Raia wa kigeni wanatuchukuliaje na utawala huu?!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,072
114,560
Salaam
Binadam tumeumbwa na hofu. Kama sio hofu ya Mungu basi hata hofu ya watu wanaokuzunguka ambao mara nyingi ni wadau wako!Unapotaka kufanya tukio huwezi kufanya bila kufikiria mapokeo ya wadau wako........"hivi satanic humiliate".

Katika mazingira hayo wengi tunajitahidi kufanya yaliyo sahihi hata kama yatawaumiza wengine!

Najiuliza sana kwa jinsi hali ilivyo hapa nchi ni kwetu,wadau wetu wanajenga picha gani?

Hakuna ubishi kwamba yapo matukio na matamko yamefanyika au yanafanyika nchini. Kiongozi anaweza akatamka au kufanya kitu cha ajabu kabisa kiasi cha kustaajabisha na hata kudhalilisha.

Mifano ipo mingi sana,lakini kwa uchache

Mimi sina mahusiano na raia wa kigeni,kwa wana jukwaa hebu tupashane habari ni vipi wenzetu wanatuchulia. Wakenya wanaposikia tunagombania rambirambi wanatuonaje!Wanaposikia rais anavunja katiba na wananchi wako kimya tu,nini wanakijenga vichwani?Kuna mkenya mmoja aliwahi kutoa kauli mbaya sana mitandaoni kwamba wasukuma wawili wanaswaga ng'ombe milioni 50,kwa kweli nilifadhaika sana

Nadhani umenipata
 
Wenye akili wanatuona ni kama wana wa Israel walivyomangamanga na nyika miaka arobaini kwa makosa yao ya ukaidi. Ni kama wale wa mnara wa Babeli walivyosambaratika. What a shame!
 
Shida ya Watanzania ni kwamba hatujui tunachokitaka. Wakati wa Mr. Dhaifu malalamiko yalikuwa maradufu. Naamini hata atakayekuja hali itakuwa ni ile ile.

Kuna mvuvumko wa nationalism mpaka wachambuzi wengine wameanza kuhoji kama pengine mfumo wa kidemokrasia umechakaa na dunia inajaribu kutafuta mfumo mpya. Kuanzia kwa polisi wa kueneza demokrasia duniani (hasa kama una natural resources wanazozitaka) Marekani kwenyewe Trump hapendi demokrasia sema tu taasisi zao zina nguvu na zinapambana. Warusi kule. Turkey. Na kwingineko.

Pengine wakati umefika kila jamii itafute demokrasia na mfumo wake wa kujitawala. Tatizo ni kwamba kwa Afrika sijui hata kama tunajua hata tunachokitaka. Huo ndiyo wasiwasi wangu. Hata opposition, kwa vile nao ni zao la mfumo ule ule, hawajui wanachokitaka mbali tu na kushika madaraka ili nao wapate nafasi ya kula. Tuna tatizo...

Kama ningekuwa wewe nisingejali sana jinsi raia wa kigeni wanavyotuona bali ningehangaika na sisi tunavyojiona wenyewe. Tunajielewa? Tunajua tunachokitaka? Tufanye nin?
 
Shida ya Watanzani ni kwamba hatujui tunachokitaka. Wakati wa Mr. Dhaifu malalamiko yalikuwa maradufu. Naamini hata atakayekuja hali itakuwa ni ile ile.

Kuna mvuvumko wa nationalism mpaka wachambuzi wengine wameanza kuhoji kama pengine mfumo wa kidemokrasia umechakaa na dunia inajaribu kutafuta mfumo mpya. Kuanzia kwa polisi wa kueneza demokrasia duniani (hasa kama una natural resources wanazozitaka) Marekani kwenyewe Trump hapendi demokrasia sema tu taasisi zao zina nguvu na zinapambana. Warusi kule. Turkey. Na kwingineko.

Pengine wakati umefika kila jamii itafute demokrasia na mfumo wake wa kujitawala. Tatizo ni kwamba kwa Afrika sijui hata kama tunajua hata tunachokitaka. Huo ndiyo wasiwasi wangu. Hata opposition, kwa vile nao ni zao la mfumo ule ule, hawajui wanachokitaka mbali tu na kushika madaraka ili nao wapate nafasi ya kula. Tuna tatizo...

Kama ningekuwa wewe nisingejali sana jinsi raia wa kigeni wanavyotuona bali ningehangaika na sisi tunavyojiona wenyewe. Tunajielewa? Tunajua tunachokitaka? Tufanye nin?
Udhaifu wa JK haumpi tiketi Magufuli kulea RC wa ajabu ajabu kama Makonda na Gambo,hakumpi tiketi ya kugawa watu kwa misingi ya vyama,au dharau na dhihaka kwa wengine,hata ukiukaji mkubwa wa katiba na migawanyo wa mihimili
 
Hoja yangu ya msingi umeielewa mkuu? I have this impression that you are a great thinker ndiyo maana nikatoa hoja hiyo ya jumla. I might be wrong. Sorry!
 
Kuna mkenya mmoja aliwahi kutoa kauli mbaya sana mitandaoni kwamba wasukuma wawili wanaswaga ng'ombe milioni 50
Huo ndo ukweli wenyewe mkuu wala hakuna sababu ya kugadhabika!! Sisi ni maiti ndo maana tunafanywa kama wanavyotaka!!
 
Hatuna tofauti na watu wa Zimbabwe.
Kuogopa kumpa mtu ukweli hadi maangamizi ya vizazi vinne vijavyo yanatamalaki.
 
Inashangaza raia wanaogopa utawala badala ya utawala kuogopa raia.wenzetu wakenya kwenye hili nawapa heko
 
Back
Top Bottom