Raia Mwema: Akina Masogange kuachiwa

Raia Mwema: Akina Masogange kuachiwa

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
‘UNGA' AFRIKA KUSINI

Akina Masogange kuachiwa


Ezekiel Kamwaga Toleo la 316 18 Sep 2013



316_madawa.jpg


WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa, Raia Mwema limeambiwa.


Ingawa ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo katika kundi la dawa za kulevya.

Watanzania hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 6.8.

Hata hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors) yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.

"Kusema kweli nguvu ya kesi ya akina Masogange imepungua sana mara baada ya kubainika aina ya dawa walizokuwa nazo. Kama zingekuwa ni dawa za kulevya, mambo yangekuwa mengine lakini kwa haya waliyokamatwa nayo, sidhani kama kuna kesi ngumu sana. Nataraji watapewa dhamana wakati wowote kutoka sasa," kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili ndani ya Jeshi la Polisi. Masogange na mwenzake wanashikiliwa nchini Afrika Kusini tangu Julai, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Sheria ya Dawa za Kulevya ibara ya 26 (1) a na b, dawa zinazotambulika kama za kulevya hapa nchini ni kama vile Cocaine, Heroin, Mandrax, Bangi, mirungi na nyingine lakini ephedrine haimo katika kundi la dawa za kulevya.

Ni sheria hiyo ambayo imetamka wazi kwamba mtu anayekamatwa na dawa hizo zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 haruhusiwi kupewa dhamana lakini zikipungua thamani hiyo, anaweza kupewa dhamana.

Vyanzo vya Raia Mwema vimebainisha kwamba kwa vile Ephedrine si dawa za kulevya kwa mujibu wa sheria zilizopo, watuhumiwa hao wanaweza kupewa dhamana.

Kwa mujibu wa mwongozo wa wadau wa mapambano dhidi ya Dawa ya Kulevya uliotolewa mwaka 2011, uingizwaji na matumizi ya dawa kama hizo zinazofahamika kwa jina la vibashirifu, unatawaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

Gazeti hili lilipiga hodi katika ofisi za TFDA jijini Dar es Salaam ambako lilielezwa kwamba vibashirifu huingizwa nchini kwa utaratibu maalumu kulingana na mahitaji ya kitaifa yaliyopo.
"Unapozungumzia vibashirifu, unazungumzia mambo ya kitaalamu. Nitakupa mfano, kuna mmea unaitwa Coca. Mmea huu unatengeneza dawa za kulevya zinazofahamika kwa jina la cocaine lakini ni mmea huo huo ndiyo unatengeneza soda ya Cocacola ambayo karibu kila mtu anatumia.

"Mtu anaweza kutumia Ephedrine kutibu magonjwa kama vile mafua lakini anaweza kuitumia pia kama dawa za kulevya. Unajua baadhi ya dawa zilizo kwenye kundi la dawa za kulevya zinatumika pia hadi kwenye hospitali mbalimbali lakini kwa shughuli na kiwango maalumu.

"Mtu akitaka kuagiza dawa hizo ni lazima apate kibali kutoka kwetu. Tukizikamata kwa mtu ambaye hana kibali tunaziteketeza. Hiyo ndiyo adhabu ya kwanza lakini kama kutaonekana kulikuwapo na nia ya uhalifu, basi mkono wa sheria utachukua mkondo wake, alisema mmoja wa maofisa waandamizi wa TFDA aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa kuwa si msemaji rasmi wa mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, matumizi ya Ephedrine yalianza nchini China miaka zaidi ya 200 Kabla ya Kristo na inapatikana sana katika mmea wa Ma Huang ambao unatumika kutibu magonjwa mbalimbali katika tiba za Kichina.

Mwaka 1994, aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Argentina, Diego Maradona, aliondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia nchini Marekani na baadaye kufungiwa kucheza soka baada ya kukutwa na hatia ya kutumia Ephedrine ambayo ni miongoni mwa dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Raia Mwema limekosa taarifa za kwa nini vyombo vyote vya habari vya Afrika Kusini viliripoti kwamba dawa walizokutwa nazo zilikuwa ni Methamphetamine lakini sasa taarifa mpya zinataja kuwa ni Ephedrine.

Hata hivyo, nyaraka tofauti ambazo gazeti hili limezipata zinaonyesha kwamba Ephedrine na Methamphetamine zinafanana kila kitu tangu kwenye muundo wa molekyuli (chembe) zake isipokuwa Ephedrine ina kitu kinachoitwa Hydroxil ambacho hakipo kwenye Methamphetamine.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu taarifa hizi mpya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema anafahamu kuhusu hilo lakini wao wanaendelea na upelelezi wao kuhusu watu waliowatuma akina dada hao kupeleka dawa hizo nchini Afrika Kusini.

"Haya mambo yanafanyika huko Afrika Kusini na sisi hatuwezi kuingilia labda kama wakitaka kitu kutoka kwetu. Cha msingi kwetu ni kwamba dawa hizo zilitoka kwetu na wasichana wale hawana uwezo wa kuwa na mzigo wenye thamani ile. Tunawatafuta wahusika na tukipata taarifa tutawapa," alisema Nzowa ambaye anatajwa kujijengea heshima kubwa kwenye vita hii dhidi ya dawa ya kulevya.

========

Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya
Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu
Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka
Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange
Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu
Kesi kusikilizwa
Tetesi za kuachiwa huru
Hukumu
 
kilo 150 za Ephedrine zenye thamani ya Tsh Bil 6.8.........¤¤¤¤¤¤¤
wonder shall never end"
 
kweli hii ndio tanzania,,,HAKUNA KINACHOSHINDIKANA,,,

SINA LADHIADA ZAIDI YAKUSEMA ,,,,VIBASHIRIFU NDIO HABARI YA MUJINI,,,,,
 
kilo 150/6.8 Bil= million 22.06 per kilo of ephedrine.
simple drugs for illnesses with such cost

hayo ndio maajabu bana kilo zote hizo na gharama zake hizo na bado tunaambiwa sio mzigo bana
hii ni Tanzania zaidi ya uijuavyo
na Lukuvi alifunga safari kufuatilia kesi hii na mzigo huu
ndo maana wamekuja na taarifa hii baada ya juhudi za Nzowa na Lukuvi na wengineo
 
nikikaa na kutafakari kuhusu hii habari yakina masogange,,,naona kama ni tamthilia ya
[h=3]walang hanggan (my eternal),,,,kumbe zile jitahada zote walizotumia kina masogange na mtandao wao kupita (jnia),,,ni kwa ajili ya vibashirifu,,,vya kutengenezea dawa za kifua,,,,kesi lazima iwe nyepesi....[/h]
 
demu anamegwa na wakubwa wa magamba,kuna safari ya ghafla mkuu wa kaya aliifanya ssouth africa juzi kati,tuombe asiwe ametoa mgodi wa dhahabu ili waachiwe.
 
Mzigo ulibadilishwa kwa safari ya kutoka Tunduma hadi Mbeya itakuwa South Afrika bana!!!!!!! tena walikosea wangeweka tu unga wa ngano ili kuonyesha walikuwa wanapeleka kwa wenyeji wao huko south kwa ajili ya kupikia chapatti!!!!baaaaaaaasi!!!!!!
 
Ndo maana huwa cfuatilii makesi ya madawa ya kulevya maana yote huwa ni tamthilia tu.hawa watu huwa naskia mitandao yao inanguvu kuliko hata serkal zetu.sasa ndo naamini.mara hii imegeuka na kuwa walibeba piliton tu..iba kuku uone.ila sembe ukipata mchongo piga tu.coz hufungwi
 
Hawa wanatakiwa wakirudi wapelekwe uwanja wa taifa tuwazomeeeee mpaka basi
 
demu anamegwa na wakubwa wa magamba,kuna safari ya ghafla mkuu wa kaya aliifanya ssouth africa juzi kati,tuombe asiwe ametoa mgodi wa dhahabu ili waachiwe.

mkuu migodi imekwisha sasa anagawa miji mizima mizima, mito, maziwa, milima n.k
hapo ndio shida inapoanzia na sisi wananchi kuhusika, maana akigawa dar-es-salaam kwa kuwatoa jamaa zake hasara kwetu sisi.
 
Back
Top Bottom