Rais anadanganywa na Watanzania tunadanganywa

Inafikirisha sana.

TANESCO walituambia kwamba umeme wanazalisha takribani 1600MW na matumizi ya Nchi nzima ni 1200MW ila jana wametoa taarifa wana upungufu wa 358MW hivyo wataanza mgao, swali langu kwa TANESCO mgao wa nini wakati tuna ziada ya 42MW?
Kati ya mambo yaliyomwondoa Kalemani, ni uwongo. Hata huko vijijini, baadhi ya vijiji walikuwa wanaunganisha nyumba 3 mpaka 5, wanaondoka. Yeye anakimbilia kwenye TV kutangaza kuwa vijiji 10 wananchi wameunganishwa uameme, kumbe wameunganishiwa nyumba 10 tu. Amekuja kuumbuka uwongo wake wakati walipoingiza kodi ya majengo kupitia LUKU.

KWA HIYO HATA HIZO Megawat walizokuwa wanasema kuwa walikuwa wanazalisha, bila shaka ulikuwa uwongo.
 
kwenye huu umeme ndugu yangu kuna siasa mingi mno, ni ngumu kujua nani anasema ukweli, Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati, Tanesco wenyewe au kambi ya Waziri wa zamani Kalemani.
PM tunafahamu kuwa huwa ni mwongo. Labda tuangalie statements za January na Rais, sijui mwongo wa kuungana na PM, ni nani kati ya hao wawili.
 
Hizi kauli huwa mnazitoa wapi nyie washamba ?
Hujawahi kujua Rais na Congress ya Marekani waliwahi kudanganya Iraq kuna silaha za maangamizi wakatoa idhin ya uvamizi?
Rais ni taasisi haiwezi kudanganywa!
 
Huyu mzanzibar ana uchingu na wabara watanzania tumefeli kama taifa
 
kwenye huu umeme ndugu yangu kuna siasa mingi mno, ni ngumu kujua nani anasema ukweli, Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati, Tanesco wenyewe au kambi ya Waziri wa zamani Kalemani.
Ukweli ni kuwa ukame hauji kama chafya.
 
Watu mmekuwa wepesi wa kusahau ! Huyu mama yenu ni matunda ya awamu ya 5 .

Awamu ya 5 ilikubuhu kwa uongo na misifa isiyokuwa na lazima mfano ni data za makusanyo ya kodi TRA, data za ujenzi wa miradi mikubwa , "uchafuzi mkuu 2020"

Kubwa la yote ni Jiwe alitengeneza tabia ya uongo ndio maana hadi kifo chake kilighubikwa na utata na uongo mwingi rejea Kassim alichosema msikitini kuwa Jiwe anasoma mafile yuko busy na tarehe Samia aliyosema jiwe alilazwa hadi kufariki, kwa tabia hiyo na mengine mengi itachukua walau miaka 7 nchi kurudi kwenye hali ya kawaida ila watu waliambiwa na hawakusikia kuwa nchi inaenda shimoni

Ni wakati sasa wa watanzania kuvuna matunda ya October 2020 waliposhindwa kuitetea demokrasia ya nchi
 
Kwanza Mama Shikamoo na Pole na Uchovu.

Kwa vile wewe najua unatupenda na una nia ya dhati ya kutuletea maendeleo ngoja nikupe kitu kidogo hapa.

Watanzania wote tulio umri kati ya miaka 20 hadi 100 tulikumbwa na UDUMAVU huko nyuma, usituone tunavaa na kupendeza ukazani sote tulikuwa hivyo huko nyuma. Naamini unaelewa nini maana ya UDUMAVU kwa sasabu ulipokuwa Makamu wa Rais ulishughulika sana na UDUMAVU kupitia wakuu wa mikoa.

Madhara ya UDUMAVU yametufanya tuwe na akili kidogo sana na kutotaka kufanya mambo yanayohitaji uthubutu wa kutuamia akili. Na kwa sababu hiyo tunapotewa jukumu tunajikuta tunahangaika na kutapata bila kulifanya kwa weledi. Hivyo tunakosa efficiency na kama hatujasimamiwa kwa mijaredi mambo huwa hayaendi.

