Kwa kuangalia mpangilio wa Ukurasa wa kwanza wa gazeti la Rai la tarehe 19.2.2015, nna maoni yafuatayo:
1. Huenda huu ukawa ni mpango ama mkakati wa "kumfagilia" ndugu Lowassa. Nnaona akiwa katika picha kubwa, ameshika kifimbo chenye alama ya bendera ya Taifa, wakati wanasiasa wengine, Mbowe na Kinanawakiwa katika picha ndogo wanaangaliana (kama vile wanakabiliana), wakihinikizwa na habari kuwa vyama vyao vinaharibu nchi.kwangu mie huu mpangilio siyo bahati mbaya.
2. Mwandish/Mhariri analenga "kutafuta huruma" za watu (na wapiga kura?) kuwa Muhusika anawindwa "kwa sababu yuko juu kisiasa".
3. Habari haina chanzo cha kuaminika... Habari imejificha chini ya kivuli cha "Rai imebaini". Hapa naona kuwa..... Yuko katika hali ya sintofahamu baada ya kupokea taarifa toka vyanzo tofauti..... ingefaa, katika hali ya kawaida ya maadili ya Uandishi mahiri... kumtumia/kumtaja MHUSIKA kama chanzo cha habari tajwa.