Rais anadanganywa na Watanzania tunadanganywa

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
8,326
Reaction score
11,719
Kwanza Mama Shikamoo na Pole na Uchovu.

Kwa vile wewe najua unatupenda na una nia ya dhati ya kutuletea maendeleo ngoja nikupe kitu kidogo hapa.

Watanzania wote tulio umri kati ya miaka 20 hadi 100 tulikumbwa na UDUMAVU huko nyuma, usituone tunavaa na kupendeza ukazani sote tulikuwa hivyo huko nyuma. Naamini unaelewa nini maana ya UDUMAVU kwa sasabu ulipokuwa Makamu wa Rais ulishughulika sana na UDUMAVU kupitia wakuu wa mikoa.

Madhara ya UDUMAVU yametufanya tuwe na akili kidogo sana na kutotaka kufanya mambo yanayohitaji uthubutu wa kutuamia akili. Na kwa sababu hiyo tunapotewa jukumu tunajikuta tunahangaika na kutapata bila kulifanya kwa weledi. Hivyo tunakosa efficiency na kama hatujasimamiwa kwa mijaredi mambo huwa hayaendi.

Nikiwa kama mtaalamu wa kuibua miradi na kufuatilia hadi ikamilike nimejikuta natumia mda mwingi sana kusimamia watu kuliko kawaida na kipindi nikiwaachia tu wafanye wenyewe wanaharibu hata kama wanajua kuifanya hiyo kazi. Kazi nyingi hazifiki mwisho.

Tatizo linyoikumba hii nchi ni kwa sababu tu watu wamelegea sehemu baada ya kukosa mfuatiliaji. Ungeweza kufuatilia ungegundua unadanganywa kikubwa. Na ungegundua hata sisi Raia wako tunadanganywa huku ukweli tunaujua.

MIFANO:
1. Waziri wa Nishati anasema umeme unakatika kwa sababu ya matengenezo; Waziri mkuu anasema tuna umeme wa kutosha; TANESCO wanasema kuna uhaba wa Maji;

2. DASAWA wanasema kuna mgao wa maji kwenye maeneo ya mabonde na mtelemko isipokuwa Masaki na maeneo mengine ( Kwa taarifa tu ni kwamba Masaki hakuna Maji week ya pili): Wew unasema Maji hakuna kwa sababu mito imepungua maji. Yaani Mani yamechepushwa; CCM wanasema Mvua zimekaiwa ndio maana maji hakuna.

MAOMBI YANGU:
1. Swala la kupungua kwa Maji haliwezi kuja kama surprise lazima kuna sehemu kuna uzembe. Naomba ufuatilie kwa ukaribu; mtu mzembe asikuharibie mambo yako. Wazembe wote wakupishe. Ukiona mtu anamakundi yake muweke pembeni; Chukua damu mpya upige kazi.

2. Anza kwenda field mwenyewe; Toa mfano wa namna watendaji wako wanatakiwa kufanya kazi, ukweli ni kwamba hata wao hawajakuelewa unataka wafanyeje kazi. Kwa sasa wasaidizi wako wengi wakiwemo Mawaziri;RCs,DCs hawafanyi kazi wala hawajisumbui labda kama unakuja ziara. Wengi wanaamka wanakunywa supu, wanawasha gari wanazunguka kidogo wana rudi ofisin badae nyumbani.

3. Ongeza ukali kidogo, japo ukali ni hurka ya mtu lakini onesha ukali, usicheke na nyani tunaoumia ni sisi raia wa huku chini. Hata hiyo pesa ya kujenga shule kuna maeneo inapigwa vizuri tu na maisha yanasonga.

Tumia TIS wakusaidie.
 
Inafikirisha sana.

TANESCO walituambia kwamba umeme wanazalisha takribani 1600MW na matumizi ya Nchi nzima ni 1200MW ila jana wametoa taarifa wana upungufu wa 358MW hivyo wataanza mgao, swali langu kwa TANESCO mgao wa nini wakati tuna ziada ya 42MW?
 
Rais anadanganganywa mchana kweupe.

Watanzania tunadanganywa mchana kweupe.

Kuna genge hatari limeishika serikali bila ya mama kujua.

Wanajua anapenda safari, na wanatumia mwanya huo kumfanya asijuwe kinachoendelea site.

Kama walivyompangia safari ya Tanga wakabaki wakimalizia kazi na Dk yuleee!

Kuna haja ya kamati ya bunge kutembelea site ili watanzania tuujuwe ukweli.
 
Inafikirisha sana.

Tanesco walituambia kwamba umeme wanazalisha takribani 1600MW na matumizi ya Nchi nzima ni 1200MW ila jana wametoa taarifa wana upungufu wa 358MW hivyo wataanza mgao, swali langu kwa TANESCO mgao wa nini wakati tuna ziada ya 42MW?
kwenye huu umeme ndugu yangu kuna siasa mingi mno, ni ngumu kujua nani anasema ukweli, Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati, Tanesco wenyewe au kambi ya Waziri wa zamani Kalemani.
 
Heshima yako kiongozi!

Tukubali ni wanadamu wanaweza danganywa au kudanganya kwa kujua au kutokujua.
 
kwenye huu umeme ndugu yangu kuna siasa mingi mno, ni ngumu kujua nani anasema ukweli, Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati, Tanesco wenyewe au kambi ya Waziri wa zamani Kalemani.

