Rais amwita wema kwake

Rais amwita Wema Sepetu chumbani kwake, nia ni kumliwaza. Amtumia gari na mpambe... Habari kamili uk wa 4....

NIKANUNUA GAZETI MAANA YALIKUWA YAMEWEKWA CHINI YA MIPIRA HUWEZI FUNGUA NDANI.

Uk wa 4 sasa,

Rais wa Manzese madee mwenye chumba kimoja hapo manzese, hivi karibuni alimtumia tax Wema Sepetu na kumkaribisha kwake ili amliwaze kwa msiba ulotokea hivi karibuni. Dereva wa tax hiyo alieleza kuwa baada ya kufika nyumbani kwa wema, aligoma kupanda gari hilo hivo kuondoka mikono mitupu. Nkasema moyoni leo wameniokota hawanipati tena.



....hahahahahah lol! mie pia niliwahi kukutwa na hili. Nilikuwa naangalia vichwa vya habari katika magazeti mbali mbali (kwa muuza magazeti) basi nikaona kichwa cha habari kisemacho, "Rais apata ajali" halafu habari iko ndani ya gazeti. Lilikuwa ni moja ya magazeti haya ya hovyo hovyo, basi nikaamua kulinunua. Kule ndani kumbe ni Rais wa chama cha ngumi nchini (wakati huo) alikuwa Emanuel Mlundwa ndiye aliyepata ajali. Sikusoma kingine chochote katika gazeti lile na niliamua kulitupa.
 
Hahaha! Pole mkuu. Hongera kwa uamuzi wa wa kuacha kununua. Nakumbuka gazeti moja zamani liliwahi kuandika "Osama Akamatwa" halafu kwenye maelezo kumbe aliyekamatwa ni Osama wa Manzese. Tusiponunua watajifunza.
 
Nadhani wanafanya hivi makusudi kwa sababu wanajua kuwa sisi wasomaji tu-wambea sana, km si wadadisi.
 
... OMG.. I love this !! Kwanza hakuwa Rais aliyekuwa kichwani kwangu, pili Wema mwenyewe didnt go ... !!!
 
Teh te te teh! Pole sana mdau, wadau wengi tu walishawahi kuokotwa na hayo magazeti. Hata hapa jf kuna mwendawazimu alishawahi kutuokota! Aliandika "waziri afikishwa kortini kwa kubaka", kumbe ni jamaa wa wapi sijui huko anaitwa waziri ally.
 
pole mwaya, mi hayo matakataka huwa yananiboa kweli kwa kuzidisha chumv
 
mmmh...kweli mjini hapa!me mwenyewe nlikuwa nshaamini na nilikuwa nimeandaa bonge la comment nilivosoma kichwa cha habari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom