RAI - Nguvu ya Hoja?

Kichwangumu,
Ahsante sana kwa mchango wako.
Lakini usijifanye kuwa umevaa miwani ya mbao na kuziba masikio. Kama kweli hujui kuwa Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) ndiye mmiliki wa Tanzania Daima, basi unaangukia kule kwa wahenga walikosema kuwa 'usilolijua litakusumbua' ... 'usilolijua ni sawa na usiku wa giza'
Kwahiyo kaa chini tafakari, fanya upembuzi then utapa mwelekeo!

Pundamilia07,

Asante sana.

Hakimu kunijua mimi kuwa ni mwizi hakumfanyi asisikilize ushahidi na utetezi. Kujua kuwa Rostam na Freeman wana fedha ya kutosha na wamiliki wa magazeti hakunifanyi mimi niache kusahau na kujadili matatizo ya mtanzania.

Asante tena
 
Sijakupata vizuri mkuu, hebu fafanua.
 
Sijakupata vizuri mkuu, hebu fafanua.

Kaka,

Tuwe Objective, tusitafute excuse za matatizo yetu au hali fulani ya mtu isikudrive kuamua tofauti na nia yako. Kumbuka tupo kwenye JF, JUKWAA SIASA NA SIO VINGINEVYO. Sidhani kama pesa ya Lowassa, Manji, Rostam, Ndesa, Freeman, Pundamilia, Dr. Slaa, Kichwangumu ni tatizo la mtanzania.

Labda tuangalie ni jinsi gani alizipata. ni halali au? Hapa ndio tunapigania kufuta ufisadi kwa njia yeyote kama walitumia kodi yetu na sie kama mtaji.

Kama wana common interest katika biashara hilo sio tatizo kuungana. Common interest is needed in this battle not individuals kama unavyotaka niamini. Kama pesa yake na biashara zake zinasaidia wafamilia yake sina tatizo na sio kusaidia au kukopesha CCM na CHADEMA based on personal interest. Huu ni utumwa mwingine tunatengeneza wa kushindwa kujitawala hata kimawazo kama akina Bibile

Hope umenipata
 
Hebu labda nijaribu kuuliza swali la moja kwa moja huenda tunaweza kuwa sawa na kwenda pamoja.

Je, unafahamu kuwa Freeman ndiye mmiliki wa Tanzania Daima?
 
Mkamap,

Hata Mengi alishasema kuwa wao wanatoa tu policy kwenye Kulikoni na Thisday na sio kuandika.

Kwi kwi kwi yaani wewe katika watu mashuhuri unaowaamini wakiongea Mengi ni mmojawapo? Mbona hakuna gazeti lake hata moja ambalo huwa linaandika skendo zake (Chukua mfano ile ya Mdogo wake na Waingereza)? Mbona thisday na kulikoni ndiyo yaliyoshikia bango issue ya Manji wakati ule wana ugomvi na Mengi? (hapa sina maana kwamba wasifichue ufisadi lakini ni kwanini washikie bango wale wagomvi wa Mengi tu?).

Ni ukweli usio kificho kuwa Media ya Tanzania inawatumikia hao mabwana zao (wamiliki wao). Nakwambia ukisoma gazeti kama kuna skendo ina mhusu RA, basi unasoma T/Daima kwanza halafu unaangalia Mtanzania/Rai wanamtetea vipi. Unaweza ukakuta kimya. Au wanaweza wakatoa mazuri peke yake. Hivyo hivyo kama kuna skendo ya Mbowe unaikuta kwenye Mtanzania/Rai, basi unaangalia T/Daima ili kuona wanamtetea vipi au wameandika mazuri gani. Hivyo media Tanzania haiko balanced kabisa. Ukisikia kuna skendo inamhusu mtu hasa hawa matajiri basi unaweza kabisa kubuni ni gazeti litakuwa limeandika hiyo story.

Kwa hiyo kujifanya kushangaa Rai wanapowashambulia T/Daima ni unafiki wa sisi wenyewe. Maana huo ndiyo umekuwa mtindo wa magazeti yetu au media zetu. Yaani inakera sana kwa sisi wasomaji au watazamaji. Unaona kabisa vyombo vya habari vimekuwa midomo ya wafanyabiashara/wanasiasa/wenye madaraka serikalini.
 
Mkodoleaji,

Hakika umekodoa hasa na kama Kichwangumu hajaelewa, basi aendelee kuuliza ili tumtoe gizani au asiendelee kusumbuka tena. What you narrated in your last posting is the hard fact.
 
mhariri wa TZ daima na balile wote ni makanjanja tu!Balile anawatumikia kina RA na kikosi chake na wa TZ daima anawatumikia kina Mbowe na kikosi chake!1+1=1
Wote wale wale!

Kwa Wakuu wote JF!

kinachonifurahisha mimi ni kuwa wote tunaelewa kusoma nyakati. hatupati shida kugundua ukweli wa mambo hata kama umefichwa.

big up wote wenye moyo wa dhati wa kulifikisha taifa hili teule la TZ ktk nchi ya "ahadi" tuliyoahidiwa na Mwalimu yenye maziwa na asali
 
Habari zinazoingia sasa hivi zinadokeza kuwa Mhariri wa gazeti la RAI Bw. Balile ameondolewa wadhifa wake huo. More to come!
 
Balile ni mtu wa ajabu sana alikuwa anakula pesa za membe at the same time HADEMA nako alikuwa anakula

says alot about the mans character

huyu ndiye balile:

Deodatus Balile

pic_balile.jpg

NIKIWA na matumaini chungu wa tele kuwa mpendwa msomaji wangu hujambo, leo nimeona ni vyema nitupie macho sekta mpya inayoibukia hapo nchini kwetu, ambayo kimsingi ni fursa na ufunguo wa kukuza uchumi wetu.

Sekta hii ni tawi jipya la huduma katika usuluhishi wa migogoro (conflict resolution).

Nikijaribu kuangaza katika mitandao mbalimbali, kwa sasa jina la Tanzania linakuja juu kwa kiwango cha kutisha katika sekta hii ya usuluhishi wa migogoro. Yapo mataifa magwiji kama Uswisi, yenye kuaminika kuwa ni eneo salama kwa mazungumzo na mikataba mizito, na ndiyo maana leo ukiangalia mikutano inayofanyika Geneva, Uswisi, ni mingi kuliko maelezo.

Geneva imekuwa nyumbani kwa mikataba mingi ya kimataifa, kuanzia sekta ya diplomasia, uchumi (ikiwamo Shirika la Biashara la Kimataifa – WTO), biashara na usuluhishi. Kwa bahati mbaya nchi hii haina maliasili kwa kiwango kikubwa. Viongozi wa taifa hili walilifahamu hilo na kuamua kuwekeza katika huduma. Uchumi wa Uswisi unategemea au unajiendesha kutokana na mapato yatokanayo na sekta huduma kwa asilimia 98.

Taifa hili lina benki kubwa na zenye fedha nyingi kuliko mataifa karibu yote duniani na lilijiingiza katika biashara ya usiri wa kumbukumbu za fedha, ambapo viongozi wengi wa dunia hii hupora fedha katika mataifa yao na kuzihifadhi Uswisi. Nieleweke hapa, sisemi kuhifadhi fedha za wahalifu ni mchezo mzuri, lakini nataka kujenga hoja yenye kuonyesha walivyojipanga kuhakikisha sekta ya huduma inakuwa nguzo ya uchumi wao.

Taifa kama Uingereza ambalo ni visiwa vidogo vyenye ukubwa sawa na mkoa kama wa Morogoro vikichanganywa, lina uchumi mkubwa ajabu. Taifa hili la Uingereza limewekeza katika sekta ya huduma. Kama Uswisi, nao mikataba mikubwa mingi hutiwa saini hapa. Leo ukitafuta kampuni kubwa 10 za masuala ya uhasibu, zote zina makao makuu hapa London.

Kati ya kampuni 10 kubwa za masuala ya kisheria duniani, 6 zipo hapa Uingereza, tatu zipo Marekani na moja ina makao makuu ya umiliki wake Uholanzi na Uingereza (kwa wakati mmoja).

Hali ni hivyo katika uhandisi, ugavi, mawasiliano na sekta nyingine nyingi. Waingereza wamejielekeza katika huduma. Kwa Marekani shughuli kama hizo zinazohusu mikutano mbalimbali ya kimataifa na huduma nyingine zikiwamo za kifedha, kisheria na fani nyingine, zinaendesha uchumi wa taifa hilo kwa asilimia 63 sasa.

Mataifa haya sasa yanafunga viwanda na kuvihamishia India na China, huku yenyewe yakibaki kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa.

Nimeyasema haya, yanisaidie kujenga hoja juu ya fursa tuliyonayo Watanzania katika usuluhishi wa migogoro ya kimataifa. Kazi anayoifanya Dk. Salim Ahmed Salim, ya kusuluhisha mgogoro wa Darfur, nchini Sudan, inalitangaza taifa letu kwa kiwango cha ajabu.

Habari nyingi zinazochapishwa zinaitaja Arusha kama kituo cha usuluhishi wa migogoro kilichobobea, ambapo wanarejea mgogoro wa Burundi na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari iliyopo Arusha. Leo mataifa mbalimbali yameanza kuamini kuwa ikiwa Afrika Kusini, inayoonekana kuwa mshindani mkubwa wa Tanzania katika sekta hii ya usuluhishi ikishindwa kusuluhisha mgogoro wa Zimbabwe, basi ikabidhiwe Tanzania, itauweza.

Imani hii kwa taifa letu, ni nguzo kubwa na chimbuko la maendeleo. Kwa nchi zinazotokea kupata fursa kama hizo, huo ndiyo mwanzo wa kutimua vumbi kuelekea mji wa maendeleo.

Najua yapo mataifa mengi yangependa kupata fursa hii ila kutokana na misingi fasaha aliyoijenga muasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, taifa letu linayo fursa ya ziada; amani, utulivu na utengamano wa kisiasa.

Kimsingi kazi ya usuluhishi wa migogoro ni biashara kubwa. Nasema ni biashara kwa misingi kuwa watu wetu watakaokuwa wanafanya kazi katika mabaraza au mahakama za usuluhishi, ni wazi watakuwa hawajitolei. Hawa watakuwa wanalipwa, kumbi za mikutano na hoteli wanapolala wahusika wakati wa mikutano vinalipiwa, bila kutaja chakula na matumizi ya ziada wanayofanya washiriki wa mikutano hii wanapokuwa hapo nchini.

Hata hivyo, lipo jambo moja linalonitia wasiwasi kwa sasa. Jambo hili ni umahiri wa watu wetu hasa katika fani hii ya usuluhishi wa migogoro.

Kipo kizazi kilichofanya kazi Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miongo kadhaa na kupitia uzoefu au shule walizopata wakapata utalaamu unaotumika kushawishi na hatimaye kutatua migogoro hii.

Kinachonitia wasiwasi na kunilazimu kumtahadharisha waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwa fursa hii tunaweza kuipoteza sioni mipango thabiti ya kuandaa vijana wapya wa kuendeleza taaluma hii ya usuluhishi. Conflict Resolution ni fani maalumu inayokuja juu kwa kasi kubwa duniani na watu wanaisomea kuanzia shahada ya kwanza hadi ya uzamivu, ila sijaona mpango-mkakati wa kuhakikisha Tanzania inakuwa na wataalamu wa kutosha katika nyanja hii.

Kwa kuwa wizara hii iliyopo chini ya Membe inayo dhamana ya usuluhishi wa migogoro, nimsihi aliangalie suala hili na kujaribu kutafuta hata vyanzo mbadala vya mapato, vijana wetu wanaoibukia wenye umri wa miaka 19 hadi 30, wapelekwe shule katika fani hii tuwe na wataalamu wa kutosha.

