Rafiki yangu amevunja uchumba wangu

Rafiki yangu amevunja uchumba wangu

Hbr wana MMU ?

Bila kupoteza muda niende kwenye mada. Naandiki nikiwa na uchungu mkubwa sana moyoni mwangu.

Ilikuwa tarh 2/1/2019 siku moja tu baada ya mwaka mpya nilirudi nyumba nikitokea Nairobi nilipokwenda kwa shughuli zangu binafsi, nilipofika home nikaoga na kuamua kutoka kwenda nyumbani kwa mpenzi wangu. Huyu mpenzi wangu tulikuwa tumeshaenda mbali sana kiasi cha kuwa nimeshalipa na mahali kwao.

Sikutaka kumpa taarifa kama nimerudi ili nimfanyie surprise kama mjuavyo tena surprise ni kitu cha kawaida kwa wapenzi.

Nilibeba vijizawadi ambavyo nilimnunulia nilipokuwa Nairobi, nikashika njia huyo mpaka home kwake, ilikuwa inaelekea saa tatu usiku Mara huyo nikafika. Nilipokelewa na house girl.

Nilipoingia sebuleni tu house girl akaninong'oneza kuwa mtu yupo chumbani na mpenzi wangu.
Sikuamini Maneno yake nikaelekea chumbani kwa speed kujaribu kufungua mlango ulikuwa umefungwa nafunguo, nikaamua kugonga ilichukua muda kidogo mpaka mlango unafunguliwa.

Alipofungua mlango tu mm nikamsukuma nakuzama ndani, wakati huo yeye alikuwa na kanga moja tu, mara nikakutanisha uso na rafiki yangu kipenzi akiwa kajilaza kwenye Kitanda cha mpenzi wangu huku akiwa kajifunga taulo ambalo huwa nalitumia mm nikilala kwa mpenzi wangu.

Sikuamini macho yangu, nilisimama kwa dakika kadhaa nikiwa sijui cha kufanya baadae nikaamua kuondoka bila ya kusema neno.

Baada ya kuondoka mpenzi wangu alinipigia simu kwa kweli sikupokea alipiga mpaka akachoka. Siku moja baada ya tukio aliamua kunifuata home hakuja peke yake alikuja na wazazi wake kwa kweli niliwafukuza sikuwa tayari kuongea lolote.

Baada ya wiki kupita niliitwa na mshenga akaniuliza kilichotokea nilimueleza kila kitu alichonijibu kama hayo ni kweli huyu hakufai tena .

Alinishauri nikutana naye mbele ya wazazi wake nimpe msimamo wangu, sikusita nilikutana nao nikawaeleza kuwa sitaweza kuendelea tena na binti yao. Mambo yakawa mengi wakaanza kunisihi nisamehe kwa kweli nilishindwa nikainuka na kusepa zangu.

Tangu siku ile wananisumbua sana kila siku kunitumia watu ili niendelee na binti yao kiukweli siwezi kuwa mnafiki moyo wangu hauwezi hili kbsa. huwa sina unafiki kabisa.

Mimi ni mwamnifu sana sijawahi kuwa na mahusiano nje yake iweje Leo yeye anifanyie hivi?

Rafiki yangu kweli umeamua kunifanyia unyama huu woote? Hukumbuki fadhira zangu? Bila Mimi ungekuwa hivyo? Ungekuwa hapo ulipo?

Nimeandika haya kwa lengo la kuwashirikisha ili nitue mzigo wa uchungu nilionao moyoni mwangu.

Sina mpango naye tena hata aje nani.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hilo hata mie nimewahi kufika stage ambayo ilibaki nikufunga ndoa tu. Nilikuwa mbali simu yake ikawa haipatikani kwa siku kama 3 hivi. Akanitafuta kwa namba nyingine akaniambia kapoteza line ila simu anayo. Nikajiuliza unapotezaje line unabaki na simu kwanini visipotee vyote? Nikawa naendelea kuipiga ile namba siku moja ikaita na akapokea mwanaume baada ya mahojiano akasema ni simu ya mpenzi wake. Siku hiyohiyo ndio ikawa kwaheri japo yeye na ndugu zake walishawishi lakini ilishindikana. Baada ya miezi 3 ikagundulika ana mimba ikawa hakuna tena wa kunishawishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marafiki huwa wanafiki sana ndo mana siku hizi huwa sipendi marafiki wengi kabisa, nimewahi kuwa na washkaji ambao nilihisi ni tumeshibana lakini nyuma ya pazia wanamtongoza msichana wangu na kumwambia mimi malaya hamna sketi inanipita asee bahati yule dada ananijua vizuri sana akaniambia babe niliyoambiwa siwezi kuyaamini sababu nakujua labda wangeongea lingine, nilichofanya ni kuwafungia vioo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni makosa ya kibinadamu mkuu. Mwanamke naye ni binadamu. Km mwanaume anavokutwa na mchepuko anaomba msamaha kwamba ni shetani kampitia sasa mbona mwanamke anaonekana ni shetani herself?

Ukiwa sio mtu makini dunia ya sasa utakufa mapema sana mtu akabebe magonjwa huko aje akuambukize kiurahisi tu. Kwa kifupi mtu ambae amelala na rafiki yako chumbani kwake halafu ww uje umuoe utakuwa huna akili nzuri
 
kilimatinde wewe ndiyo mwanaume wa kweli. Hakuna kumumunya maneno. Cha msingi kimila warejeshe magari hata kama ni sent 5 ili kuweza kuvunja UHUSIANO ili pia uweze kulipa mahari mke mwingine. Kwetu ukilipa mahari mahari ikitokea mmeachana bila kufunga ndoa au hata kuishi pamoja mkazaaa basi hutaweza kulipa mahari kwa mwanamke mwingine.
 
Sasa mkuu uamuzi c umeshaufikia hizi ngonjera zoote za nn mm nikajua unataka wanajamvi wakushauri kumbe unataka usifiwe cjui ama nn,,,any way hakuna namna ila nani anauhakika na haya maelezo yako,,ila tu nikwambie wanawake asilimia kubwa saiv wanamegwa tu awe mke wa mtu au mchumba wa mtu ,,cha msingi elewa hcho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom