali itasitisha matumzi ya Mashangingi, lakini mpaka sasa kitendawili,

  Umasikini unaongezeka, Sasa hivi Gap ya tajiri na masikini iko juu. Je kikwete unasemaje juu ya Hili? Embu punguza safari za nje walau kidogo tu ili pesa unazotumia kwenye safari ziweze kutumika sehemu nyingine, Au safari nyingine tuma mwakilishi au balozi akuwakilishe ili upunguze gharama.
   
 19. T

  TANURU Senior Member

  #19
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rev. Kishoka,

  Hoja nzito hizo. Usitegemee jibu.
   
 20. GY

  GY JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kishoka

  Naongezea tu kwenye analysis yako fupi kuwa Tanzania inazo pesa

  Tazama hivi kuna kesi ngapi mahakamani ambazo serikali inawashtaki watendaji wake na wafanyabiashara kwa kuchota pesa za umma

  • EPA 133b
  • BOT majengo pacha a.kak Liyumba scam 221b
  • BOT utangenezaji noti >100b
  • Mramba na mambo yake >13b
  • Ongeza nyingine
  Sasa unaweza kuibiwa kama huna? Maskini anaibiwa nini sasa wakati hana

  Zipo ndo maana zinaibiwa
   
Loading...