Napendekeza umri huu kwa sababu hawa wakipata utalaamu kwa umri wao wataweza kulitumikia taifa kwa miaka 30 na zaidi, badala ya kupeleka shule kwa kiwango cha uzamivu mtu mwenye miaka 48, akirejea kutoka masomoni anatumikia miaka minne anastaafu kwa hiari au anaongeza miaka mitano na kulazimika kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Itakuwa ni aibu kwa taifa letu kuwa na sifa ya usuluhishi wa migogoro, lakini watendaji wa mabaraza au mahakama husika wanatoka mataifa mengine na hakuna Watanzania wenye kufanya kazi hii.

Chonde chonde Membe lifikirie hili, na ikiwezekana ulitafutie ufumbuzi. Tukisuasua, fursa hii tutaipoteza. Mungu Ibariki Tanzania.

deobalile@yahoo.com – 0007904159144

IMGP0224.jpg

nami nikamjibu balile hivi:

Ok sasa nadhani ni wakati muafaka kwangu kujadili hoja za bwana Balile

NIKIWA na matumaini chungu wa tele kuwa mpendwa msomaji wangu hujambo, leo nimeona ni vyema nitupie macho sekta mpya inayoibukia hapo nchini kwetu, ambayo kimsingi ni fursa na ufunguo wa kukuza uchumi wetu

Balile, hujaonyesha umefikia vipi conclusion kuwa conflict resolution ni sekta mpya inayoibuka nchini kwetu hebu fafanua zaidi.Kwani kwa upande wangu sidhani kama ni sekta mpya kwa nchi kama Tanzania ambayo imekuwa imekuwa ikimediate tangu tulipopata uhuru na mpaka leo hii inaendelea. Na kama ilivyo International Relations, conflict resoluton inaevolve tuu na tunaona roles za Non-State actors zikiwa zinatiliwa mkazo zaidi kutokana na wao kuwa na know how zaidi katika speciality fulani fulani...lakini unayo fursa ya kufafanua.

Sekta hii ni tawi jipya la huduma katika usuluhishi wa migogoro (conflict resolution). Nikijaribu kuangaza katika mitandao mbalimbali, kwa sasa jina la Tanzania linakuja juu kwa kiwango cha kutisha katika sekta hii ya usuluhishi wa migogoro. Yapo mataifa magwiji kama Uswisi, yenye kuaminika kuwa ni eneo salama kwa mazungumzo na mikataba mizito, na ndiyo maana leo ukiangalia mikutano inayofanyika Geneva, Uswisi, ni mingi kuliko maelezo. Geneva imekuwa nyumbani kwa mikataba mingi ya kimataifa, kuanzia sekta ya diplomasia, uchumi (ikiwamo Shirika la Biashara la Kimataifa – WTO), biashara na usuluhishi. Kwa bahati mbaya nchi hii haina maliasili kwa kiwango kikubwa. Viongozi wa taifa hili walilifahamu hilo na kuamua kuwekeza katika huduma. Uchumi wa Uswisi unategemea au unajiendesha kutokana na mapato yatokanayo na sekta huduma kwa asilimia 98.

Yah, ni kweli mji wa Geneva umekuwa ukiplay a very huge role kama sehemu ya kusaini mikataba mbali mbali ya kimataifa lakini jambo ambalo ni la muhimu zaidi ni kuwa umesahau kufahamisha watu kuwa moja kati ya sababu kuu ya Geneva kuwa na status hiyo ni kihistoria Geneva ilikuwa makao makuu ya League of Nations pale Palais Wilson kabla ya kuhamishiwa Palais des Nations na vile vile wao kuwa neutral wakati wa World War 2 ilipelekea kuwa favourite destination ya mayahudi wengi ambao walikua walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha na assets mbali mbali walikuwa wanauliwa katika nchi zingine za Ulaya na Uswisi pamoja na United States ndizo zilikuwa kimbilio lao of course secret banking system ya Uswisi ilikuwa inawahakikishia amana zao so in a way uko sawa ila ulitakiwa ufafanue zaidi role ya League of Nations and impact ya WW2 ambayo imeifanya uswisi kuwa ilivyo leo not only Geneva lakini miji kama Zurich na Berne.

