Raha ya kupanda daladala

Raha ya kupanda daladala

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,349
Jana Jumapili ilikuwa siku ya kazi kwa sisi wengine. Niliamua kupanda basi kwa usumbufu wa parking na si kuwa na safari nyingine zaidi ya kazi na kurudi nyumbani.

Kituoni nilikaa na mama mmoja aliyenizidie umri kidogo. Kilicho tufanya tuanze kuongea ni kijana aliyetuomba hela akapate kifungua kinywa. Tulijikuta tuna something in common. Huyu mtoto tunaeweza kumzaa asiende kazini wakati sisi mama zake tunasubiri bus kwenda kazini.

Baada ya hapo nilipata shost tukaanza kusogoa. Shost aliniambia alikuja Dar miaka ya 1977-78. Ni mjomba wake alimuomba kwa wazazi wake. Baada ya kumaliza shule aliajiriwa na kupata nyumba ya National Housing ya vyumba viwili.
Kazini mkataba uliisha alilipwa kiinua mgongo na kuamua kujenga Guest House mkoani alikozaliwa. Guest ilikwisha na kuanza biashara.

Siku moja kanisani alikutana na mdada aliyeanza nae darasa la kwanza. Huyu dada ni mwalimu na amekuja Dar kumfuata mume wake. Wana watoto watatu lakini ndoa ina matatizo makubwa. Baada ya kubadilishana namba za simu mwalimu alimuomba msaada wa pango la nyumba ili ahame kwa mumewe.

Kwakuwa shost hakujaliwa kuwa na mtoto alimkaribisha mwalimu kwenye flat yake. Walijibana na watoto akimpa mwalimu muda wa kujipanga upya. Huku na huku akahisi anaibiwa pesa kwenye Guest House yake mkoani. Kwakua hana ajira mjini aliamua kwenda kusimamia biashara yake. Alimuacha mwalimu kwenye flat kwa makubaliano aiangalie.

Alikaa mkoani miaka miwili. Alikuja kugundua mzunguko wa pesa mkoani si kama Dar. Hakuna cha kuibiwa wala nini. Baada ya miaka miwili alirudi mjini akifikiria biashara ya mama ntilie mjini na vipesa vya Guest vitamsogeza.

Amerudi anakuta mwalimu amebadilisha mkataba na kuwa sasa yeye ndiye mpangaji halali wa NHC. Shost amepangisha chumba. Nilimpa pole sana.

Tenda Wema uwende, umdhaniae ndiye.
 
Naona umepata marafiki na kumuona mpiga vizinga mmoja,,,,mpiga vizinga anakera sana.

Hali kadhalika na ninyi wanawake,,,kuna wengine hafikirii hata kuuza sabuni,,,yeye kila kitu mpaka ampige vizinga mwanaume,,,mnatisha kwa hilo
 
Jana Jumapili ilikuwa siku ya kazi kwa sisi wengine. Niliamua kupanda basi kwa usumbufu wa parking na si kuwa na safari nyingine zaidi ya kazi na kurudi nyumbani.

Kituoni nilikaa na mama mmoja aliyenizidie umri kidogo. Kilicho tufanya tuanze kuongea ni kijana aliyetuomba hela akapate kifungua kinywa. Tulijikuta tuna something in common. Huyu mtoto tunaeweza kumzaa aiende kazini wakati sisi mama zake tunasubiri Basie kwanda kazini.

Baada ya hapo nilipata shost tukaanza kusogoa. Shost aliniambia alikuja Dar miaka ya 1977-78. Ni mjomba wake alimuomba kwa wazazi wake. Baada ya kumaliza shule aliajiriwa na kupata nyumba ya National Housing ya vyumba viwili.
Kazini mkataba uliisha alilipwa kiinua mgongo na kuamua kujenga Guest House mkoani alikozaliwa. Guest ilikwisha na kuanza biashara.

Siku moja kanisani alikutana na mdada aliyeanza nae darasa la kwanza. Huyu dada ni mwalimu na ameamua Dar kumfuata mume wake. Wana watoto watatu lakini ndoa ina matatizo makubwa. Baada ya kubadilishana namba za simu mwalimu alimuomba msaada wa pango la nyumba ili ahame kwa mumewe.

Kwakuwa shost hakujaliwa kuwa na mtoto alimkaribisha mwalimu kwenye flat yake.
Nafikiri daladala imepata pancha abiria wameshuka ikipona ataendeleza story.
 
Jana Jumapili ilikuwa siku ya kazi kwa sisi wengine. Niliamua kupanda basi kwa usumbufu wa parking na si kuwa na safari nyingine zaidi ya kazi na kurudi nyumbani.

Kituoni nilikaa na mama mmoja aliyenizidie umri kidogo. Kilicho tufanya tuanze kuongea ni kijana aliyetuomba hela akapate kifungua kinywa. Tulijikuta tuna something in common. Huyu mtoto tunaeweza kumzaa aiende kazini wakati sisi mama zake tunasubiri Basie kwanda kazini.

Baada ya hapo nilipata shost tukaanza kusogoa. Shost aliniambia alikuja Dar miaka ya 1977-78. Ni mjomba wake alimuomba kwa wazazi wake. Baada ya kumaliza shule aliajiriwa na kupata nyumba ya National Housing ya vyumba viwili.
Kazini mkataba uliisha alilipwa kiinua mgongo na kuamua kujenga Guest House mkoani alikozaliwa. Guest ilikwisha na kuanza biashara.

Siku moja kanisani alikutana na mdada aliyeanza nae darasa la kwanza. Huyu dada ni mwalimu na ameamua Dar kumfuata mume wake. Wana watoto watatu lakini ndoa ina matatizo makubwa. Baada ya kubadilishana namba za simu mwalimu alimuomba msaada wa pango la nyumba ili ahame kwa mumewe.

Kwakuwa shost hakujaliwa kuwa na mtoto alimkaribisha mwalimu kwenye flat yake. Walijibana na watoto akimpa mwalimu muda wa kujipanga upya. Huku na huku akahisi anaibiwa pesa kwenye Guest House yake mkoani. Kwakua hana ajira mjini aliamua kwenda kusimamia biashara yake. Alimuacha mwalimu kwenye flat kwa makubaliano aiangalie.

Alikaa mkoani miaka miwili. Alikuja kugundua mzunguko wa pesa mkoani si kama Dar. Hakuna cha kuibiwa wala nini. Baada ya miaka miwili alirudi mjini akifikiria biashara ya mama ntilie mjini na vipesa vya Guest vitamsogeza.

Amerudi anakuta mwalimu amebadilisha mkataba na kuwa sasa yeye ndiye mpangaji halali wa NHC. Shost amepangisha chumba. Niliona pole sana.

Tenda Wema uwende, umdhaniae ndiye.
Hii story inafanana kabisa na moja ilitokea Dodoma. Mafanyakazi (ke) alihamia Dar. Rafiki yake akamuaproach kuwa mchungaji wao kahamia Dodoma na anahangaika kupata makazi. Mama hakutaka kupangisha nyumba kwani alitaka kuwaachia ndugu zake kwa matumaini ya kurudi Dodoma kwa makazi ya kudumu baadae. Na hii ilikuwa ni nyumba ya shirika. Mama akakubali kumpangisha Mchungaji baada ya kuombwa sana. Kumbuka mkataba original ni kati ya shirika na mteja wake. Baada ya kipindi mwenye nyumba alirudi Dodoma na kuamua kwenda kuangalia kama bili (nadhani zilikuwa za umeme au maji za nyumba yake zinalipwa).alipata mshutuko baada ya kuambiwa account ipo kwajina tofauti na la kwake, na lilikuwa la mchungaji . Kwenda kumuuliza mchungaji kulikoni akawa anampiga chenga. Kwenda kwa mdhamini wa mchungaji haelewi kitu. Katika kufuatilia akabaini mchungaji alifungua kesi mahakamani akidai mkataba nashirika kwani yeye ndo alikuwa mtumiaji wa nyumba hiyo (nadhani shirika hawaruhusu mpangaji wao kupagisha- ingawa watu husaidiana).Wito wa mama mahakamani mchungaji ni kama alikuwa naficha na hivyo akawa hatokei siku za kesi. Baadae wito ukatangazwa magazetini na mama hakubahatika kuuona. Nadhani manavijua vile vitangazo vidogo vidogo ambavyo huwa vinaita watu kwenye kesi vikitishia kusikiliza upande mmoja iwapo hutafika. Ndicho kilichotokea. Kesi ilisikilizwa upande mmoja na mchungaji akapewa ruhusua ya kuingia mkataba na shirika. Nyumba ikawa imeondoka na mamaalikuwa mjane na alikaribia kustaafu. Hii ilitokea some years back ila true story.
 
Hivyo vizinga vya hela ya kula au nauli kwa Dsm ni kitu cha kawaida, nimewahi kuombwa nauli na vijana wawili maeneo ya Riverside ubungo ya kuwafikisha Mbezi ya kimara, elfu moja sio kitu, nikawapa. Hapo nilikuwa namsindikiza rafiki kwenda Mabibo hostel, baada ya dakika 10 nakutana na vijana wale wale wananiomba nauli ya kwenda Kimara kwa mara ya pili baadaye wakahisi aibu na kukimbia mbali.Kwahiyo vizinga ni kawaida Miss.
 
Hii story inafanana kabisa na moja ilitokea Dodoma. Mafanyakazi (ke) alihamia Dar. Rafiki yake akamuaproach kuwa mchungaji wao kahamia Dodoma na anahangaika kupata makazi. Mama hakutaka kupangisha nyumba kwani alitaka kuwaachia ndugu zake kwa matumaini ya kurudi Dodoma kwa makazi ya kudumu baadae. Na hii ilikuwa ni nyumba ya shirika. Mama akakubali kumpangisha Mchungaji baada ya kuombwa sana. Kumbuka mkataba original ni kati ya shirika na mteja wake. Baada ya kipindi mwenye nyumba alirudi Dodoma na kuamua kwenda kuangalia kama bili (nadhani zilikuwa za umeme au maji za nyumba yake zinalipwa).alipata mshutuko baada ya kuambiwa account ipo kwajina tofauti na la kwake, na lilikuwa la mchungaji . Kwenda kumuuliza mchungaji kulikoni akawa anampiga chenga. Kwenda kwa mdhamini wa mchungaji haelewi kitu. Katika kufuatilia akabaini mchungaji alifungua kesi mahakamani akidai mkataba nashirika kwani yeye ndo alikuwa mtumiaji wa nyumba hiyo (nadhani shirika hawaruhusu mpangaji wao kupagisha- ingawa watu husaidiana).Wito wa mama mahakamani mchungaji ni kama alikuwa naficha na hivyo akawa hatokei siku za kesi. Baadae wito ukatangazwa magazetini na mama hakubahatika kuuona. Nadhani manavijua vile vitangazo vidogo vidogo ambavyo huwa vinaita watu kwenye kesi vikitishia kusikiliza upande mmoja iwapo hutafika. Ndicho kilichotokea. Kesi ilisikilizwa upande mmoja na mchungaji akapewa ruhusua ya kuingia mkataba na shirika. Nyumba ikawa imeondoka na mamaalikuwa mjane na alikaribia kustaafu. Hii ilitokea some years back ila true story.
Very sad
 
Yah hivi vitangazo vinawekwa hata kwa kuvunja ndoa. Ni wachache sana wanaobahatika kuvisoma
 
Back
Top Bottom