Nikiwa kama mtaalamu wa kuibua miradi na kufuatilia hadi ikamilike nimejikuta natumia mda mwingi sana kusimamia watu kuliko kawaida na kipindi nikiwaachia tu wafanye wenyewe wanaharibu hata kama wanajua kuifanya hiyo kazi. Kazi nyingi hazifiki mwisho.

Tatizo linyoikumba hii nchi ni kwa sababu tu watu wamelegea sehemu baada ya kukosa mfuatiliaji. Ungeweza kufuatilia ungegundua unadanganywa kikubwa. Na ungegundua hata sisi Raia wako tunadanganywa huku ukweli tunaujua.

MIFANO:
1. Waziri wa Nishati anasema umeme unakatika kwa sababu ya matengenezo; Waziri mkuu anasema tuna umeme wa kutosha; TANESCO wanasema kuna uhaba wa Maji;

2. DASAWA wanasema kuna mgao wa maji kwenye maeneo ya mabonde na mtelemko isipokuwa Masaki na maeneo mengine ( Kwa taarifa tu ni kwamba Masaki hakuna Maji week ya pili): Wew unasema Maji hakuna kwa sababu mito imepungua maji. Yaani Mani yamechepushwa; CCM wanasema Mvua zimekaiwa ndio maana maji hakuna.

MAOMBI YANGU:
1. Swala la kupungua kwa Maji haliwezi kuja kama surprise lazima kuna sehemu kuna uzembe. Naomba ufuatilie kwa ukaribu; mtu mzembe asikuharibie mambo yako. Wazembe wote wakupishe. Ukiona mtu anamakundi yake muweke pembeni; Chukua damu mpya upige kazi.

2. Anza kwenda field mwenyewe; Toa mfano wa namna watendaji wako wanatakiwa kufanya kazi, ukweli ni kwamba hata wao hawajakuelewa unataka wafanyeje kazi. Kwa sasa wasaidizi wako wengi wakiwemo Mawaziri;RCs,DCs hawafanyi kazi wala hawajisumbui labda kama unakuja ziara. Wengi wanaamka wanakunywa supu, wanawasha gari wanazunguka kidogo wana rudi ofisin badae nyumbani.

3. Ongeza ukali kidogo, japo ukali ni hurka ya mtu lakini onesha ukali, usicheke na nyani tunaoumia ni sisi raia wa huku chini. Hata hiyo pesa ya kujenga shule kuna maeneo inapigwa vizuri tu na maisha yanasonga.

Tumia TIS wakusaidie.
Samia hawezi.
 
Hao wazembe ndo mama anawapenda sana maana huwa wanaporojo ningi kama makamba
 
Tatizo la Tanzania uendeshaji wa nchi unategemea akili za rais na siyo katika. Anachoamua rais ndiyo huwa na hela zote anazo yeye
Huo unaitwa ukweli mtupu

Yaaaaani eti hatma ya taifa iko kichwani kwa mtu mmoja anaejiita rais

Mi nadhani kuna haja ya bunge au iundwe tume ambayo itakuja na dira ya taifa yani malengo na matakwa ya wanainchi halafu katiba iwe pale kuyalinda hayo malengo kwa kipindi kama cha miaka kumi.

Baada ya hapo vyama vipewe hayo malengo katika kampeni zao za kuchukua nchi wazunguke na kuzurula majukwaani nchi nzima wakiwaeleza wanainchi watatimizaje malengo yetu kwa kipindi hicho tulichokubaliana.

Kama mgombea atashindwa kutuambia atayatimizaje watu keenye mkutano wasambae kwani hawafai na kama ataeleweka aelezee na aje na sababu za kueleweka ili kila mtu ajue tunakoelekea ili hata raisi akichepuka bunge na katiba vimsimamie na kumkumbusha kuwa malengo yetu ni haya na si hayo kama taifa.

Hii itaondo mikanganyiko ya kihulka za mtu, na ilani za vyama zisizotekelezeka

Sio mtu anakurupuka na ilani ya kipumbavu eti (milion 50 kila kijiji halfu kwenye utekelezaji eti tunafukuza vyeti feki) kompyuta kila mwalimu utekelezaji kujenga bwawa la umeme n.k

Hii itasaidia kila mmoja kujua tunakoelekea ila hata dereva akipotea sote tupige kelele na kumkumbush uelekeo wetu
 
Back
Top Bottom