Rafiki yangu yuko njia panda kuhusu mchumba wake

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,426
2,000
Hii siyo story ni ukweli na mda huu nipo na mmoja wa wahuska.

Kuna jamaa anaishi na mke ambaye hawajafunga ndoa lakini ni miaka 5 sasa na wana mtoto mmoja, kimsingi jamaa anavyodai wameishi kwa kuvumiliana sana ingawa kwa misukosuko,magomvi,migogoro.

Walikutana wakiwa A\level wakaenda chuo mpaka wakahitimu wako wote.

Sasa tukio la hivi karibuni ni kwamba walizozana na mkewe,mkewe akadai waachane lakini jamaa akamwambia sioni wala sina sababu ya kuachana na wewe.

Jamaa kaenda mbali zaidi akamkumbusha mkewe kumbuka tulikotoka,tuliwahi ishi maisha ya kulala kesho hatujui tunakula nini,bt mkewe haelewi basi jamaa kamwambia mkewe apige simu kwao kwa mama ake na ndugu zake awataarifu kwamba wanatengana na atoe sababu.

Jamaa yeye alishafka ukweni kwa shinikizo la mkewe na alipokelewa vizuri sana mpaka pa kulala,mama mkwe alimkubali sana jamaa,hivyo anahisi aibu sana leo aseme anaachana na mtoto wao tena kwa shinikizo la mtoto wao.

Sasa tokea hiyo juzi mpaka leo xmass mke hapiki wala hafanyi,jamaa yuko njiapanda sana.

USHAURI WENU WANA MM
 

dist111

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
3,515
2,000
Amwache tu ndoa isiyokuwa na amani sio ndoa


Ingawa hawajaoana, ila kwa muda wote waliokaa pamoja wanajuana zaidi ya hapo! Amvumilie tu, manake wanawake wanapitiaga vipindi vigumu sana, huwezi jua yuko ktk mabadiliko gani!

Ikipita miezi angalau 2 na bado mwanamke anamsimamo huo! basi hapo hana jinsi ila kwa wiki 1-3 anaweza mvumilia, Actually uhusiano ni uvumilivu! so amvumilie kwa ss
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,852
1,250
Yaani jamaa anaona tabu kuachana na huyo girlfriend wake??
kwa mtazamo upi ni girlfriend mkuu? wameishi 5 solid years pamoja, yaani chini ya paa moja na wanamtoto bado tutaiweka kwenye hiyo status mkuu?
 

pachachiza

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
1,741
2,000
inawezekana dem ashapata mwengine so asijekuta analazimisha kuoa wakati haitadumu. kabla ya kuoa ni lazima uangalie yule uliyenae mtadumu sio swala la kuwa mnajuana kwa muda mrefu coz ndoa ni ndoana haswa ya kikristo.
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,852
1,250
mtu hamtaki, anamng'ang'ania wa nini?? na kwanini ajiskie vibaya mbele ya wazazi wa mkewe?
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
10,667
2,000
hii siyo story ni ukweli na mda huu nipo na mmoja wa wahuska, kuna jamaa anaishi na mke ambaye hawajafunga ndoa lakini ni miaka 5 sasa na wana mtoto mmoja, kimsingi jamaa anavyodai wameishi kwa kuvumiliana sn, ingawa kwa misukosuko,magomvi,migogoro, walikutana wakiwa A\level wakaenda chuo mpaka wakahitimu wako wote,sasa tukio la hivi karibuni ni kwamba walizozana na mkewe,mkewe akadai waachane lakini jamaa akamwambia sioni wala sina sababu ya kuachana na ww, jamaa kaenda mbali zaid akamkumbusha mkewe kumbuka tulikotoka,tuliwahi ishi maisha ya kulala kesho hatujui tunakula nn, bt mkewe haelewi basi jamaa kamwambia mkewe apige simu kwao kwa mama ake na ndugu zake awataarifu kwamba wanatengana na atoe sababu,kwan jamaa yeye alishafka ukwen kwa shinikizo la mkewe na alpokelewa vzuri sn mpaka pa kulala,mama mkwe almkubali sn jamaa,hvyo anahis aibu sn leo aseme anaachana na mtoto wao tena kwa shnkzo la mtoto wao,sasa tokea hyo juz mpaka leo xmass mke hapki wala hafanyi,jamaa yuko njiapanda sana USHAURI WENU WANA MM

Mwambie huyo Jamaa asisubiri Mpaka ashinikizwe kufanya kitu.
Mshauri atangaze ndoa kwa huyo Mwanamke, huenda Mwanamke haioni future na Jamaa baada ya kuwekwa kinyumba miaka mitano bila dalili za ndoa, tena mpaka amshinikize ndiyo Jamaa anaenda Ukweni.
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,136
2,000
Miaka mitano unatumika tu?

