Rai ya Alphonce Mawazo kwa wana CHADEMA

Mbona mnataka Jasho la Zitto, ambalo ndio limekufanya hata wewe uipende CHADEMA lidondoke bure? wanafiki wakubwa nyie!


Chadema Mwanza yampiga ‘stop’ Zitto


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Ziwa kimesema hakitaki kumuona Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kwa kuwa ni msaliti.

Pia kimewatahadharisha viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa kwamba yeyote atakayeonekana kuwa karibu na Zitto katika shughuli za chama au kutoa siri, atashughulikia haraka na kuwekwa kwenye kundi la wasaliti.

Akizungumza jijini hapa jana, Kiongozi wa Operesheni Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu, alisema kuwa wanaunga mkono kwa asilimia 100 uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema wa kuwavua uanachama Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, huku Zitto akipachikwa jina la ‘Mbunge wa Mahakama’.

Njugu alisema uamuzi huo ni sahihi kwani watu hao watatu waliaminiwa na chama, lakini wakakigeuka na kukisaliti kwa manufaa yao.

“Kwa kitendo alichokifanya, kukisaliti chama na kukipeleka Mahakamani, tunasema hatumtaki kabisa, ingawa ana haki ya kwenda sahemu yoyote na kufanya mkutano lakini tunatoa tahadhari mapema.

“Ikiwa atakuja Mwanza na kujihusisha au kutumia nembo ya chama katika shughuli zake za kisiasa, hapo atakuwa amechokoza nyuki. Hivyo hivyo kwa kiongozi atakayeonekana kuwa karibu au kumpa ushirikiano, atashughulikiwa haraka.

“Zitto hawezi kuwa kikwazo kwa Chadema kufikia malengo yake, tunasema chama hiki hakijabomoka wala kugawanyika makundi yenye mitazamo tofauti, hii ni kama hali ya baba kumwadhibi mtoto wake.

“Tunajua hizi vurugu zinazotokea zinaratibiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Usalama wa Taifa na vyama vingine vya siasa ambavyo vinatishwa na nguvu za Chadema. Lakini tunasema tutafika Ikulu salama,” alisema.

Njugu alisema kitendo cha Zitto kutoa tuhuma kwa viongozi wa Chadema ni dalili ya kuanza kutapatapa kutafuta huruma ya wananchi na Mahakama.

Alisema kama alikuwa anajua viongozi hao wana tuhuma za aina hiyo, angezitoa mapema kabla ya kuibuka yaliyompata.

“Unajua kuna wabunge ambao waliandaliwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe, tangu wakiwa vyuoni akiwamo Zitto. Amefika hapo kwa sababu ya Mwenyekiti sasa anakosa fadhila.

“Wengine ambao Mbowe alikuwa akiwaandaa wakiwa vyuoni ni John Mnyika, Halima Mdee, Ezekiel Wenje na John Mrema ambaye ni kiongozi mkubwa Makao Makuu.

“Mbowe alikuwa akiwafuata vyuoni na kukaa nao baada ya kuona ni vijana wenye mwelekeo wa kuleta mabadiliko na chama kikawaamini na hata kuwapa majimbo. Lakini naona Zito amejisahau.

“Mimi nawaomba viongozi wa kitaifa kutofanya kosa la kumsamehe au kumrejesha ndani ya chama pengine kutokana na uamuzi wa Mahakama. Itakuwa ajabu kweli kweli na wanachama hawataelewa,” alisema.

Wakati huo huo, makundi ya wanachama wa vyama mbalimbali walikusanyika eneo la Kemondo maarufu kama ‘Bunge la Mwanza’ kuzungumzia kinachoendelea ndani ya Chadema.

Eneo hilo ambalo lipo katikati ya jiji likiwa na matawi ya Chadema na CUF, wanachama wengi wa Chadema walipongeza hatua hiyo.

Wanachama hao walikuwa wakisoma magazeti mbalimbali kwa sauti kuhusu Zitto, na kujadiliana ambapo asilimia kubwa walionekana kutoridhishwa na mwenendo wa kada huyo wa Chadema.


Source: Rai
 
Nimeingia jimbo la Kishapu kwa ziara ya siku nne,nawaomba wanachadema kupuuza na kutolipa uzito suala la zito.tuiamini kamati kuu na baraza lake,wengine tutawanyike tukajenge chama.

Tusiingie kwenye mtego wa adui wa mabadiliko yaani CCM,wanachotaka ni zogo hizi kuendelea nasi tupunguze kasi ya kuwashughulikia, acheni kulifanya gumzo vijiweni na badala yake tujadili uundaji wa misingi.

Hakuna haja ya kufadhaika na kuhisi kana kwamba kuna tatizo kweli,HAKUNA TATIZO CHADEMA,nawaomba tena na tena muelekeze nguvu zote vijijini ambako hata Zito hawamjui wao wanajua chadema.

Mkuu Mungu akutangulie pambana mkuu, nashukuru kwa ujumbe murua hata mimi naunga mkono twende tukakijenge chama '' CHADEMA MSINGI'' ndiyo habari ya sasa!
 
Mbona mnataka Jasho la
Zitto, ambalo ndio limekufanya hata wewe uipende CHADEMA lidondoke bure?
wanafiki wakubwa nyie!

Earthmover,rafiki yako ameamua kupita short cut,amekula zaidi ya alichopanda chadema,DHAMBI KUBWA SANA KAFANYA.
 

Chadema Mwanza yampiga ‘stop’ Zitto



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Ziwa
kimesema hakitaki kumuona Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kwa
kuwa ni msaliti.


Pia kimewatahadharisha viongozi wa Chadema Kanda ya Ziwa
kwamba yeyote atakayeonekana kuwa karibu na Zitto katika shughuli za
chama au kutoa siri, atashughulikia haraka na kuwekwa kwenye kundi la
wasaliti.


Akizungumza jijini hapa jana, Kiongozi wa Operesheni Kanda
ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu, alisema kuwa wanaunga mkono kwa
asilimia 100 uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema wa kuwavua uanachama Dk.
Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, huku Zitto akipachikwa jina la ‘Mbunge
wa Mahakama’.

Njugu alisema uamuzi huo ni sahihi kwani watu hao watatu waliaminiwa na
chama, lakini wakakigeuka na kukisaliti kwa manufaa yao.

“Kwa kitendo alichokifanya, kukisaliti chama na kukipeleka Mahakamani,
tunasema hatumtaki kabisa, ingawa ana haki ya kwenda sahemu yoyote na
kufanya mkutano lakini tunatoa tahadhari mapema.

“Ikiwa atakuja Mwanza na kujihusisha au kutumia nembo ya chama katika
shughuli zake za kisiasa, hapo atakuwa amechokoza nyuki. Hivyo hivyo kwa
kiongozi atakayeonekana kuwa karibu au kumpa ushirikiano,
atashughulikiwa haraka.

“Zitto hawezi kuwa kikwazo kwa Chadema kufikia malengo yake, tunasema
chama hiki hakijabomoka wala kugawanyika makundi yenye mitazamo tofauti,
hii ni kama hali ya baba kumwadhibi mtoto wake.

“Tunajua hizi vurugu zinazotokea zinaratibiwa na Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Usalama wa Taifa na vyama vingine vya siasa ambavyo vinatishwa na
nguvu za Chadema. Lakini tunasema tutafika Ikulu salama,” alisema.

Njugu alisema kitendo cha Zitto kutoa tuhuma kwa viongozi wa Chadema ni
dalili ya kuanza kutapatapa kutafuta huruma ya wananchi na Mahakama.

Alisema kama alikuwa anajua viongozi hao wana tuhuma za aina hiyo,
angezitoa mapema kabla ya kuibuka yaliyompata.

“Unajua kuna wabunge ambao waliandaliwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe,
tangu wakiwa vyuoni akiwamo Zitto. Amefika hapo kwa sababu ya Mwenyekiti
sasa anakosa fadhila.

“Wengine ambao Mbowe alikuwa akiwaandaa wakiwa vyuoni ni John Mnyika,
Halima Mdee, Ezekiel Wenje na John Mrema ambaye ni kiongozi mkubwa Makao
Makuu.

“Mbowe alikuwa akiwafuata vyuoni na kukaa nao baada ya kuona ni vijana
wenye mwelekeo wa kuleta mabadiliko na chama kikawaamini na hata kuwapa
majimbo. Lakini naona Zito amejisahau.

“Mimi nawaomba viongozi wa kitaifa kutofanya kosa la kumsamehe au
kumrejesha ndani ya chama pengine kutokana na uamuzi wa Mahakama.
Itakuwa ajabu kweli kweli na wanachama hawataelewa,” alisema.

Wakati huo huo, makundi ya wanachama wa vyama mbalimbali walikusanyika
eneo la Kemondo maarufu kama ‘Bunge la Mwanza’ kuzungumzia
kinachoendelea ndani ya Chadema.

Eneo hilo ambalo lipo katikati ya jiji likiwa na matawi ya Chadema na
CUF, wanachama wengi wa Chadema walipongeza hatua hiyo.

Wanachama hao walikuwa wakisoma magazeti mbalimbali kwa sauti kuhusu
Zitto, na kujadiliana ambapo asilimia kubwa walionekana kutoridhishwa na
mwenendo wa kada huyo wa Chadema.


Source: Rai

Heko,hongereni sana,hakuna kuleta mbwembwe kwenye mapambano.
 
Kamanda hongera kwa kazi kubwa ya ukombozi uifanyayo. Ila kote upitapo wahimize sana kufanya zoezi la chadema ni msingi coz ujenzi wa misingi ni wa muhimu sana kuzidi hata mikutano ya hadhara. Kila la kheri wa ukweli.
 
Nimeingia jimbo la Kishapu kwa ziara ya siku nne,nawaomba wanachadema kupuuza na kutolipa uzito suala la zito.tuiamini kamati kuu na baraza lake,wengine tutawanyike tukajenge chama.

Tusiingie kwenye mtego wa adui wa mabadiliko yaani CCM,wanachotaka ni zogo hizi kuendelea nasi tupunguze kasi ya kuwashughulikia, acheni kulifanya gumzo vijiweni na badala yake tujadili uundaji wa misingi.

Hakuna haja ya kufadhaika na kuhisi kana kwamba kuna tatizo kweli,HAKUNA TATIZO CHADEMA,nawaomba tena na tena muelekeze nguvu zote vijijini ambako hata Zito hawamjui wao wanajua chadema.[/:thumbup:
 
Back
Top Bottom