Mwanapropaganda
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 4,235
- 2,505
Kilichonifanya kutaka sherehe hizi zipigwe marufuku ni namna wahusika wanavyosheherekea bila kujali nani yupo hapo, wanawake wanavua nguo kabisa na kuacha matiti wazi mbele ya watoto wadogo bila kujali madhara yake kisaikolojia. Video za vigodoro zinazagaa mitaani zikionesha watoto wadogo wajishuhudia watu wazima wakicheza muziki wakiwa uchi.
Naweza kusema kwamba vigodoro ni moja ya visababishi vya mmomonyoko wa kimaadili na kuchochea ngono zisizotarajiwa kitu ambacho kinapelekea kuongezeka kwa maambukizi ya vvu.
Sababu nyingine ni kwamba, vigodoro hivyo vimekuwa kero hasa kwa kupiga muziki wa sauti ya juu usiku kucha kitu ambacho huonekana ni kuingilia uhuru binafdi wa watu waishio karibu na tukio linapofanyika.
Wizara inayohusika nautamaduni naomba mlitazame suala hilo, likapigwa vita kama tohara za kimila ambazo zinasemwa huchangia kuenea kwa maambukizi ya vvu kwa sababu ya hali ya mambo imebadilika, hivyo wakati wa sasa sio sawa na hapo kabla ambapo watu walikuwa wa kabila moja na wenye itikadi zinazofanana. Kwa sasa sherehe ya vigodoro ni jambo lililopitwa na wakati kwa sababu jamii za mijini zimechanganyika, hivyo wasisababishe kero kubwa kwa watu wasiohusika na tukio hilo.
Hakuna kabila lolote nchini Tanzania lililo na utamaduni ambapo watu huonesha nyuchi zao kama burudani mbele ya kadamnasi/hadhira.