Heri ajiondokee aisee

Ukweni kwenyewe kaenda kwa shinikizo? Sio muoaji huyo
 

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,426
2,000
Miaka mitano unatumika tu?

Heri ajiondokee aisee

Ukweni kwenyewe kaenda kwa shinikizo? Sio muoaji huyo

simple mind hizi, hakika hayajakufika kumpa mtu jibu la faster ni rahisi sn, kwaakili yako unaamini huyu jamaa kwasababu hajafunga ndoa basi anamtumia huyo mwanamke? pia hawa watu wameajiliwa mwaka huu mke mwl, jamaa ni records manager wa kampuni fulani,inamaana wamepita vpnd vgumu sn kwa maelezo ya jamaa.
 

Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,136
2,000
Hivi mtu ameshakwambia hakutaki kila mmoja ashike njia yake,unang'ang'ania ili nini?
Ndio uonekane umependa sana au?
Mwambie wakae wajadili future ya mtoto then waagane kwa wema.
Mapenzi hayalazimishwi,yakiisha yameisha.
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
58,523
2,000
kwa mtazamo upi ni girlfriend mkuu? wameishi 5 solid years pamoja, yaani chini ya paa moja na wanamtoto bado tutaiweka kwenye hiyo status mkuu?

Haijalishi umeishi pamoja kwa muda gani mkuu...

Kama mleta mada alivyooleza, kilichofanyika ni mwanaume kutambulishwa tu kwa wazazi wa mwanamke.

Kutambulishana na kuishi pamoja bado hakuhalalishi kuwa watu wawili ni mwili mmoja.
 

Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,136
2,000
Mwambie huyo Jamaa asisubiri Mpaka ashinikizwe kufanya kitu.
Mshauri atangaze ndoa kwa huyo Mwanamke, huenda Mwanamke haioni future na Jamaa baada ya kuwekwa kinyumba miaka mitano bila dalili za ndoa, tena mpaka amshinikize ndiyo Jamaa anaenda Ukweni.

Hapo sasa!
Miaka mitano husikii ndoa hata ikitajwa kwa utani tu?
Nani anataka uchumba ndugu?
 

Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,328
1,500
Miaka mitano. Mtoto mmoja. Ukweni mara moja. Kidato kimoja. Jamaa aseme kuwa anamtumia msichana wa watu. Ndoa si lazima uwe na milioni kumi, hata laki moja inatosha kwa wewe na mkeo kufunga ndoa yenu. Kwa nini yeye alazimishwe kwenda ukweni ili hali unajua ndiyo mke? Nadhani kuna kitu kimejificha. Yawezekana hata huyo mtoto ndiyo chanzo cha yeye kwenda ukweni baada ya kumpa ujauzito huyo mzazi mwenzie wakiwa chuo.

Dada songa mbele hakuna ndoa hapo
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,852
1,250
Haijalishi umeishi pamoja kwa muda gani mkuu...

Kama mleta mada alivyooleza, kilichofanyika ni mwanaume kutambulishwa tu kwa wazazi wa mwanamke.

Kutambulishana na kuishi pamoja bado hakuhalalishi kuwa watu wawili ni mwili mmoja.

labda kwa misingi ya dini mkuu
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,888
2,000
simple mind hizi, hakika hayajakufika kumpa mtu jibu la faster ni rahisi sn, kwaakili yako unaamini huyu jamaa kwasababu hajafunga ndoa basi anamtumia huyo mwanamke? pia hawa watu wameajiliwa mwaka huu mke mwl, jamaa ni records manager wa kampuni fulani,inamaana wamepita vpnd vgumu sn kwa maelezo ya jamaa.

Mbona you are taking it personal?

Kwanza information ziko sketchy, hujasema wamegombana nini! All in all, miaka 5 hajamuoa anasubiri nini? Mshauri ampe mkataba kwanza bibie.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom