Rafiki yangu ana duplicate

Rafiki yangu ana duplicate

Tusaidie jina la hicho kitabu
Wakati nasoma secondary nilikuwa mtunzi sana wa hadithi za kiingereza, niliwahi kutunga hadithi moja mwalimu wangu aliitumia kufundishia darasani. Ila hii haiwezi kufundishia.
 
Ndio wakat wa likizo coz aliondokaga nacho..af cjasema alikikuta bwenn nmesema alikikuta libraly coz alikua kiongoz wa libraly..
 
Hicho kitabu kinaitwaje, room 2 iko bweni gani? Maana pale ifunda room huitwa kulingana na block iliyopo.
hamna kitu km hicho kila block lina roo 2 yaan mkwawa kuna A2 na B2 na mabwen mengine pia yana mablock yenye roo 2..asa we cjui umesoma ifunda gani..mi nazungumzia ifunda tech na ifunda tech haina cha kusema room 2 iko bwen gan wakat kila bweni lina room 2 mbili..na atuit room 2 tunaita A2 B2 C2 na kuendelea upo hapo..kitabu kinaitwa the magic book..note ifunda kuna vitabu ambavyo ukisema uvitafute madukan hakuna tanzania nzima.
 
Hivo vitabu wazee wazaman walikuwa wanavificha au kuvifukia wanapokaribia umri wa utu zima vinakuwa na siri nyingi na kazi nyingi ila sjajua ni moja ya vitabu vya aina hiyo ama sivyoo ila nikwambie kitu hiko kitabu ni km ni moja ya aina hiyoo mpaka ufundishwe kukitumia na yy huyo Ali alikuwa hajui kukitumia kawaida ya vitabu km hivo km hujui kutumia vinaishara ya kukujuza sikitabu cha kawaida hapohapo unapokisoma unaweza ukahisi chumba kiko juu chini na mengineyo alitakiwa akipotezee tuu nitarudi baadae .........
ofcoz yaweza kua hivyo..mana aliishia tu robo ndo ivyo je angekimaliza c angekua anapaa mchana huku watu wanamtazama duh kudadek.
 
hamna kitu km hicho kila block lina roo 2 yaan mkwawa kuna A2 na B2 na mabwen mengine pia yana mablock yenye roo 2..asa we cjui umesoma ifunda gani..mi nazungumzia ifunda tech na ifunda tech haina cha kusema room 2 iko bwen gan wakat kula bweni lina room 2 mbili..na atuit room 2 tunaita A2 B2 C2 na kuendelea upo hapo..kitabu kinaitwa the magic book..note ifunda kuna vitabu ambavyo ukisema uvitafute madukan hakuna tanzania nzima.

Sijui kwa sasa ila nnachojua ifunda hakuna room 2. Ila kuna hizo ulizotaja, huwa zimekaa kiblock, mfano block A na B na C1 mpaka C3 hili ndio bweni la Mkwawa na mabweni mengine ya milambo,seuta na chaburuma yamegawanywa hivyo. Sasa room 2 sijui labda sinza kule kwa mademu maana sikujui vizuri. Hicho kitabu ngoja nkitafite maana kiambiwa tu mi mbado kuamini
 
Bavaria kwenye likes received una 3583 lakini kwenye likes given una 0!yani hajawahi kutoa like hata moja!!! Ninini hii??? Ni uchoyo au??? Just curious!


Nipe umuhimu wa kutoa likes.
 
Last edited by a moderator:
Pale nlimaanisha "ile naingia chumbani tu nkamkuta ally" room 2 yan chumbani tu..
 
Habar wana JF.

Mimi nilisoma na huyu rafiki yangu shule moja ya kuitwa Ifunda tech, Iringa hiyo. Sasa wakati tuko form three 2011 yeye akagombea uongozi wa library akapata. Sasa ile siku anaenda kukabidhiwa ofisi ilimbidi apange vizuri vitabu kule maktaba ili aanze kazi rasmi ya kuazimisha vitabu.

Katika kupanga akakiona kitabu fulani hivi akakipenda akakiweka pembeni ili badae akisome. Basi kile kitabu akakisoma hadi robo akaona hata hakielewi vizuri akakihifadhi.

Kumbe kile kitabu kadri alivyokua akikisoma ndo alikuwa anazidi kudeviate from normal person. Yaani alikuwa anakutana na vitu vya ajabu pale skuli ila akawa hajatuambia anaficha, ila baadae tukawa hatumwelewi.

Kuna mshikaji akaanza akasema "Mazee huyu Ally mbona simwelewi yaani wakati natoka bombani nikapishana nae anaenda bombani ila nafika huku bwenini namkuta anatokea kwa kule" hah tukabisha bisha palee yakaisha, tulimbeza tukamwambia we macho yako yana makengeza, basi yakaisha.

Sasa kuna siku mimi nilikua natoka masjid naelekea bwenini nikapishana nae yeye alikuwa anatokea bwenini anakwenda masjid. Wala hatukuongea tulipishana tu kwa sababu yeye alikuwa anawahi masjid na mimi nawahi bwenini kujisomea. Kumbuka ilikuwa ni mchana sio usiku.

Sasa mimi ile naingia room 2 namkuta jamaa anapiga story na washikaji, nikamuuliza wewe si tumepishana kule akabisha akasema mimi hapa sijatoka.Tatizo alikuwa anabisha kumbe mwenyewe anajijua ila alikuwa anataka iwe siri.

Basi maisha yakaendelea..

Sasa kuna siku moja tulikuwa mimi na yeye tunatoka bwenini tunaenda masjid usiku saa mbili kuna sehemu kuna mti fulani hivi tulivyofika akaniuliza oya mwana unasikia ngoma zinazopigwa hapo chini ya mti. Haa nikashtuka ngoma tena wakat mti wenyewe hauko porini uko karibu na hiyo njia tunayopita halafu sio mkubwa labda kama mwembe no yaani naona kabisa pale shinani kweupe halafu ananiambia kuna watu wanapiga ngoma!

Tulikimbia kinoma hadi masjid tukapitiliza hadi bombani kuchukua maji ya kutia udhu.. Sasa wakati tuko bombani akaanza kunisimulia vizuri. Akaniambia pale kwenye ule mti kuna watu wafupi sana wanapiga ngoma wanafurahia sheree akaongezea akasema na wewe una kesi pale kwa sababu wakati tunapita ulimkanyaga mtu mmoja pale njiani.

Niliogopa sana yaani nikaona huyu jamaa anaongea vitu gani! Sasa wakati tunarudi nikawa naogopa kishenzi yaani nikawa naenda nae bega kwa bega. Tulivyofika bwenini akaanza kuniambia unajua kwamba tulivyofika pale kwenye mti we ulibaki. Haah! Nikashangaa, nilibaki tena? Akasema ndio na nilikupigia sana kelele kukuita ili unikimbilie usibaki pale ila walikung'ang'ania wale watu.

Akasema nilikuvuta sana ila ilishindikana mimi nikakuacha, akasema ila wewe una nguvu za asili ambazo zilikuwezesha kujing'atua pale na kuanza kunikimbilia na ukanikuta hapa, akanionyesha sehemu nilipomkutia yaani ina maana kuanzia hapo kurudi hadi pale kwenye mti Ally alikuwa anatembea peke yake japokua mimi nilijiona niko nae mda wote.

Akaongeza akasema na usingeweza kutoka pale sijui ingekuaje, dah nikaona huu msala..basi bwana jamaa ikaendaenda siku akaniambia ukweli kwamba chanzo ni kitab, .akaniadithia mambo mbalimbali aliyokuwa akiyaona. Yaani mambo mengi tu akaniadithia siku fulan hivi alikuwa yuko prepo na mshkaj fulani hivi classmate asa wakapiga msuliii mda wa kuondoka yule classmate akamfata ally kwenye kit chake akamkuta amejilaza kichwa kwenye meza akawa anamtingisha huku akimwita aamke wasepe bwenini.

Kumbe Ally alikuwa amekaa kwenye kiti hajalala anamtazama jamaa anamsikiliza anasemaje yaani namaanisha alikuwa hajajilaza kama ambavyo yeye alikuwa anamuona yeye ally alikuwa amekaa tu kawaida kama vile mwanafunzi anaemskiliza mwalimu darasani mfano wake yaani sasa ally akawa anamshangaa jamaa iweje amtingishe anamwamsha wakat yeye yuko anamtazama usoni..dah ally akaamua tu kuinuka wakasepa..

Akaniadithia hadi wa2 anaowaona pale skul ambao cc hatuwaon..akaniadithia cku ile alvokua anafundishwa na jamaa flan iv anaitwa mapper ilkua ucku km sa nne iv walkua wanapigia pindi mesini..kumbe jamaa anafundisha anadhani yuko na ally kumbe mwenzie zamaan keshaondoka kuelekea kwenye kikao kumbe sku hiyo kulikua na mkutano ni mbali kdogo kutoka apo skul yan km unaelekea kwenye makaz ya raia ila yeye alijiona tu anakwenda hata hajui anakwenda wapi na yule mapper anaendelea kufundisha kivuli..jamaa anakwambia kufka kule akakutana na boys wengi tu nawao wamekuja kwenye iko kikao...

Bac yule mkuu akatoa nasaha zake pale afu wakaruhusiwa..akaniambia miongon mwale boys alowaona mmoja ni rafki yake huko singida alikotoka kumbuka hapo ni iringa..anakutana na watu wa singida tena ktk kikao cha dakika kumi tu af kila mtu anarud kwao..bac jamaa akarud akaendelea na pindi...

Sasa wadau nataka mtoe maoni yenu haya mambo yanakuajekuaje mana mi had leo sielew yani coz jamaa alikua na uwezo ad wa kuyayuka yan..na kile kitab pia anasema alikua akikiweka sehem anakikuta kimehama kipo sehem nyingine..

Hebu toeni coment zenu wadau mi had leo cjaelewa yan.. Mi niishie tu hapo mana naona hizi namba za herufi nazotakiwa kuandika zinaisha.

Karibuni wadau mseme chochote.

Duh!!!hapo ulipo na wewe ni jini ambae hujatimia.bada ya miaka mitano utakua jini kamili.tafadhali wahi dua kabla ya muda huo!
 
Back
Top Bottom