Elections 2010 Raia Mwema: Dk Slaa awataka Duni, Hamad wa CUF

Kila mtu ana historia yake, ya kijamii, ya kimasomao, ya kikazi, ya kidini.
Tunawakataa wagombea au tunawakubali kwa kuangalia historia zao kujua tabia zao, pia tunaangalia mahusiano yao ya zamani na sasa na namna yanavyomfanya aweze au ashindwe kutumikia vizuri zaidi.
Nyerere, (hapendi uonevu wa ki-rangi) alikuwa hodari, alifaa kwa kupigania uhuru na kuanza nchi changa?
Mwinyi, (hapendi mtu apate shida) alikuwa mpole mvumilivu alitufaa kuvumilia mabadiliko ya kiuchumi an akimtazamo?
Mkapa, (alikuwa jasiri, anajiamini) alitufaa kubadilisha vitu ambavyo vilikuwa vinaenda kwa mazoea?
Kikwete (anapenda watu wafurahi-anaowajua au kujua habari zao) alitufaa wakati alipokuwa balozi
 
Hatutaki mabadiliko yaliyotoka kanisani yenye agenda ya kikanisa, tunataka mabadiliko yaliyotoka kwa wananchi yenye agenda ya kuhudumia wa Tanzania wa dini zote. na kuheshimu dini zote ..Padre kuwa rais ni BIG NO!

tupe source ya kwamba agenda hii ya mabadiliko imetoka church!
 
Raia Mwema: Slaa awataka Duni, Hamad wa CUF

Baada ya mgombvea urais kupitia Chadema, Dk W. Slaa kubadili upepo wa kisiasa nchini kuelekjea uchaguzi mkuu mwaka huu, chama hicho sasa kimo katika mkakati mahsusi wa kumpata mgombea mwenza mwenye ushawishi mkubwa kuroka kutoka CUF, Raia Mwema imethibitishiwa.

Habari za uhakika kutoka Chadema na CUF zimethibitisha kwamba mazungumzo yasiyo rasmi yamekwisha kuanza pamoja na kuwa tayari m,ajina mazito ya wanasiasa kutoka Zanzibar yameanza kutajwa kuombwa kuwa pamoja na Dk Slaa katika uchaguzi huo wa Oltoba 31.

Wanaotajwa ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Juma Duni Haji na aliyekuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, ambao wote ni watu wenye ushawishi mkubwa katika siasa za Visiwani na Bara.

Duni ambaye tayari CUF imemteua kuwa mgombea mwenza wa Preof Ibrahim Lipumba, anayebeba kwa mara ya nne bendera ya chama hicho katika kuwania urais, anatajwa kutakiwa na Chadema kutokana na ushawishi wake ndani ya siasa za Zanzibar na hata Bara.

Kwa mujibu wa habari hizo, kukubali kwa Duni kutategemea zaidi msimamo wa chama chake katika kumuunga mkono Dl Slaa, hatua ambayo imeelezwa kuanza kujadiliwa katika vikao visivyo rasmi kabla ya kuingia katika vikao rasmi vya vyamna hivyo ili hatimaye kufikia uamuzi.

Mwaka 200 Chadema walimuunga mkono mgombea urais wa CUF, Prof Lipumba, ambako katika mikutano yake nchi nzima alisimama kuwapigia debe wagombea wa Chadema na CUF huku mitandao ya vyama hivyo ikitumika katika harakati za kampeni hizo, hali ambayo inaelezwa kupendekezwa kuwapo katika katika uchaguzi wa mwaka huu.

Kwa upande wa Hamad Rashid, anatajwa kama ni mtu aliye karibu na Dk Slaa wakiwa wamefanya kazi kwa muda mrefu bungeni katika ofisi ya Kambi ya Upinzani, na anatajwa kuwa mmoja wa wanasiasa waliomshawishi mwanasiasa huyo wa Chadema kuwania urais.

….Habari zaidi katika Raia Mwema ya leo – mwenye full soft copy yake atuwekee tafadhali.


My take:

This story is too good to be true, though it has certain convincing elements. Can that be possible?

Good move, brilliant pass from Chadema and Dr. Slaa is in the mi,,,,..............
 
Marafiki na jamaa zangu wengi sana ni wana CUF.. Na mimi sikujiunga na chama hicho kwa sababu tu ya dhana kubwa ya wanachama wake kwamba CCM ni chama kinachoendeshwa na Vatican..Sikupenda mtazamo wao wakisiasa ambao nilijua toka zamani kutawakosesha kura za wananchi.

CUF ilishindwa mwaka 2000 kwa sababu ya kutumia tiketi hii kuomba kura za wananchi..Naamini kabisa Nyerere hakuwa sababu ya wananchi kumchagua Mkapa isipokuwa matumizi ya mbinu ya Udini ndiyo yalikuwa sababu kubwa ya ushindi wa CCM na Mkapa bara pamoja na kwamba CUF na Chadema waliunganisha nguvu zao nyuma ya Lipumba..

Sasa ni mategemeo yangu Watanzania wamejifunza, lakini kwa vile sisi Watanzania tuna tabia ya kutokubali ukweli hasa pale tunapokuwa wahusika wakubwa wa madhara hutafuta sababu nyingine kinyume cha kujitazama sisi wenyewe kuwa ndio sababu. Na kwa tabia hii tumeshindwa kusoma alama zile za mwaka 2000 pamoja na kwamba Lipumba alikuwa na sifa zote kuliko Mkapa..Dejavu - mambo yanajirudia kutokana na Wadanganyika kutokuwa na kumbukumbu.

Nitarudia kusema hivi, ikiwa wana CUF mnaamini kwamba utawala wa CCM unaendeshwa na kanisa iweje leo mkataba wao umeisha kwa sababu kasimama DR.Slaa? na hivi kweli ktk kujenga hoja kama hizi hamuoni kama ndio mnazidi kupoteza nafasi ya CUF, chama ambacho kimekuwa kikipigana kwa muda mrefu kufuta hizi tuhumu za Udini ambazo ndizo zimekifikisha hapa kilipo?..

Tusijidanganye wakuu zangu CUF ingeweza sana kuwa imara na mbadala kama kingeweza kujitangaza chenyewe kama chama na kinachoweza kuleta maendeleo nchini badala ya muda mrefu kuzungumzia CCM na Chadema ni vyama vya aina gani ili kujenga chuki ya kiimani. Tabia kama hizi huitwa Unafiki na hakika kila mtu hujiweka mbali na mnafiki akijua kwamba siku zote hutazama maisha ya wengine na kusambaza habari wakati yake mwenyewe yanamshinda.

Ni wakati wa kuondoa tofauti zetu, kuunganisha nguvu na kama kweli huyo Dr.Slaa ametumwa na kanisa sii itakuwa vizuri kama nawe ukiwa ndani mshirika ukayajua zaidi yaliyofichika kuliko kukaa nje ukidhania!..Ni imani yangu kwamba mtu yeyote anayelialia na kanisa kutawala nchi yetu alipenda kuona misikiti ikichukua nafasi ya kanisa..Na kwa sababu kama hizi ndio maana nashindwa kujiunga na CUF kwani naelewa fika kuwa ndani ya nyumba yangu ya Uislaam Tanzania kumejaa unafiki mtupu. Viongozi wangu wa dini ni wanafiki, wezi, mafisadi na informer wakubwa wa chama CCM na mafisadi wake.

Nilikuwepo!
 
Mwambieni Slaa aache kampeni za makanisani! Ujumbe uliotolewa makanisani Jumapili iliyopita umewafikia wengi. Mnajisumbuwa!
 
mhn ! na mimi naombsa kujua ni ujumbe gani huo ! mechi naona imeanza mapema na vuvu zela zinaanza kunguruma hata kabla mtu hajapigwa chenga .:A S-heart-2: presha zina panda, presha zinashuka
 
Muheshimiwa kama na wewe umepata malaria sugu twambie,kwani padri siyo Mtanzania?kila mtanzania anahaki ya kuwa kiongozi hata wewe umechina kwa sms yako nakushauri ufatilie kin achoendelea katika maeneo ambayo ameshapita.
 
waumini wa dini zote ndiyo wapiga kura na imani Slaa hayuko kanisani wakati huu,kwanini anawagusa mwacheni Mungu anapompa kibali Mtu atainuliwa na watu wote,kikwete anajiinua mwenyewe ndiyo maana hana jipya..................................Mtashangaa na roho zenu mwachi mtu wa watu tunampenda na tutamzungumza kila kona jinyonge ukitaka.
 
raia mwema: Slaa awataka duni, hamad wa cuf

baada ya mgombvea urais kupitia chadema, dk w. Slaa kubadili upepo wa kisiasa nchini kuelekjea uchaguzi mkuu mwaka huu, chama hicho sasa kimo katika mkakati mahsusi wa kumpata mgombea mwenza mwenye ushawishi mkubwa kuroka kutoka cuf, raia mwema imethibitishiwa.

habari za uhakika kutoka chadema na cuf zimethibitisha kwamba mazungumzo yasiyo rasmi yamekwisha kuanza pamoja na kuwa tayari m,ajina mazito ya wanasiasa kutoka zanzibar yameanza kutajwa kuombwa kuwa pamoja na dk slaa katika uchaguzi huo wa oltoba 31.

wanaotajwa ni pamoja na naibu katibu mkuu wa cuf, juma duni haji na aliyekuwa kiongozi wa upinzani bungeni na mbunge wa wawi, hamad rashid mohamed, ambao wote ni watu wenye ushawishi mkubwa katika siasa za visiwani na bara.

