Heci
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 3,684
- 6,409
Hii dunia ina watu wa ajabu Sana. Huyu rafiki yangu ana asili ya Mbulu na anaishi Bunju ambako ana mke na watoto wawili.
Last week alinipigia simu mida ya saa kumi na mbili jioni kuwa anataka tuone na yeye amefika jirani na nyumbani kwangu Ununio.
Nikamweleza kuwa nipo home. Nyumba yangu nimejenga vyumba viwili na sebule, choo cha ndani na choo kingine kiko chumbani kwangu, ila kwa kuwa kina hitilafu, na ninaishi peke yangu na Mimi nimekuwa nikutumie public toilet.
Alipokuja rafiki yangu alinieleza kuwa alikuwa ametiwa ndani kwa muda wa siku nne na mke wake akishirokiana na ndugu za mkewe baada ya kumpiga Sana.
Alinieleza mengi ambayo kwa kweli hayakuwa mambo yenye ukweli ndani Yake. Akaniambia amepitia kwangu akitokea Ununio Beach kuchota maji ya Bahari ili akasafishe nyota yake.
Anakaa kwangu kwa siku mbili akidai kwamba huko kwake anahisi upweke kwani mke na watoto wamehanishiwa kwa ndugu wakiogopa jamaa akitoka jela atawadhuru.
Baada ya siku mbili akaondoka, ila nilipoingia bafuni kuoga, sikulukuta dodoki langu. Na nilipompigia simu kuhoji kama amelichukua alikata simu na hapokei tena simu zangu.
Huyu jamaa yeye ni nesi, ila anapenda Sana maswala ya uchawi na ushirikina. Ana mawe huwa anayaweka kwenye kibuyu, akitaka kwenda popote Kwanza lazima amwage mawe hayo na kuyahesabu huku akiongea kikwao, baada ya hapo ndio huamua kwenda ama kutokwenda.
Sasa najiuliza dodoki langu la kujisugulia anaenda kulifanyia nini? Kwangu haingii Mtu, na kila nyumba iliyo jirani na kwangu iko fenced na hatuingiliani