Rafu za mapema zamnyima usingizi Halima James Mdee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rafu za mapema zamnyima usingizi Halima James Mdee

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ejogo, Oct 2, 2010.

 1. e

  ejogo JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima James Mdee hana usingizi, akitafakari rafu za mapema ambazo inadaiwa anapigwa na wapinzani wake.

  Habari zilitua kwenye dawati la Risasi Jumamosi na baadaye kupata
  uthibitisho kwa Halima mwenyewe kuwa kuna michezo michafu anafanyiwa
  lakini unaomuumiza kichwa ni ule wa kupandikiza wapigakura feki jimboni
  kwake.

  Habari zinasema kuwa kuna watu feki kutoka maeneo tofauti na Jimbo la
  Kawe ambao wanaandaliwa mazingira ya kupiga kura kinyume na utaratibu
  uliowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na muongozo wa
  Daftari la Kudumu la Wapigakura.
  Akilizungumzia hilo, Halima alisema taarifa za watu kusambazwa ili
  kupiga kura kinyume na utaratibu amezipata muda mrefu na anazifanyia
  kazi kikamilifu kwa sababu anahisi ni mpango maalum wa kummaliza
  kisiasa.

  “Unajua huu mchezo hauwezi kufanikiwa bila kupata baraka za NEC, hili
  nalifuatilia na ndiyo maana nahoji mbona mpaka sasa daftari halijawekwa
  hadharani, hii
  chelewachelewa inaweza kuambatana na hujuma,” alisema Halima na kuongeza:
  “Siwezi kupuuza taarifa ninazopewa, nafuatilia kuona ukweli wa kile
  kinachosemwa. Nitafika mpaka tume kuhakikisha hili halifanikiwi,
  kitendo cha kuchukua wananchi Mbagala ili wampigie kura mgombea fulani
  ni uhuni na siyo siasa.

  “Wananchi pia wajue, kama mgombea anataka kushinda uchaguzi kwa kutumia
  ‘faulo’ huyo hawezi kuwa kiongozi bora baadaye. Uadilifu wa mtu lazima
  uonekane kuanzia mwanzo hadi mwisho. Na ninasisitiza, hao watu wa
  Mbagala na Tandika hawatapiga kura Kawe.”

  Jimbo la Kawe, ni kati ya majimbo ambayo yameonesha kuwa na upinzani
  mkubwa kutokana na kushirikisha wagombea watatu wenye nguvu, Halima,
  Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Angela Kizigha wa CCM.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Halima. Relax. Mwaga sera. Utashinda.

  (Hata Usiposhinda kwa hizo hila zao, lazima urudi mjengoni ukawakilishe)
   
 3. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata akishindwa anapita kule kwenye viti maalum. Si ma-girlfriend wa viongozi wa chama washapitishwa kisirisiri? :tonguez:
   
 4. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole sana kwa kuwa dekio lamafisadi
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  halima mdee naomba sana ushirikiano wako nitumie namba yako ya simu nikutumie pesa za kukusaidia ktk harakati
  zako za kisiasa hapo TZN. nilipokuwa nyumbani mwaka 2009 mwezi dec mpaka january nilifuraishwa sana na hotuba
  yako uliyoitoa bungeni. ulionyesha uchungu mkubwa na nia yangu nikukuonyesha kuwa tupo watanzania tunao care
  na tungelipenda kukusaidia ktk harakati zako za kuleta mapinduzi ya kisiasa hapo nyumbani. naomba uwasiliane nami
  ktk zuberi.hamisi@yahoo.com tafadhali sana maana hii itanifanya angalau nilale usiku kwa amani kwa maana at least i
  did something trying to stop CCM from destroying our country.
   
 6. ismase

  ismase Senior Member

  #6
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Una nia ya dhati ya kumsaidia au una lako jambo. kuwa wazi maana hakuna cha bure dunia hii ikizingatia binti mwenyewee mmmuh......??????
   
 7. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hivii,nomba niulize, jee ni lazima sote hapa JF tuwe CHADEMA? ni kwa nn mtu akitoa comments zake negative dhidi ya CHADEMA lazima mwite fisadi?jee hii ina ,maana kila Mtanzania ambayesi CHADEMA ni fisadi?hbu acheni kupotoshaUmma uamini kuwa CHADEMA hufuata haki atika kupata viti maalum, hii si kweli. Ni lazima mkubali kukosolewa sio kuanza kuli2 eti kuna rafu.............................
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Si lazima sote tuwe Chadema lakini comments nyingine are very boring, huwezi kusema wamepitisha magirl friend wao ukiwa hata evidence huna ukaachwa, lazima upewe maneno yako. Mkunga ur also dekio la mafisadi
   
 9. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Jibu ni hapana ... hapa ni uwanja huru na kila mtu anaruhusiwa kuwa na uanachama wa chama chochote au kutokuwa na chama kabisa. LAKINI ...kwa vile Chadema inasimamia ukweli ina maana ukisema uongo moja kwa moja una-qualify kuwa ant-Chadema
   
 10. N

  Njaare JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  MH! Kushaabikia CCM yataka Moyo
  Kwani unaonekana kama wee si wa Tanzania hii. Au bado unafikiria yale ya sabini ya kuwa binadamu wote ni sawa na Africa ni moja.
   
 11. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #11
  Oct 2, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama mtu mwenye AKILI TIMAMU atadiriki kuandika hapa UTUMBO unaouandika wewe!

  Una-insinuate kwamba Halima ni "girlfriend" wa kiongozi wa chama, UNA UHAKIKA?

  Unaweza kutoa madai hayo yako ya KIPUMBAVU yasiyo na hoja yoyote ile ya msingi, kwa kuwa tu huwezi kuadabishwa kwa uongo wako huo.

  Ungeitwa mbele ya Halima uthibitishe madai yako hayo, UNGEKWENDA?
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa sababu huyu Kudadeke amezoea kushabikia Kikwete na Lowassa ambao waligawa u DC kwa magelifriend zao.
   
 13. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Duh!! Mi nilifikiri kuna mgando wa maziwa tu,kumbe hadi wa ubongo upo.
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Hapana si lazima, huu ni uwanja huru. Kinachowafadhaishwa wengi humu JF ni swali la kwa vipi Mtanzania yeyote mwenye akili timamu, mwenye uchungu na nchi yake na anayeitakia mema taifa lake, anaweza kuishabikia CCM. Mgombea Uraisi kutoka CCM anasimama jukwaani na kuanza kuwasafisha na kuwanadi watuhumiwa wa kila aina ya uchafu kwa macho makavu tena mbele ya wananchi bila aibu wala haya.

  Si hivyo tu kinachoudhi zaidi ni kuwaona wananchi ambao hawana hata uhakika na mlo wao wa siku, wakilazimika kumshangilia huyo mshirika wa mafisadi kwa sababu tu wamepewa kitu kidogo kama kanga, fulana, kofia na labda bahasha. Sasa taabu inakuja hivi hapa JF ni ukumbi ambapo tunaita koleo kwa jina lake na tunamkoma nyani giledi bila kumtazama uso na bila kujali rangi, wadhifa, itikadi, dini, mali wala umri wake.

  Kama wengi humu ndani wataonekana wanaunga mkono Chadema ni kwa kuwa ni chama kinachoonyesha utashi wa kutaka kuleta mabadiliko kwa mfano katiba ambayo mapungufu yake yamewawezesha wezi na walafi kutanua na kuitafuna nchi hii kwa nusu karne bila kuwajibishwa. Tunacholilia ni utawala unaozingatia sheria na ambao unalinda haki za msingi za kila mwananchi bila ubaguzi wa aina yoyote kwa kuhakikisha usawa kwa wote.

  Tanzania bila CCM yawezekana.

   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Mkunga,

  Mkuu JF ni jukwaa huru kabisa lakini inahitaji moyo wa chuma kuikosoa CHADEMA.Kila jambo linalotendwa na CHADEMA ni zuri hakuna kukosoa na ukijaribu utapewa majina ya ajabu.Nitatoa mifano michache ambayo imenishangaza kidogo.

  [1] Kitendo cha Dr W Slaa kumwoa mke wa mtu sikukipenda hata kidogo hasa tukizingatia nafasi yake ndani ya jamii na nafasi anayopigania kuipata [Urais].Kitendo chake hakikuniondoa kumpatia kura yangu lakini nilisononeka sana kila nilipokuwa nikijaribu kutafuta utetezi nililazimika kutumia hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja.

  Utetezi wa wanaJF wengi uliegemea zaidi kwenye ushabiki wa kichama badala ya kutazama uhalisi wa jambo lenyewe.

  [2] A. Mgombea ubunge wa CHADEMA Arusha mjini alihusika bila shaka yoyote kumuuza diwani wa upinzani CCM na kushiriki kumpigia kampeni hadi kushinda udiwani akiwa CCM.

  B. mgombea ubunge huyu alihusika bila shaka yoyote kuondoa kesi ya kupinga ushindi wa Mheshimiwa F Mrema wa CCM,baada ya kupewa kitu kidogo.

  C. Mgombea huyu pia hakusema kweli kuhusu elimu yake kwa waliosikiliza mdahalo TBC1 wagombea ubunge Arusha mjini Bwana Lema alidanganya watazamaji kwamba ana Advance Diploma in Human Resources Management jambo ambalo si kweli hata kidogo.Mwaka 2005 Bwana Lema alidai ana Diploma ya Theologia jambo ambalo si kweli.Ikiwa hali hii itaachiwa mwaka 2015 pengine atagombea kupitia CUF atadai ana PhD yamkini wana CHADEMA mtakuwa tayari kumkosoa kwasababu atakuwa akiwakilisha chama kingine !.

  Utetezi wa wanaJF ulinishangaza kidogo.wengine walisema una chuki binafsi,wengine mbona unamwandama sana Lema,wengine crap,wengine porojo.
  Nikajaribu kupitia post za waliokuwa mabingwa wa kumtetea Bwana Lema ambazo zilikuwa zikizungumzia ufisadi wa CCM nilibaki kinywa wazi wachangia wale wale hawaku sema crap,unachuki binafsi na nk.

  Mkuu Mkunga JF si jukwaa la CHADEMA isipokuwa wapo baadhi ya watu wanatakakutufanya wajinga kwamba mafisadi wako CCM pekee yake CHADEMA wapo malaika kitu ambacho si kweli hata kidogo.Wapo watu wabovu CCM pia wapo watu safi.Wapo watu wabovu CHADEMA pia wapo watu safi tuwaseme bila kujali wanawakilisha chama gani.

  Tofauti kati ya CHADEMA na CCM ni kwamba CCM wapo madarakani ni rahisi kuona madhaifu mengi kwa sasa.Udhaifu wa CCM unaidhuru jamii [watanzania] moja kwa moja.Madhaifu ya CHADEMA hayana madhara kwa jamii mpaka hapo watakapo shika dola.Ni haki ya jamii kuikosoa CCM na ikiwezekana kuiweka kando,naamini muda wa kuipiga chini CCM umefika wasi wasi wangu mkubwa ni dalili nilizoanza kuziona ndani ya jamii ya watanzania hasa JF hawataki kusikia au kuona CHADEMA ikikosolewa naanza kujiuliza siku ikishika dola mambo yatakuwaje ?.Uhuru wa kupata habari naanza kuhisi utakandamizwa mengi nasubiri siku yeyewe ifike.
   
 16. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuishabikia CCM inahitaji kuwa na akili kama ya mwendawazimu. Yaani ufumbe macho na kila baya ulione zuri. hapo utakuwa na moyo huo. Bye
   
 17. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Halima hawezi kupoteza kawe. Amekwisha shinda tayari. labda tuongelee majimbo mengine. ' trust me, I know this'
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sielewi Utaratibu wa kupigaji kura Tanzania kama ni sawa na hizi nchi za nje ambao wao swala kama hili haliwezekani kabisa kutokea. Kwanza kila mpiuga kura anapiga kura sehemu alojiandikisha na unapoingia ktk chumba cha kupiga kura unatoa kitambulisho chako cha Uraia ambacho kinapitiwa na wajumbe wawakilishi wa vyama vinavyogombea kuhakikisha kwamba wewe ndiye mwenye kitambulisho hicho na jina lako lipo ktk daftari la wapiga kura.

