Joseph
JF-Expert Member
- Aug 3, 2007
- 3,518
- 1,086
Namshukuru sana Mchambuzi kwa kuleta article yake ambayo kwa mtazamo wake yeye ina ukweli ndani yake wakati hali halisi si kweli.Ninachojua mimi katika mitandao mingi ni kuwa unaruhusiwa kupiga kura baada ya kuwa mwanachama/member wa mtandao husika na huruhusiwi kupiga kura mara mbili,wanaosema wamepiga mara kumi nadhani kuna mashaka juu ya hilo.
Cha msingi tuangalie uhalisia wa jambo hili la kura hizi za maoni kupitia katika mitandao,magazeti ya serikali mf.Daily News walianzisha kura ya maoni na kilichowapata natumai wengi tunakijua na hata ukiangalia katika mitandao mingune utaona kuwa kilichokuwa kinasemwa na mwandishi wa Raia Mwema ni kweli na hakuna sababu ya kuanza kubeza kilichoandikwa.
REDET NA SYNOVATE wameendesha kura ya maoni kwa kuwahoji watu wasiozidi mia mbili na wamepata majibu yao ambayo naona kwako ni furaha tele na hujataka hata kuyagusia,je data zao na za JF na mitandao mingine unataka tuamini kuwa ni za uongo?Hata kura zilizopigwa Daily News ni za uongo mpaka zikafutwa?