Taifa hili lina benki kubwa na zenye fedha nyingi kuliko mataifa karibu yote duniani

Naomba kupingana na wewe kwenye hili na hata sijui data umezitoa wapi lakini naweka kukufahamisha kuwa hoja yako hapo juu iko very simplistic kwani hujafafanua au kuweka wazi..sasa naweza kukuweka sawa kwa kukupa data zifuatazo:

Top 4 Banking groups in the world ambazo ziko ranked by Shareholder equity ni:
CITI GROUP-United States
JP MORGAN-United States
BANK OF AMERICA-United States
HSBC-United Kingdom

Top 4 Banks in the world ambazo ranked by market capitalisation ni:

1 CITY GROUP- United States
2 ICBS-China China ICBC
3 BANK OF AMERICA- United States
4 HSBC- United Kingdom

Top 4 bank holding companies in the world ambazo ziko ranked by profit ni:

1 CITYGROUP- United States Citigroup
2 BANK OF AMERICA- United States Bank of America
3 HSBC- United Kingdom HSBC
4 JP MORGAN CHASE - United States

Bwana balile source ya data zangu ni hii hapa:

EURO MONEY: http://www.euromoney.com/page.asp?PageID=2050
ECONOMIST: http://www.economist.com/surveys/displaystory.cfm?story_id=6908408

na lilijiingiza katika biashara ya usiri wa kumbukumbu za fedha, ambapo viongozi wengi wa dunia hii hupora fedha katika mataifa yao na kuzihifadhi Uswisi. Nieleweke hapa, sisemi kuhifadhi fedha za wahalifu ni mchezo mzuri, lakini nataka kujenga hoja yenye kuonyesha walivyojipanga kuhakikisha sekta ya huduma inakuwa nguzo ya uchumi wao.

sawa basi nami nitaendelea kusoma hoja yako ambayo umendelea kwa kusema hivi:

Taifa kama Uingereza ambalo ni visiwa vidogo vyenye ukubwa sawa na mkoa kama wa Morogoro vikichanganywa, lina uchumi mkubwa ajabu. Taifa hili la Uingereza limewekeza katika sekta ya huduma. Kama Uswisi, nao mikataba mikubwa mingi hutiwa saini hapa. Leo ukitafuta kampuni kubwa 10 za masuala ya uhasibu, zote zina makao makuu hapa London.

sawa sasa naomba source ya hii hoja

Kati ya kampuni 10 kubwa za masuala ya kisheria duniani, 6 zipo hapa Uingereza, tatu zipo Marekani na moja ina makao makuu ya umiliki wake Uholanzi na Uingereza (kwa wakati mmoja).

I beg to diiffer bwana Balile zijui unatumia data za mwaka gani na umefikia conclusion hii kivipi lakini naweza kukupa listi ambayo ni sawa na utaona katika top 10 UK ina law forms 3 tu .

CLIFFORD CHANCE- UK
LINKLATERS-UK
SKADDEN,ARPS,SLATE,MEAGHER & FLOM -USA
FRESFIELS BRUCKHAUS DERRINGER-UK
LATHAM &WATKINS-USA
BAKER McKENZIE-USA
ALLEN & OVERY-UK
JONES DAY-USA
SIDLEY AUSTIN-USA
WHITE &CASE-USA

source yangu bwana Balile ni hii:http://www.thelawyer.com/global100/

Hali ni hivyo katika uhandisi, ugavi, mawasiliano na sekta nyingine nyingi. Waingereza wamejielekeza katika huduma. Kwa Marekani shughuli kama hizo zinazohusu mikutano mbalimbali ya kimataifa na huduma nyingine zikiwamo za kifedha, kisheria na fani nyingine, zinaendesha uchumi wa taifa hilo kwa asilimia 63 sasa.