  Kila mjumbe ana kopi ya daftari hilo hivyo unapokubalika tu jina lako linapigwa msitari mwekundu kama umefika na kisha unapewa form ya kupiga kura na kuelekezwa sehemu ya faragha ambayo utapiga kura yako. Na kila kituo kina independent Observer, askari au wana usalama wakitazama kwa makini kinachoendelea baina ya wapiga kura, wajumbe wawakilishi wa vyama na sanduku la kura.

  Hivyo hivyo inakwenda kwa kila mtu anayeingia kupiga kura, na haiwezekani kabisa mtu atoke Mbagala kuja piga kura kituo ambacho jina lake halipo ktk dafatari au amesahau kitambulisho chake..Na kila kituo kina hesabu kamili ya watu waliojiandikisha kupiga kura kwa hiyo wanajua kila hatua na asilimia ya wapiga kura walipiga tayari against idadi inayotakiwa.

  Na pengine hofu ya Bi. Halima iitakuwa imechelewa kufikishwa kwa sababu huu sii wakati wa kulalamika ila kuzidisha mashambulizi..Kwenye utata wa utaratibu mzima wa Upigaji kura unatakiwa kurekebishwa mapema badala ya kulalamikia NEC hali kuna uwezekano mkubwa wa kuthibiti uhalifu kama huo.
   
 19. O

  Ogah JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kwenye msafara wa Mamba hata Kenge huwemo.............ni kweli kuna watu hawako serious in answering some of the allegations ambazo zinaelelkezwa kwa Chadema.......pengine kwa kuwa sio responsibility yao kujibu and they take an opportunity ku-release some frastrations zilizo kuwa built-up na CCM miaka nenda rudi.............inahitaji uvumilivu wa hali ya juu kwa kweli juu ya Majambazi CCM walivyotutenda..............

  Kumbuka ndani ya CCM Kenge wamezidi idadi ya Mamba.........kwa hiyo mambo ni tibwilitibwili............trust me Dr. Slaa yuko hapa JF kila patapo nafasi huja hapa kuonyesha yale anayokusudia kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu...........sidhani hao kenge wachache hawatashughulikiwa na kamanda huyu............ufisadi hauko kwenye madini pekee tuliyozungumzia hapa JF...........tumepiga madongo mpka waliojipa elimi ambazo hawastahili............the same standard itatumika kwa wanachadema/cuf/nccr and the like.................

  hapa ni kumpiga nyani giladi mchana kweupe hapendwi mtu hapa.................it is so happen that hapa JF Chadema imekubalika sana kutokana na baadhi ya viongozi wao (kuanzia Mtei, Mbowe, Mnyika, Zitto, Dr. Slaa, Dr. Kitila ni wanachama hapa JF) kuwepo hapa na ku-clarify so many doubts walizokuwa nazo wanajamvi.............its so happened.............hakuna anayezuiwa hapa JF

  nafasi hiyo hiyo CUF/CCM/NCCR wana rukhsa kuitumia kumwaga sera zao hapa na kutetea pale walipoenda fyongo.............lakini wao (CCM) wakija hapa ni blah blah blah na vitisho na kujiaminisha kuwa wao ni mashine kubwa haiwezi kushindwa na hata Rais Kikwete mwenyewe AMETUBEZA JF kuwa tunadanganyana na kupoteza muda.............yeah they/He may be right...........sasa wasilalalmike kuwa JF ni pro Chadema..........waache watu wawachambue na kuwapa ukweli.............

  The bottom line JF SIO CHADEMA....ni chombo huru kabisa ila haizuii wanachama wake kuwa wanasiasa/wapenzi wa vyama vyetu..........

  ..............i know what the current politicians think about NCHI YETU...........what i can say mimi na wewe tulete mabadiliko and this is our opportunity.................

  CAN YOU IMAGINE 50 YEARS with all the resources tuko wapi leo hii na nchi yetu bado ni kichwa cha mwendawazimu..........expecting different results.................damn
   
Loading...