Raia wa Tanzania nchini Marekani watuma ujumbe

raia wa tanzania wanaoishi na kufanya shughuli zao nchini marekani wametuma ujumbe kwa wananchi wa hapa tanzania wakiwataka kutumia hekima na busara zao katika kuchagua viongozi wenye sifa stahiki ambao pia watakubalika na mataifa ya ulaya na marekani.

Aidha wamesema ni vema katika uchaguzi huu tukachagua rais mwenye uwezo binafsi, utendaji uliotukuka, asiye na doa na anaechukia rushwa ili kusaidia tanzania kupiga hatua za kimaendeleo.

Wananchi hao wameenda mbali na kusisitiza kuwa tunapaswa kuwa mbali na wale wote wenye harufu ya rushwa, tamaa ya madaraka kwani hawafai kabisa, wataturudisha nyuma kimaendeleo.

lowassa ndio chaguo lao ndugu.usizunguke mbuyu.
 
Wangeandika tu wazi wazi kuwa mwaka huu Watz tusijinyonge tena na Kamba ile ile ya miaka yoote tangu uhuru. Tutafute tena nyingine angalao tulete mabadiliko.
Huwezi ogea tope kwenye chungu kile kile useme utatakata. MABADILIKO NI LAZIMA. Wao wakitaka waje kupiga kura au wakae huko ughaibuni, sisi tulio nyumbani tunatosha kuwaletea hayo mabadiliko. LOWASA ATOSHAAAAAAA
 
Ulizania wao hawajitambui kama wewe?
 
Raia wa Tanzania wanaoishi na kufanya shughuli zao nchini Marekani wametuma ujumbe kwa wananchi wa hapa Tanzania wakiwataka kutumia hekima na busara zao katika kuchagua viongozi wenye sifa stahiki ambao pia watakubalika na mataifa ya Ulaya na Marekani.

Aidha wamesema ni vema katika uchaguzi huu tukachagua rais mwenye uwezo binafsi, utendaji uliotukuka, asiye na doa na anaechukia rushwa ili kusaidia Tanzania kupiga hatua za kimaendeleo.

Wananchi hao wameenda mbali na kusisitiza kuwa tunapaswa kuwa mbali na wale wote wenye harufu ya rushwa, tamaa ya madaraka kwani hawafai kabisa, wataturudisha nyuma kimaendeleo.

Wangeanza kumgomea vasco da gama asikutane nao maana ndio kubwa LA maadui
 
I see! Walioko Marekani eti?! Ushauri wao huu nauchukulia kama chozi la samaki tu.
 
Raia wa Tanzania wanaoishi na kufanya shughuli zao nchini Marekani wametuma ujumbe kwa wananchi wa hapa Tanzania wakiwataka kutumia hekima na busara zao katika kuchagua viongozi wenye sifa stahiki ambao pia watakubalika na mataifa ya Ulaya na Marekani.

Aidha wamesema ni vema katika uchaguzi huu tukachagua rais mwenye uwezo binafsi, utendaji uliotukuka, asiye na doa na anaechukia rushwa ili kusaidia Tanzania kupiga hatua za kimaendeleo.

Wananchi hao wameenda mbali na kusisitiza kuwa tunapaswa kuwa mbali na wale wote wenye harufu ya rushwa, tamaa ya madaraka kwani hawafai kabisa, wataturudisha nyuma kimaendeleo.

Nakubaliana nao kwa mambo mengi waliyosema ila hatujachagui Raisi ambaye anakubaliki ulaya au Marekani.Tunachagua Raisi ambaye anaweza kuitumikia nchi yetu tukufu ya Tanzania basi kwa moyo wote na maarifa ya hali ya juu.
 
Sawa sawa waambie kuwa ukawa tunaendelea kupokea wale wote wanaokimbia mfumo dhalimu unaonuka rushwa kila kona kwa kujiunga na safari ya ukombozi wa taifa letu.
 
Mimi nipo illinois marekani hivi sasa ni saa tatu na dakika 27 asubuhi nipoandika text hii huku
ni lowassa kama
wangeturuhusu kupiga kura ccm ingepata asilimia mbili au tatu tu kwani
hatuwezi kukubaliana na ujinga wa ccm kuendelea kuwafanya watanzania mbumbu ili uwe mtaji
wao wakati wa uchaguzi
hakuna mtu muelewa na mwenye ufahamu mpana anaweza kushabikia ccm
 
Kuna watu bado wanaamini kuwa wakisema " Raia wa Tanzania nchini Marekani watuma ujumbe" basi watu wote tutatetemeka. Walioko Kenya, Uganda, Malawi, Msumbiji,Burundi,Rwanda,Zambia, Ulaya, Uarabuni, na kwingineko nao wanasemaje?
 
Huyo MALAIKA asiye na doa mbona hayupo kwenye kinyang'anyiro hiki,au wanamaanisha nini kusema kiongozi asiye na doa?
 
Raia wa Tanzania wanaoishi na kufanya shughuli zao nchini Marekani wametuma ujumbe kwa wananchi wa hapa Tanzania wakiwataka kutumia hekima na busara zao katika kuchagua viongozi wenye sifa stahiki ambao pia watakubalika na mataifa ya Ulaya na Marekani.

Aidha wamesema ni vema katika uchaguzi huu tukachagua rais mwenye uwezo binafsi, utendaji uliotukuka, asiye na doa na anaechukia rushwa ili kusaidia Tanzania kupiga hatua za kimaendeleo.

Wananchi hao wameenda mbali na kusisitiza kuwa tunapaswa kuwa mbali na wale wote wenye harufu ya rushwa, tamaa ya madaraka kwani hawafai kabisa, wataturudisha nyuma kimaendeleo.
Mtu anaye kubaliki Ulaya na marekani??????.... Kwa kauli yao hiyo waambie kuwa wao ni wapuuzi.
 
Raia wa Tanzania wanaoishi na kufanya shughuli zao nchini Marekani wametuma ujumbe kwa wananchi wa hapa Tanzania wakiwataka kutumia hekima na busara zao katika kuchagua viongozi wenye sifa stahiki ambao pia watakubalika na mataifa ya Ulaya na Marekani.

Aidha wamesema ni vema katika uchaguzi huu tukachagua rais mwenye uwezo binafsi, utendaji uliotukuka, asiye na doa na anaechukia rushwa ili kusaidia Tanzania kupiga hatua za kimaendeleo.

Wananchi hao wameenda mbali na kusisitiza kuwa tunapaswa kuwa mbali na wale wote wenye harufu ya rushwa, tamaa ya madaraka kwani hawafai kabisa, wataturudisha nyuma kimaendeleo.

Kumchagua rais mzur kama Magufuri
 
Raia wa Tanzania ya wapi? Rais ambaye hana kashfa ni Lowassa tu.
 
Watueleze kilichowakimbiza tz, Na kuwepo kwao USA kumesaidia nini tz Na watz, watambue tunajua walio wengi hawawezi kupata kazi nzuri Kwa sababu ya elimu Na makuzi, Na Kama wanawaunga mkono waliowasababishia hayo, ni vyema wabaki huko, tutengeneze kizazi kitakachoweza kukabiliana Na mataifa mengine kielimu, kifikira Na kiuchumi.
 
Ila mimi nimeambiwa chagueni raisi mzuri Lowasa sio wanao kuwa kama mamoko kwenye jukwaa tena wamesisitiza kwamba msichague rais anaye rukaruka na kujamba jukwani ataharibu Tanzania
 
Back
Top Bottom