Rais ajaye 2025 ni kanda ya kati Dodoma

Rais ajaye 2025 ni kanda ya kati Dodoma

Palamagamba
Wanajamvi, nawasalimia sana. Si vibaya tukaanza kumtafuta rais atakayepokea kijiti toka kwa JPM. Na wala siyo vibaya rais ajaye akawa ni mtu mwenye sifa zoote zinanazohitajika kutokea kanda ya kati mikoa ya Dodoma na Singida. Zanzibar tayari, kusini tayar, kanda ya ziwa tayar, magharibi tayari. Kanda zilizobaki ni 2, kanda ya kati na kaskazini kabla hatujarudi tena Zanzibar. Angalizo, maoni haya yasipokelewe kwa mtizamo wa ubaguzi wa kikanda, bali desturi nzuri isiyo andikwa popote lakini yenye manufaa makubwa.
 
The next President is a Muslim kwahiyo wakati mnaendelea kupiga ramli zenu hiki kigezo mkizingatie
 
Halafu mods mnalala sana huu uzi hapa sio mahala pake
 
Nadhani ukanda hauna nafasi,ila ikitokea mtu anauwezo hata akitoka Chato Si mbaya,tukianza kusema ukanda nasisi wa Nyanda za juu kusini tutaingia barabarani kudai zamu yetu ila kwasababu tunaangalia competence na Si eneo analotoka mtu,basi tubaki na misimamo huo kabla hamjatuamsha na ukanda
 
The next President is a Muslim kwahiyo wakati mnaendelea kupiga ramli zenu hiki kigezo mkizingatie
Muslim???? Au tunaangalia mwenye uwezo maana wapagani tupokimya tu hatujapata muwakilishi bado,msituamshe ktk udini maana bado hatujawakilishwa sisi wenye miungu mingine
 
Muslim???? Au tunaangalia mwenye uwezo maana wapagani tupokimya tu hatujapata muwakilishi bado,msituamshe ktk udini maana bado hatujawakilishwa sisi wenye miungu mingine
Kundi lenu halitambuliki inakubidi tu uwe mpole hakuna udini ni utaratibu tu
 
Bora tuchague jiwe kuliko mutu ya kanda ya kati...

Wengi bdo wana akili za kimasikini..
 
Kanda ya kati inahitaji mkombozi period. Ipeleke mtu akachungulie jikoni. Nimepita mikoa ya singida na dodoma nimegundua kuwa wanahitaji mkakati kabambe wa kuondoa umasikini. Sasa wakiwa na rais pale ikulu, hoja hii itawawia nyepesi.
Kama kanda ya kaskazini haijawahi kuwa na Rais lakini iko mbele kimaendeleo nini kimekufanya utake kutuaminisha Rais kutoka haya maeneo ndiyo atawaondolea umasikini. Labda nikukumbushe kusini walishatoa huyo Rais but huwezi kufananisha na kaskazini hata sasa wana hadi waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom