RAIA MWEMA: CHADEMA kwafukuta

Lissu lazima agombee urais 2025 hata kama CHADEMA wakitangaza kujitoa kwa sababu yoyote ile. Kugombea urais kwa Lissu ni mradi wenye tija sana hata akiwa na uhakika kuwa hatashinda.

Mbona unalazimisha Lissu agombee. Msimamo wa chama ni bila Katiba Mpya chadema haishiriki uchaguzi. Kumbuka Lissu ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA.
 
Huwaamini gazeti la raia mwema?
 
Lissu lazima agombee urais 2025 hata kama CHADEMA wakitangaza kujitoa kwa sababu yoyote ile. Kugombea urais kwa Lissu ni mradi wenye tija sana hata akiwa na uhakika kuwa hatashinda.
Kugombea urais kwa Lissu ni mradi wenye tija kwake? how?
 
Hapo ndio utajua kwamba tunacwanasiasa maslahi waliopitiliza nchi hii!
Yeyote anayetaka maslahi kupitia siasa, anaenda CCM. Huko ndiko watu wanagawana madaraka na pesa.

Maslahi kwenye upinzani yatatoka wapi? Huko unatakiwa ujiandae kupoteza pesa, biashara na hata ajira, kama ni mwajiriwa wa Serikali.
 
Sasa hivi mamilioni ya Mbowe hayahitajiki kwa Tundu Lissu, tayari amepata kamradi kake pale Ubeljiji amabacho kinamuingizia pesa ya kutosha. Kumbuka hata ile helikopta aliyotumia kwenye uchaguzi 2020 haikutokana na pesa za CHADEMA.
Aanzishe chama chake kama Zitto alivyofanya vinginevyo sijui
 
Ungetuletea habari kamili ingependeza zaidi, lakini kutuwekea kichwa cha habari pekee umetuacha tufanye kazi ya kubahatisha..
Kwa nn unapenda sana kutafuniwa? Alafu kuhusu huo mpasuko mbona nimeshaleta sana humu, tafuta nyuzi za nyuma alafu Soma utaelewa
 
Migogoro ya kutengeneza kwa maslahi ya chama Tawala kama sehemu ya maridhiano ili serikali ya umoja wa kitaifa ipatikane 2025!!


Fikra huru

Cha msingi Tanzania isonge mbele!
 
Hili gazeti limelambishwa asali. Nimeona kwenye toleo la leo wakisema ongezeko la faida kwenye mabenki ni sababu ya kazi ya Samia, really?
 
Inakuwaga hivyo hivyo bwashee!
Bwashee, naona kwa sasa tushughulikie kauli ya mwenyekiti wetu wa CCM kwamba wananchi wanababikiziwa kesi za madawa ya kulevya na Mapolice wetu ambao walioapa kulinda usalama wa raia na mali zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…