duni ambaye tayari cuf imemteua kuwa mgombea mwenza wa preof ibrahim lipumba, anayebeba kwa mara ya nne bendera ya chama hicho katika kuwania urais, anatajwa kutakiwa na chadema kutokana na ushawishi wake ndani ya siasa za zanzibar na hata bara.

kwa mujibu wa habari hizo, kukubali kwa duni kutategemea zaidi msimamo wa chama chake katika kumuunga mkono dl slaa, hatua ambayo imeelezwa kuanza kujadiliwa katika vikao visivyo rasmi kabla ya kuingia katika vikao rasmi vya vyamna hivyo ili hatimaye kufikia uamuzi.

mwaka 200 chadema walimuunga mkono mgombea urais wa cuf, prof lipumba, ambako katika mikutano yake nchi nzima alisimama kuwapigia debe wagombea wa chadema na cuf huku mitandao ya vyama hivyo ikitumika katika harakati za kampeni hizo, hali ambayo inaelezwa kupendekezwa kuwapo katika katika uchaguzi wa mwaka huu.

kwa upande wa hamad rashid, anatajwa kama ni mtu aliye karibu na dk slaa wakiwa wamefanya kazi kwa muda mrefu bungeni katika ofisi ya kambi ya upinzani, na anatajwa kuwa mmoja wa wanasiasa waliomshawishi mwanasiasa huyo wa chadema kuwania urais.

….habari zaidi katika raia mwema ya leo – mwenye full soft copy yake atuwekee tafadhali.


my take:

this story is too good to be true, though it has certain convincing elements. Can that be possible?


inawezekana ikawa kweli lakini tatizo kubwa ni kwamba cuf ni watu wenye uchu wa madaraka, kwa hivi hawawezi kukubali kufanya hivyo hata siku moja, mfano mzuri ni mwenyekiti wao, wananchi hawamtaki yeye analazimisha kupendwa, kama amekosa maratatu nzima kwanini asiwaachie wenzake kama walivyo fanya mrema, cheyo, mbatia, mbowe naviongozi wengine.. Kwahiyo mi naona bora chadema wajikongoje wenyewe tu na si kutegemea mtu kutoka cuf
 
Kila kitu kina mwanzo na mwisho wake, ccm inamwisho wake wa kutawala kama chama tawala, lakini kabla hatuja wanyang'anya utawala ccm na kuwapa wengine inabidi tuangalie mafanikio na kushindwa kwao,, ili isije tuka wanyang'anya kwa lengo la kujenga bila kuja kwamba tutabomoa zaid,
hii nawapa angalisho tu kwani kila mtu ana weackness, na vyama pia vina weakness kama kunachama kinaudini, kunachama kina ukabila ingawa havijioneshi lakini utaona hata makao makuu ya wilaya yapo katika office za bakwata.. Hii inakishushia chama uaminifu tunabadilike ili tuwe kidemocrasia zaidi,, siyo tujitege kusubiri raisi akosee ili na sisi tupate cha kuongea,, au ukiona watu hawajakusikia muda mrefu unatangaza maandamano si tabia mzuri kwa wasomi.
 
HIVI HUYO LIPUMBA ANAJUA MAANA YA HAKI SAWA KWA WOTE? KWASABABU NASHANGAA YEYE AMENG'ANG'ANIA KUGOMBEA MARATATU ANGEKUWA ANAJUA MAANA YA HAKI SAWA ANGETOA NAFASI YA KUGOMBEA KWA WENGINE PIA KUPITIA CUF, SASA ANAPOTEZA VITI VINGINE UCHAGUZI HUU,, MUTANIKUBALIA UCHAGUZI UKIISHA..:A S-heart-2:
 
Hakuna duni wala hamadi ,ila kama watapenda kuhamia huko sawa ,nawahamie kwani CUF kuna watu wanatamani wengine waondoke ili washike usukani ,ivi yule hiza kapita ,shaibu kapita ,rwakatware nae kapata kugombea ubunge uko Bukobaa.
Wacha tuweke sawa pale Zanzibar afu tunakuja kumaliza kazi huku Tanganyika ,maana hatuna mambo ya chadema kulipua mabomu yasiokuwa na faida ivi yale mabomu mliokuwa mkilipuwa yamemjeruhi nani ,kitachowafanya WaTz kuona kuwa kweli yamelipuka na kujeruhi !!:rapture: Bye Chadema
 
Hawa Chadema wameshindwa kuuza sera zao za kikabila na zakidini wanataka kutumia majina makubwa ambayo walishwa established na CUF ??

Shame on you chadema, Tunataka viongozi wenye sera zisizo za kikabika nakidini. Watanzania kamwe hawatomruhusu kilaza kama Mbowe na Mchungaji kama Slaa kuongoza watanzania wasiokuwa na udini wala ukabila
 
Back
Top Bottom