Tanesco ndiyo wataalam hao wengine ni wanasiasa wanaopokea ripoti kutoka TANESCO kuhusu capacity na utilization.

Kwahiyo hapa sisi tunambana TANESCO.
 
Tatizo la Tanzania uendeshaji wa nchi unategemea akili za rais na siyo katika. Anachoamua rais ndiyo huwa na hela zote anazo yeye
 
kaka umeandika kifupi lakini huo ndiyo ukweli, Mamlaka ya Katiba ya nchi ni sawa sawa na Mamlaka ya Rais. Kwa maneno mengine Rais akishaapishwa tu basi muda huo huo anageuka na kuwa KATIBA.
 
Rais anadanganganywa mchana kweupe.

Watanzania tunadanganywa mchana kweupe.

Kuna genge hatari limeishika serikali bila ya mama kujua.

Wanajua anapenda safari, na wanatumia mwanya huo kumfanya asijuwe kinachoendelea site.

Kama walivyompangia safari ya Tanga wakabaki wakimalizia kazi na Dk yuleee!

Kuna haja ya kamati ya bunge kutembelea site ili watanzania tuujuwe ukweli.
Kamati ya bunge tena?
Iundwe tume huru, kama tume iliyochunguza soko la kariakoo.
 
Kaka siyo vizuri hivyo kuchongeleana.
Huo ndio ukweli mtupu wanazunguka na gari na kurudi kwa ofisi!
Mnashindwa nini kwenda kwa wananchi mkayaona wanayoyaishi.
Hapa kijijini kwetu hatujawahi kumwona mkuu wa mkoa wala mbunge kututembelea.
 
Kabisa kabisa.
 
Kwanza Mama Shikamoo na Pole na Uchovu.

Kwa vile wewe najua unatupenda na una nia ya dhati ya kutuletea maendeleo ngoja nikupe kitu kidogo hapa.

Watanzania wote tulio umri kati ya miaka 20 hadi 100 tulikumbwa na UDUMAVU huko nyuma, usituone tunavaa na kupendeza ukazani sote tulikuwa hivyo huko nyuma. Naamini unaelewa nini maana ya UDUMAVU kwa sasabu ulipokuwa Makamu wa Rais ulishughulika sana na UDUMAVU kupitia wakuu wa mikoa.

Madhara ya UDUMAVU yametufanya tuwe na akili kidogo sana na kutotaka kufanya mambo yanayohitaji uthubutu wa kutuamia akili. Na kwa sababu hiyo tunapotewa jukumu tunajikuta tunahangaika na kutapata bila kulifanya kwa weledi. Hivyo tunakosa efficiency na kama hatujasimamiwa kwa mijaredi mambo huwa hayaendi.

Nikiwa kama mtaalamu wa kuibua miradi na kufuatilia hadi ikamilike nimejikuta natumia mda mwingi sana kusimamia watu kuliko kawaida na kipindi nikiwaachia tu wafanye wenyewe wanaharibu hata kama wanajua kuifanya hiyo kazi. Kazi nyingi hazifiki mwisho.

Tatizo linyoikumba hii nchi ni kwa sababu tu watu wamelegea sehemu baada ya kukosa mfuatiliaji. Ungeweza kufuatilia ungegundua unadanganywa kikubwa. Na ungegundua hata sisi Raia wako tunadanganywa huku ukweli tunaujua.

MIFANO:
1. Waziri wa Nishati anasema umeme unakatika kwa sababu ya matengenezo; Waziri mkuu anasema tuna umeme wa kutosha; TANESCO wanasema kuna uhaba wa Maji;

2. DASAWA wanasema kuna mgao wa maji kwenye maeneo ya mabonde na mtelemko isipokuwa Masaki na maeneo mengine ( Kwa taarifa tu ni kwamba Masaki hakuna Maji week ya pili): Wew unasema Maji hakuna kwa sababu mito imepungua maji. Yaani Mani yamechepushwa; CCM wanasema Mvua zimekaiwa ndio maana maji hakuna.

MAOMBI YANGU:
1. Swala la kupungua kwa Maji haliwezi kuja kama surprise lazima kuna sehemu kuna uzembe. Naomba ufuatilie kwa ukaribu; mtu mzembe asikuharibie mambo yako. Wazembe wote wakupishe. Ukiona mtu anamakundi yake muweke pembeni; Chukua damu mpya upige kazi.

2. Anza kwenda field mwenyewe; Toa mfano wa namna watendaji wako wanatakiwa kufanya kazi, ukweli ni kwamba hata wao hawajakuelewa unataka wafanyeje kazi. Kwa sasa wasaidizi wako wengi wakiwemo Mawaziri;RCs,DCs hawafanyi kazi wala hawajisumbui labda kama unakuja ziara. Wengi wanaamka wanakunywa supu, wanawasha gari wanazunguka kidogo wana rudi ofisin badae nyumbani.

3. Ongeza ukali kidogo, japo ukali ni hurka ya mtu lakini onesha ukali, usicheke na nyani tunaoumia ni sisi raia wa huku chini. Hata hiyo pesa ya kujenga shule kuna maeneo inapigwa vizuri tu na maisha yanasonga.

Tumia TIS wakusaidie.
Hiyo TIS ni aheri wangebadilishiwa jina, waitwe TOS.

Tanzania Obtuseness Services.
 
Back
Top Bottom