Naomba utoe source ya namna ulivyofikia conclusion hii je hiyo 63% ni UK au USA?

Mataifa haya sasa yanafunga viwanda na kuvihamishia India na China, huku yenyewe yakibaki kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa.

Blame it on Milton Keynes, Adam smith and Milton Friedman...au tuseme ni Laissez-faire economics ...GLOBALIZATION

Nimeyasema haya, yanisaidie kujenga hoja juu ya fursa tuliyonayo Watanzania katika usuluhishi wa migogoro ya kimataifa. Kazi anayoifanya Dk. Salim Ahmed Salim, ya kusuluhisha mgogoro wa Darfur, nchini Sudan, inalitangaza taifa letu kwa kiwango cha ajabu.

Kwa vipi? inatusaidia nini? Je salim alipokuwa kule OAU tulifaidika na nini? argument yako iko shallow hapo hebu fafa nua zaidi

Habari nyingi zinazochapishwa zinaitaja Arusha kama kituo cha usuluhishi wa migogoro kilichobobea, ambapo wanarejea mgogoro wa Burundi na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari iliyopo Arusha. Leo mataifa mbalimbali yameanza kuamini kuwa ikiwa Afrika Kusini, inayoonekana kuwa mshindani mkubwa wa Tanzania katika sekta hii ya usuluhishi ikishindwa kusuluhisha mgogoro wa Zimbabwe, basi ikabidhiwe Tanzania, itauweza.

Jibu la hili ni kuwa kuwa msuluhishi kunahitaji fedha na je unajua tunapewa kiasi gani kuwa wasuluhishi wa migogoro hii? Je unajua kuwa wasuluhishi kumetitia umasikini kwa kiasi gani? kama serikali yetu haipati pesa za kutosha ili kufanikisha hii mikutano je unategemea sisi tutafanya miracle gani? Sisi kwa sasa kusuluhisha migogoro hii ya Great Lakes region ni sawa kwani matatizo yanayoendelea huko huwa yana spill kwetu hivyo its in our interest kufanya hivyo na kama kutangaza nchi then hilo ni jukumu la wizara ya Utalii ana akina Mwenguo. Uchumi wa South Africa unawaruhusu na hizo gharama kwao si tatizo. Je unahabari kama kuna proposal kuwa watanzania waishio nje watatozwa pesa za kuendesha balozi zetu kutokana na budget restrains? sasa hebu tupe data ni kiasi gani kinatumika kwa mwaka katika masuala haya ya conflict kama hiyo ya burundi na sisi pesa tunatoa wapi?? Je EU au UN wanatupa kiasi gani?

Imani hii kwa taifa letu, ni nguzo kubwa na chimbuko la maendeleo. Kwa nchi zinazotokea kupata fursa kama hizo, huo ndiyo mwanzo wa kutimua vumbi kuelekea mji wa maendeleo.

sawa

Najua yapo mataifa mengi yangependa kupata fursa hii ila kutokana na misingi fasaha aliyoijenga muasisi wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, taifa letu linayo fursa ya ziada; amani, utulivu na utengamano wa kisiasa.

Sawa wakati wa Nyerere na sasa ni tofauti kwani Mwalimu alikuwa ni idealist na alikuwa yuko tayari kusacrifise maisha ya MTZ ili Mzimbabwe au Mu Angola aishi huru na salama lakini kama nilivyosema hapo awali mamabo yamebadilika na tusiwe tunafanya haya mambo for the sake of doing it especially kama hayana NATIONAL INTEREST kwetu.

Kimsingi kazi ya usuluhishi wa migogoro ni biashara kubwa.

enhe,

Nasema ni biashara kwa misingi kuwa watu wetu watakaokuwa wanafanya kazi katika mabaraza au mahakama za usuluhishi, ni wazi watakuwa hawajitolei. Hawa watakuwa wanalipwa, kumbi za mikutano na hoteli wanapolala wahusika wakati wa mikutano vinalipiwa, bila kutaja chakula na matumizi ya ziada wanayofanya washiriki wa mikutano hii wanapokuwa hapo nchini.

Kabla hujaendelea narudia tena swali nililokuomba hapo awali, lete cost analysis iliyopelekea kwa ARUSHA ACCORD 1 & 2 then tuambiane local staff wanalipwa kiasi gani and so on then itakuwa launchpad nzuri ya kujengea hoja otherwise utakuwa unatwanga maji kwenye kinu.

Hata hivyo, lipo jambo moja linalonitia wasiwasi kwa sasa. Jambo hili ni umahiri wa watu wetu hasa katika fani hii ya usuluhishi wa migogoro.

enhe,

Kipo kizazi kilichofanya kazi Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miongo kadhaa na kupitia uzoefu au shule walizopata wakapata utalaamu unaotumika kushawishi na hatimaye kutatua migogoro hii.

sawa,

Kinachonitia wasiwasi na kunilazimu kumtahadharisha waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwa fursa hii tunaweza kuipoteza sioni mipango thabiti ya kuandaa vijana wapya wa kuendeleza taaluma hii ya usuluhishi. Conflict Resolution ni fani maalumu inayokuja juu kwa kasi kubwa duniani na watu wanaisomea kuanzia shahada ya kwanza hadi ya uzamivu, ila sijaona mpango-mkakati wa kuhakikisha Tanzania inakuwa na wataalamu wa kutosha katika nyanja hii.

Mimi sijakuelewa, hivi balile unataka tuendeleze vijana wengi katika fani hii ya conflict resolution wakati hujatoa mchanganuo jinsi gani tutanufaika vipi na hiyo kozi. Kama utasoma nakala zangu za nyuma nimekuwa ni critic mkubwa tuu humu ndani wa Bwana Membe na Foreign kwa ujumla lakini hii yako ni kali zaidi. Kwani hujaja na hoja thabiti juu ya hili na kama unhetaka then bora uje na data kamili ili kusupport argument yako. Kama ni revamp then naweza kukuambia kuwa civil service yetu nzima inatakiwa ifanyiwe revamp au reforms na kama issue ni MOF then njoo na data mzee

Kwa kuwa wizara hii iliyopo chini ya Membe inayo dhamana ya usuluhishi wa migogoro, nimsihi aliangalie suala hili na kujaribu kutafuta hata vyanzo mbadala vya mapato, vijana wetu wanaoibukia wenye umri wa miaka 19 hadi 30, wapelekwe shule katika fani hii tuwe na wataalamu wa kutosha.

Yaani unataka Membe aangalie hila kwa kupropose AGE DISCRIMINATION, vipi mzee balile mbona hivi? je mtu akiwa na iaka 32 ndio hana nafasi au tumnyime?

Napendekeza umri huu kwa sababu hawa wakipata utalaamu kwa umri wao wataweza kulitumikia taifa kwa miaka 30 na zaidi, badala ya kupeleka shule kwa kiwango cha uzamivu mtu mwenye miaka 48, akirejea kutoka masomoni anatumikia miaka minne anastaafu kwa hiari au anaongeza miaka mitano na kulazimika kustaafu kwa mujibu wa sheria.

sawa lakini usisahau kuwa experience ya wazee nayo inahitajika japo kwa mbali hoja yako inaelekea kufanana na ya Yakubu kuhusu kuwapa nafasi wazee na majibu yani ni kuwa Public sector yetu inatakiwa ifanyiwe reforms za hali yajuuu kama nilivyoshauri hapo awali

Itakuwa ni aibu kwa taifa letu kuwa na sifa ya usuluhishi wa migogoro, lakini watendaji wa mabaraza au mahakama husika wanatoka mataifa mengine na hakuna Watanzania wenye kufanya kazi hii.

Kweli kabisa lakini hujaeleza kwa nini hili hotokea

Chonde chonde Membe lifikirie hili, na ikiwezekana ulitafutie ufumbuzi. Tukisuasua, fursa hii tutaipoteza. Mungu Ibariki Tanzania.

deobalile@yahoo.com – 0007904159144

Once again kama nilivyokuambia kuwa Membe budget yake ni ndogo sana na kama ni proposal basi nadhani ungeomba serikali iipatie wizara hii pesa zaidi lakini sidhani kama kuna haja ya kumwaga mapesa mengi kwenye conflict reslution huko Burundi na Congo ili hali tunashindwa kufanya hivyo kwenye mgogowa ZANZIBAR ambao uko ndani ya uwezo wetu nashangaa hujaliongelea hili

Natumai utarejea kujibu hoja zangu.

I really missed him kwa muda kwani hakurudi tena
 
Hii nayo ni "breaking news" kiaje?

Wanasema anaweza kurudishwa mara RA atakapojulishwa, wanasema huo ni uamuzi wa ndani ambao hauna baraka za RA. Wanasema hajang'olewa bali amewekwa pembeni kwa muda kabla ya kurudishwa.

Pamoja na hayo kama ndani ya jumba wanaweza kumuasi mwenye mali basi wajue zao zimekwisha na kwamba wakati wowote watakosa wa kuwafuata. Hii ni kama hadithi nyingi ambazo tunasimuliwa za HIMAYA INAYOANGUKA, maana hata ndani ya Jumba la Mfalme wataasi na ataangalia na kukosa pa kushika moto wa mapinduzi utakaposhika kasi.

MUNGU ENDELEA KUWALAANI NA KUWAANGAMIZA MAFISADI
 
Nilipokuwa napiga makelele juu ya hatma ya Balile na roho yake ya usaliti mlisema Lunyungu umezidi na majungu .Now here we are .Balile hana pa kwenda na mwisho umefika .Haya nilimtabiria long time ago hakuwa anaelewa nina kisema
 
vyanzo vya upande mwingine vinaonesha RA ametoa baraka zake; ila yawezekana tumeivujisha mapema wanaweza wakabadili maamuzi. Ile editorial yake ya juzi nadhani haikumfurahisha mtu yeyote ndani ya ofisi yake.

Tuangalie
 
Hizi ni issue za waandishi wa habari wenyewe, pelekeni kwenye jukwaa la wahariri mkajadili kwa mapana huko!!!
 
Wanasema anaweza kurudishwa mara RA atakapojulishwa, wanasema huo ni uamuzi wa ndani ambao hauna baraka za RA. Wanasema hajang'olewa bali amewekwa pembeni kwa muda kabla ya kurudishwa.

Pamoja na hayo kama ndani ya jumba wanaweza kumuasi mwenye mali basi wajue zao zimekwisha na kwamba wakati wowote watakosa wa kuwafuata. Hii ni kama hadithi nyingi ambazo tunasimuliwa za HIMAYA INAYOANGUKA, maana hata ndani ya Jumba la Mfalme wataasi na ataangalia na kukosa pa kushika moto wa mapinduzi utakaposhika kasi.

MUNGU ENDELEA KUWALAANI NA KUWAANGAMIZA MAFISADI

Bado sijaelewa umuhimu wa huyo Balile, na kwa nini kung'olewa kwake huko Rai kupewe uzito kiasi cha kuitwa "breaking news". I mean who is he to me and most of us? Isn't he just one of the many folks who get sacked for a variety of reasons, I mean why should this bother us? He got sacked, so what? Hii nayo ni breaking news?
 
Kithuku kuwa mtulivu na soma kwa makini mabandiko juu ya Balile hapa jamvini .Kwa nini ni habari then uje ujadili vinginevyo tulia mkuu wacha tufuatilie .
 
Wacha nimpigie Balile nisikie anasemaje .Sijui kama atakumbuka utabiri wangu .
 
Back
Top Bottom